Wakongo wa Uingereza wasaidia watoto!!


Jamii ya watu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaoishi nchini Uingereza wamezindua kampeni maalum mjini London, iitwayo Congo Unite.

Lengo ni kuchangisha fedha ili kuwasaidia watu wenye maradhi ya selimundu (sickle cell) na watoto walioachwa yatima kutokana na maafa ya vita nchini Congo.

Kampeni hiyo imeanza kwa uzinduzi wa mkanda maalum wa video na CD za wimbo maalum uitwao Congo Unite ulioimbwa kwa kuwashirikisha wasanii mbalimbali wa Congo wanaoishi nchini Uingereza.

Video hizo zitauzwa duniani kote kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia mpango huo.
Kampeni hii imepewa jina la Congo Unite ikiwa ni wito kwa raia wote wa Congo duniani kusahau tofauti zao na kuungana na kushirikiana kwa pamoja katika kujaribu kusaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili raia nchini humo.

Kampeni hii imeanza kwa kulenga kuwasaidia watu wanaokabiliwa na ugonjwa wa selimundu, watoto yatima na matatizo mengine yatokanayo na maafa ya vita.

Akizungumza na BBC mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa CONGO50 ambaye pia ndiye aliyeongoza utengenezaji wa video hiyo ya Congo Unite amesema mbali na kutumia fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya CD na Video hizo kutumika kusaidia waathirika wa selimundu, wanategemea pia kuanzisha kituo cha kulelea watoto yatima nchini Congo.

Naye mratibu wa kampeni hiyo, Mimi Zabu Litambola, amesema moja ya mambo yanayotiliwa mkazo ni kukusanya fedha ili kutafsiri vitabu na maelezo kuhusu ugonjwa wa selimundu kutoka lugha ya kiingereza kwenda katika lugha zote zinazutumika nchini Congo.

Hatua hiyo itaiwezesha jamii ya Congo kupata elimu ya kutosha juu ya ugonjwa huo.
Kampeni ya Congo Unite ni moja ya mipango iliyoandaliwa na raia wa Congo nchini Uingereza katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

JESHI LA WANANCHI LASIKITISWA NA KUONDOKEWA NA MARUBANI WAKE!!

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Banda lao katika Maonesho ya

Biashara ya Kimataifa jijini Dar leo. Aliongelea pia juu ya ajali ya ndege yao iliyotokea jana, eneo la Kabuku, Kijiji cha Manga mpakani mwa mikoa ya Pwani na Tanga.Marubani waiwili wa ndege hiyo walifariki.

TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR YAPATA KOCHA KUTOKA UINGEREZA!!

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Zanzibar, Stewart Hall, kutoka Uingereza akisaini mkataba wa miaka mitano wa kuifundisha timu hiyo katika hafla iliyofanyika kisiwani. kushoto kwake ni Rais wa Shirikisho la Soka la Zanaibar (ZFA) Ali Ferej Tamim

SERIKALI YAONGEZA MUDA WA KUSAJILI SIMU ZA MKONONI!!

NA MAGRETH KINABO NA BENJAMIN SAWE MAELEZO-DODOMA


SERIKALI imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani ili kuwezesha wananchi wengi waweze kujisajili baada ` kusikiliza kilio chao ili kuwapa fursa zaidi ya kujisajili.
Hayo yalisemwa jana Bungeni na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msollla wakati akiwasilisha hotuba yake ya makadrio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo. “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu imesikia kilio cha wananchi wengi.


Imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani hadi Julai 15, mwaka huu baada ya hapo simu zote ambazo hazijasajiliwa zitafungwa,” alisema Profesa Msolla .
Aidha Waziri Msolla alisema jumla ya kampuni 14 hadi sasa zimepewa leseni ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu. Aliongeza kuwa idadi ya watumiaji wa simu kwa kigezo cha njia za simu (line) zinazotumika imefikia 18,207,390, hivyo idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 400 ikilinganishwa na watumiaji 3,542,563 waliokuwepo mwaka 2005.


Alisema idadi ya simu za mezani hadi sasa ni 174,800 ilinganishwa na 154,420 zilizokuwepo mwaka 2005. “Hii ni sawa na ongezeko la la asilimia 13.2 . ukuaji huu umepanua wigo wa mawasiliano ya simu na kuongeza huduma nyingine zinazoendana na matumizi ya simu hapa nchini Alizitaja huduma hizo kuwa ni upatikanaji wa taarifa, huduma za mtandao, ulipaji wa Ankara za simu, maji, umeme na huduma za kibenki. Awali Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kuwa nambazote za simu za mkononi zisajiliwe kati ya Julai 1, mwaka 2009 hadi Desemba 31, mwaka 2009.


Awali mamlaka hiyo iliongeza muda wa mara ya pili wa miezi sita wa kusajili simu hizo, kuanzia Januari mwaka 2010 hadi Juni mwaka huu baada ule wa kwanza kuonyesha watu wengi walikuwa hawajajisajili.

DEMOKRASIA MAKINI WATOA RATIBA ZOEZI LA UCHAGUZI MKUU UJAO!!

Chama cha Demokrasia Makini makao makuu kinatoa taarifa kwa wanachama na wapenzi na umma kwa ujumla kuwa ratiba ya kuchukua fomu kwa ajili ya wagombeakatika nafasi za udiwani, ubunge na urais zitaanza kutolewa tarehe 1/7/2010 na kurudiswa tarehe 25/7/2010 tarehe 26/7/2010 hadi tarehe 10/8/2010 kura za maoni zitafanyika Bara na Visiwani .
Tarehe 12/8/2010hadi 16/8/2010 zitakuwa ni siku za kusikiliza rufaa tarehe 17/8/2010 ni siku ya uteuzi wa wagombea tarehe 19/8/2010 itakuwa ni uteuzi wa wagombea kwa tume taifa ya uchaguzi.
Na tarehe 20/8/2010 hadi tarehe 30/10/2010 zitakuwa ni siku za kampeni kwa wagombea wote tarehe 31/10/2010 ni siku ya upigaji kura, wote wenye mapenzi mema na chama hicho wanakaribiswa kuchukua fomu na kugombea katika nafasi hizo.

BENDERA - TANZANIA YARUDISHIWA UANACHAMA MCHEZO WA NGUMI


NA MAGRETH KINABO NA BENJAMIN SAWE- MAELEZO, DODOMA

SERIKALI imesema kwamba Shirikisho la Ngumi za RidhaaTanzania (BFT) imerudishiwa uanachama wake katika Chama cha Ngumi Dunaini(IFB),hivyo tayari ina timu ya ngumi na imeaajiri makocha kutoka Cuba kwa ajili ya maandalizi ya Olimpiki yatakayofanyika nchini India. Aidha Serikali imesema kuwa timu hiyo pia itashiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Uingereza.

Hayo yalisemwa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo , Joel Bendera wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge Nantumbo (CCM)Vita Kawawa liliouliza kuwa na nini hatima ya BFT baada ya viongozi wake kukumbwa na kashfa ya dawa za kulevya. Waziri Bendera akijibu swali hilo alisema Serikali baada ya kuona mchezo huo ni muhimu imejitahidi kuomba chama cha IFB kuirudisha uwanachama wake Tanzania ,hivyo sasa hivi timu ya ngumi na chama hicho, kimerudishiwa heshima yake na mchezo huo unaendelea wakati kesi iko mahakamani.

Akijibu swali lingine la nyongeza la Mwanawetu Zarafi , Mbunge wa Viti Maalum (CUF) lililouliza kuwa kuwafundisha watoto mchezo huo ni kiunyume na sheria na ni wa hatari , Waziri Bendera alisema kiutaratibu mchezo huo au wa aina yoyote unafundishwa katika ngazi ya utoto.

Hivyo hata siku moja huwezi ukamfundisha mtu aliyekomaa mchezo kwa sababu ataumia. Aliongeza kwamba kitaalamu unaanza ngazi ya utoto na mashindano hayo yako katika umri mdogo pia. Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maaalum Lucy Owenya alilioliuza kuwa ni taasisi zipi zinazoratibu mchezo wa ndondi alisema zipo taasisi mbili,ambazo ni Chama Cha Ndondi za Ridhaa(BFT) na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa(PST).Mwisho.

REDDS MISS KINONDONI WATEMBELEA FREE MEDIA!!

Mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima linalochapishwa na kampuni ya Free Media Absalom Kibanda akiongea na warembo wanaoshiriki katika shindano la Redds Miss Kinondoni wakati warembo hao walipotembelea chumba cha habari cha gazeti hilo mchana huu katika ofisi zao zilizopo mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam.
Ziara hii ya warembo ni ya kimafunzo kabla hawajapanda jukwaani julai 2 kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa katika utayarishaji wa gazeti hilo.
Warembo hao wanatarajiwa kuchuana katika kinyang'anyiro kitakachofanyika ijumaa wakiwania taji hilo kwenye ukumbi wa Mlimani City uliopo Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es salaam, katika shindano hilo burudani itatolewa na vijana machachari kutoka kundi la THT la jijini Dar es salaam pamoja na Sebene la kukata na shoka kutoka kwa vijana wa African Stars wana wa (Kutwanga na kupepeta).
Mhariri mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda katikati akimtambulisha Kaimu Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo Ansbert Gurumo kushoto kwa warembo wa Redds Miss Kinondoni waliotembelea ofisi za gazeti hilo leo mchana.

MOHAMMED DEWJI AZINDUA MRADI WA KUTOKOMEZA MALARIA SINGIDA!!


Katika Hotuba ya Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida mjini alikuwa na haya machache ya kusema kwa Wanachi wake “Ndugu Zangu pamoja na mambo mengine leo hii nimekuja katika ziara ya kawaida ya kuhamasisha maendeleo ndani ya jimbo langu.

Lakini kama mtakumbuka niliwaandikia barua maafisa watendaji wa vijiji waniorodheshee majina ya mama wajawazito pamoja na watoto walio na umri chini ya miaka 5 ili nije niwapatie vyandarua vyenye dawa”.MO aliendele kusema “Ikiwa hii ni awamu ya pili kwani kwa awamu ya kwanza nilitoa Vyandarua zaidi ya 6,000 ndani ya vijiji vyetu 19 vya manispaa,mwaka 2007.

Ndugu zangu lakini mnaweza kujiuliza kwa nini nimelenga makundi haya,nimelenga makundi haya kwa sababu ugonjwa wa malaria bado unaongoza kwa kuuwa watu wengi mpaka sasa,tofauti na magonjwa mengine,Na takwimu zinaoonyesha,wanaoathirika zaidi na gonjwa hili la malaria ni mama wajawazito na watoto wenye Umri chini ya miaka 5,Takwimu zinaonyesha kuwa katika kila watoto 100 watoto watano wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria”MO alizidi kusisitiza.

Ndugu zangu sasa mimi kwa kutambua hili tatizo,nimeona bora nihamasishe jamii itambue umuhimu wa kutumia vyandarua vyenye dawa ya Kinga,nasisitiza kuwa hii ni hamasa tu,pia nawaomba viongozi wenzangu tushirikiane katika kutoa elimu juu ya matumizi ya Vyandarau”alisema MO.Mbali na MO kutoa vyandarua 6000,Kampuni ya simu za Mkononi Vodacom Tanzania Kitengo cha Vodacom Foundation kimetoa Vyandarua 10,000 jimboni kwa Mh.Mohammed Dewji hii yote ni kupambana na vita dhidi ya Malaria.

TAX ZOTE JIJINI DAR ES SALAAM KUHAKIKIWA!!

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Teksi nchini Tunawajali Group Bw. Abeid Chenbe akionyesha cheti chao cha usajili kutoka BRELA wakati alipokuwa akizungumza na waandiishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusu mpango wao wa uhakiki wa teksi nchini unaoanza kesho tarehe 1 Julai ambapo teksi zote zitakaguliwa ubora na kisha zitalipiwa kodi zake na kuwekewa stika yenye picha ya teksi iliyoandikwa
(Teksi Salama Tanzania)

LIGI YA MUUNGANO KIKAPU KUFANYIKA JULAI 3-9 MWAKA HUU

Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini (TBF) Alexander Msoffe akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo asubuhi hii jijini Dar es salaa wakati alipokuwa akitangaza kuanza kwa ligi Muungano katika mchezo huo inayotarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar kuanzia Julai 3-9 mwaka huu. ambapo itashirikisha timu nane kutoka bara na timu nane kutoka visiwani, ambapo mgeni wa heshima atakuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhan.
Timu zinazotarajiwa kushiriki ligi hiyo kwa wanaume na wanaume ni Savio,JKT, Oilers, Mzinga Corporation wanaume, wanawake ni Jeshi Stars Police Dar es salaam Lioness na CMTU.
Kwa upande wa Zanzibar timu za wanau ni Stonme Town, Kisima Majogoo, Rangers, Tornardo, na wanawake ni Jeshi , JKU na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.
Katika picha kushoto ni Afisa habari mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Mwirabi Cisse.
Mike Maluwe katibu mkuu wa TBF akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es salaam kushoto ni katibu mkuu wa TBF Alexander Msofe.

VODACOM FOUNDATION YAKABIDHI VYANDARUA HOSPITALI YA IRAMBA SINGIDA!!

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (kushoto) akimkabidhi moja ya kati ya Vyandarua 1,300 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba iliyopo Kiomboi DK.Anthony Mburu (katikati)Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Peter Mwagiro akishuhudia upokeaji huo wa Msaada ambao watagawiwa wagonjwa wote waliopo eneo hilo.
Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi moja kati ya 1,300 Esta Aron akiwa na mwanae mwenye umri wa miezi 6 Peter William ambaye ni mmoja wa Wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya akina mama katika hospitali ya Wilaya ya Iramba ilioko Kiomboi Singida mfuko huo ulitoa msaada wa jumla ya Vyandarua 1,300 katika mkoa huo.

NYAMA CHOMA NA CHIPSI KIDOGO "SAAAFI SANA"

Mwigizaji wa filamu JB kushoto pamoja na mdau Daud Mambya wakichekelea chipsi mishikaki waliyokuwa wakijichana mara baada ya kugundua kuwa Camera ya FULLSHANGWE ilikuwa ikirekodi tukio hilo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Waziri Mkuu wa Kenya afanyiwa upasuaji!!


Daktari wa Waziri Mkuu Raila Odinga, Oluoch Olunya, amethibitisha kuwa Odinga amefanyiwa upasuaji katika ubongo wake baada ya kubainika kuwa kulikuwepo na shinikizo kubwa katika kichwa chake.

Daktari Olunya aliyekuwa akihutubia waandishi wa habari kuhusiana na kulazwa kwa Waziri Mkuu katika hospitali ya Nairobi, amesema kwamba Waziri Mkuu aliwaambia kuwa aligonga kichwa chake kwenye gari lake majuma matatu yaliyopita.

Mtaalamu huyo wa upasuaji wa ubongo amesema kuwa Odinga anaendelea kupata nafuu na kwamba ameweza kukaa kwa urahisi katika chumba chake hospitalini.
Muuguzi huyo pia amesema Raila ana uchovu mwingi mwilini na anahitaji kulazwa kwa siku tano zijazo.

Awali taarifa kutoka kwa ofisi yake ilidai kwamba alikuwa na uchovu tu.
Bwana Odinga alipelekwa hospitalini Jumatatu mchana baada ya kushiriki mkutano wa kisiasa na madaktari wake waliamuru apumzike hospitalini.

Hadi sasa Raila Odinga mwenye umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mkakamavu.
Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya kiafya.

Taarifa ya kupasualiwa kwake imewashangaza wengi.
Hadi sasa , maswali mengi kuhusu afya ya kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa rais Mwai kibaki.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi. Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya. www.bbcswahili.com

Nane bora zimefahamika kombe la Dunia!!


Jumatano na Alhamisi ni siku za mapumziko, kabla ya michuano ya kwanza ya robo fainali kufanyika siku ya Ijumaa.
Nafasi mbili za mwisho za robo fainali zilichukuliwa na Paraguay na Uhispania kufuatia ushindi kwenye mechi zao Jumanne.
Paraguay ilipata ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Japan kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare 0-0 katika muda wa kawaida na pia muda wa ziada, kwenye uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria.
Tuta la Yuichi Komano wa Japan liligonga mwamba huku Paraguay wakifanikiwa kufunga penalti zao zote.

Uhispania ilifanikiwa kuifunga Ureno bao 1-0 katika uwanja wa Green Point mjini Cape Town, bao lililofungwa na David Villa katika dakika ya 68.
Sasa Uhispania inasubiri kuchuana na Paraguay katika robo fainali.

Mechi ya kwanza ya robo fainali siku ya Ijumaa itakuwa kati ya mabingwa mara tano Brazil na Uholanzi katika uwanja wa Nelson Mandela Bay, mjini Port Elizabeth.

Robo fainali nyingine siku hiyo ya Ijumaa itakuwa kati ya Ghana na Uruguay katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg,hii ikiwa ni mara ya tatu katika historia ya Kombe la dunia kwa timu kutoka Afrika kufikia hatua ya nane bora.

Itakuwa ni fursa nyingine ya wapenzi wa soka barani Afrika kuungana tena kuishabikia Ghana, kama ilivyofanyika wakati wa mchuano kati ya Black Stars na Marekani.
Siku ya Jumamosi itafanyika robo fainali ya tatu kati ya Ujerumani na Argentina katika uwanja wa Green Point, mjini Cape Town.

Paraguay na Uhispania zitachuana katika robo fainali ya mwisho siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Ellis Park, mjini Johannesburg.

Nusu fainali zitachezwa Jumanne na Jumatano wiki ijayo mjini Cape Town na Durban.
Mshindi wa tatu atafahamika Jumamosi tarehe 10 zitakapokutana timu mbili ambazo zitakuwa zimepoteza kwenye nusu fainali.

Jumapili tarehe 11 ndio fainali itafanyika katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg na bingwa mpya wa dunia kutawazwa.
Mechi za robo fainali zinazotazamiwa kuwa ngumu zaidi ni ile kati ya Brazil na Uholanzi siku ya Ijumaa, na pia Ujerumani dhidi ya Argentina siku ya Jumamosi.

Brazil wameonyesha azma ya kulitwaa kombe hilo kwa mara ya sita katika mechi ambazo wamecheza, lakini Uholanzi nao wanapania kumaliza kiu ya miaka mingi ya kombe hilo, baada ya kucheza fainali mara mbili bila mafanikio.

AJALI YA NDEGE KATIKA PICHA ILIYOTOKEA HUKO MANGA MKOANI TANGA!!

Sehemu ya ndege iliyopata ajali baada ya kutua barabarani kwa dharura na kugonga basi la watalii ambalo linaonekana juu kushoto likiwa limeanguka
Ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikosi cha NGERENGERE ikiwa imeanguka na kuligonga basi la watalii waliokuwa barabarani katika eneo la MANGA mkoani TANGA na kusababisha rubani WAWILI wa ndege hiyo kupoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa rasmi, ndege hiyo yenye namba 9119 ilikuwa katika mazoezi.

Taarifa hiyo imesema askari wa JWTZ na polisi walifika eneo la tukio kwa ajili ya kuondoa ndege hiyo ambayo ilikuwa imelala katikati ya barabara na kuzuia magari ya kutoka ama kwenda Dar, Tanga na Arusha kwa masaa kadhaa. Picha na mdau Peter Mwakabwale. (Picha kwa hisani ya Michuziblog)

Askari wakagua na kusimamia ulinzi katika eneo la ajali


BAKWATA YATOA TAMKO KUHUSU MAHAKAMA YA KADHI

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa shaaban Simba (katikati) leo ametoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi nchini Tanzania, akiwataka waislamu wote nchini kufanya subira wakati majadiliano kati ya wanasheria wa Kiislamu na waserikali wakiendelea na majadiliano juu ya suala hilo.

KCB yatoa punguzo la bei ya hisa!!

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Joram Kiarie, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi na kutambulisha huduma mpya yakutoa punguzo la bei ya Hisa kwa wanahisa wa benki hiyo, na mtandao wa kutoa huduma kwa wananchi wa Afrika Mashariki na Kati, ambapo mteja wa benki hiyo anaweza kutoa pesa za nchi aliyopo.
BENKI ya KCB Tanzania imezindua promosheni ya kuuza baadhi ya hisa zake chini ya bei ya awali lengo likiwa ni kukuza kiwango cha mtaji wa kampuni hiyo kubwa kanda ya Afrika Mashariki ikiwa rasilimali ni dola za Kimarekani 2.6.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uuzaji huo wa hisa mshauri wa masuala ya kibiashara wa benki hiyo Amish Gupta alisema kwamba mpango huo mahususi umekuja ili pia uwawezeshe wanahisa wa KCB kununua hisa nyingi za benki hiyo.

Akifafanua Gupta alisema kuwa kwa sasa wateja, wadau na wanahisa wa benki hiyo watanunua hisa moja ya KCB Tanzania kwa bei 310/- kutoka 385/- bei iliyokuwa ikitumika katika kipindi cha wastani wa miezi sita iliyopita punguzo likiwa ni sawa na asilimia 21.

“Mpango huu unaotarajiwa kuanza rasmi Julai moja utakamilika Julai 23 mwaka huu na kwamba wanahisa waliofanikiwa kununua hisa za benki yetu kupitia kwa mwaka huu,” alisema Gupta.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa wakala wetu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa punguzo la bei watatajwa Agosti 5 alisema hisa zitakazonunuliwa zitatumika katika nchi zote ambako benki hiyo inatoa huduma na zinauzwa kwa wananchi wote hata waso wateja wa benki hiyo.

Alisema pesa zitakazokusanywa zitatumika kupanua wigo wa utoaji huduma nchini na sio kwenye matawi ya nje ili kuongeza kiwango cha utoaji mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na uendelezaji wa makazi.

Appiah: This team is special!!

After a few days of reflection on their historic second-round victory over USA, Ghana captain Stephen Appiah told FIFA that the Black Stars are staying themselves: relaxed and happy to be together. Having now gone further in the FIFA World Cup™ than ever before, and with a tricky match with Uruguay up next on Friday, the Bologna midfielder reflected on the values of what he calls "a special team".

"I am warmed by the players," said the 29-year-old from the team's camp outside of Rustenburg. "You can see that there is no tension, no pressure. Always with smiles, singing and laughing – stuff like that. What I've learnt is the more pressure you put on yourself, the more things go wrong. So, I have been telling the guys that they should be free [and that] nobody should even think about the games. Maybe a day or two before, then we have to focus on the game. But, for now, we're relaxed, training, laughing, singing, dancing. I think that's very important."

Handling the world's biggest football tournament in this way has been a consistent refrain from the Black Stars in South Africa. As they were four years ago on their finals debut, Ghana are the only African representatives in the knockout rounds, so they are obviously doing something right. And as anyone who has seen the joy and unity in their post-match celebrations can attest, togetherness is one of the team's hallmarks – not just in word but in spirit.
More story www.fifa.com.

Waziri Mkuu wa Kenya alazwa hospitalini!!


Hadi sasa Raila Odinga mwenye umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mwenye nguvu.
Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya kimwili.

Kwa hiyo taarifa iliyotolewa hii leo na msemaji wake imewashangaza wengi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo madaktari wameamuru Odinga alazwe hospitalini kwa muda wakisema tu kwamba ana uchovu.

Cha kukanganya ni kwamba taarifa hiyo iliwanukuu madaktari hao pia wakisema Odinga ana uwezo wa kufanya kazi kama kawaida ikiwa atajisikia kufanya hivyo. Japo hawatamruhusu kufanya hivyo.

Hadi sasa, maswali mengi kuhusu afya ya kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa Rais Mwai kibaki ambaye baada ya uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi.

Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya.

Rais wa East Africa Speakers Bureau azungumzia siku ya wajasiliamali!!

Rais wa East Africa Speakers Bureau, Paul Mashauri (kushoto) akiongea wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu siku ya Wajasiliamali itakayofanyika Julai 20 katika Viwanja Vya Karimjee jijini Dar es Salaam chini ya Udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania. Kulia ni Meneja Mauzo wa Zain Zedi Seleman.

Blatter aomba radhi kwa makosa ya waamuzi!!


Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter ameomba msamaha kwa ajili ya makosa yaliyofanywa na waamuzi kwenye Kombe la Dunia, ambapo bao llilofungwa na Frank Lampard wa England dhidi ya Ujerumani lilikataliwa, na pia kukubaliwa kwa bao la kuotea lililofungwa na Carloz Tevez wa Argentina dhidi ya Mexico.

Bwana Blatter amesema mdahalo kuhusu haja ya kutumia teknolojia kubaini iwapo mpira umevuka mstari wa goli au la utaanzishwa upya kwenye mkutano wa bodi ya kimataifa ya vyama vya soka utakaofanyika mwezi Julai.

Mkutano wa bodi hiyo uliofanyika mwezi Machi uliamua kukataa kutumika kwa teknolojia hiyo kwenye Kombe la Dunia, kwa tetesi kwamba kusimamisha mechi kwa ajili kuthibitisha kwenye video ikiwa mpira umevuka mstari au la kutaathiri mtiririko wa mchezo na pia kuzinyima timu fursa ya kufunga.

Mjadala kuhusu haja ya kutumika kwa teknolojia hiyo uliibuka tena siku ya Jumapili wakati Ujerumani ilipoifunga England mabao 4-1 mjini Bloemfontein na kuiondoa kwenye mashindano.
Kwenye mechi hiyo, mwamuzi kutoka Uruguay Jorge Larriando na msaidizi wake walikataa kutambua kwamba mpira uliopigwa na Frank Lampard katika dakika ya 38 ulivuka mstari wa lango la Ujerumani na kuingia kabla ya mlinda mlango kuuondosha.

Bao hilo lingeiwezesha England kusawazisha kabla ya mapumziko.
Baadaye siku hiyo katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg kulitokea utata mwingine kwenye mechi kati ya Argentina na Mexico.
Mwamuzi aliruhusu bao la kwanza la Argentina lililofungwa na Carlos Tevez akionekana kuwa ameotea.
Kulitokea mabishano makali uwanjani wakati wa mapumziko baada ya tukio hilo kuonyeshwa tena kwenye skrini kubwa ndani ya uwanja.
Blatter amesema amezungumza na vyama vya soka vya England na Mexico na kuomba msamaha.

AJIRA MILIONI 1.3 ZAPATIKANA: MAKONGORO MAHANGA!!


MAGRETH KINABO NA BENJAMIN SAWE MAELEZODODOMA.

SERIKALI imesema kwamba jumla ajira 1,313, 561 zimepatikana katika kipindi cha mwaka 2006 hadi kufikia Desemba mwaka 2008 kwa sekta binafsi na Aprili mwaka huu kwenye sekta ya umma, ambapo sekta ya isiyorasmi inaongoza kwa asilimia 81.7 ya ajira zote.

Aidha katika sekta hiyo iliyoongoza wananchi wamejihusisha zaidi kwenye shughuli kama vile biashara ndogondogo na utoaji huduma. Hayo yalisemwa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Dk. Makongoro Mahanga wakati akijibu swali na Mbunge wa Bumbuli(CCM) William Shellukindo lililouliza kuwa ni maeneo gani ambayo yameongezeka ajira kwa asilimia katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Akijibu swali hilo , Dk. Mahanga alisema ongezeko la ajira kwenye sekta isiyorasmi kunachangiwa na sababu ya urahisi wa kuanzisha shughuli ndogondogo ambazo zinahitaji mtaji mdogo, urahisi wa upatikanaji wa maligahafi, miradi kumilikiwa na kaya, mahitaji ya teknolojia taaluma na ushindani .

Alisema sekta binafsi inaongoza kwa kutoa ajira 1,185,387 sawa na asilimia 90.2 na Serikali imetoa ajira mpya 128,174 sawa na asilimia (9.8). Dk .Mahanga alizitaja sekta nyingine zilizozalisha ajira mpya ni ujenzi kwa asilimia 9.31 y a ajira zote, ikifuatiwa na elimu asilimia 2.97, afya asilimia 2.89, usafirishaji na mawasiliano asilimia 1.22, huduma za asilimi 0.61. Aliongeza kwamba mchanganuo wa ajira mpya kuhusu kilimo, uvuvi na ufugaji kiasilimia zinatarajiwa kutolewa mara baada ya zoezi la uchambuzi wa sensa ya kilimo iliyofanyika mwaka 2009 kukamilika. Naibu Waziri huyo alisema Serikali inategemea kufanya utafiti kuhusu kuhusu ajira gani zenye mvuto zaidi kwa Watanzania.

Bonanza Nyama Chabezi Tegeta Jumapili,Vimwana wa Mashujaa kupamba jukwaa!!


Bendi ya Mashujaa Musica (Watoto wa Cash Lady) siku ya jumapili itashuka katika viwanja vya Nyama Chabezi Tegeta kutumbuiza wakati wa Bonanza litakaloshirikisha vikundi mbalimbali vya Viduku, na Michezo ya watoto ikiwa ni pamoja na Pool, kuvuta kamba michezo yote itaanza saa nane mchana ikiwa ni pamoja na michezo ya watoto ya kukimbiza Kuku na watoto kushindana kucheza makirikiti.

Burudani hiyo itaanza saa nane mchana ambapo Mashujaa Musica watatumbuiza chini ya wanamuziki wake wote akiwemo Rapa Mahili Ibrahim Milinda Nyeusi(Vuvuzela), Kiongozi wa Bendi Jado Fidifosi, Mtalaam wa Masauti Pasia Budance na Raja Rada. Kwa mujibu wa msemaji wa Mashujaa musica, Shaaban Mpalule, Maandalizi yote kwa ajili ya onyesho hilo yamekamilika “sisi tumeshajipanga kwa ajili ya burudani hiyo, hivyo kazi imebaki kwa wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi ili washuhudie kazi mpya ya bendi yangu ikiwa ni pamoja na kupata radha mpya ya nyimbo mpya”alisema Mpalule Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa bendi ya Mashujaa kutumbuiza katika eneo la ukunda wa Mbezi ambapo wamesema wataonyesha miondoko mbalimbali ikiwemo kuchinja bata, Wamefulia, kwa kiingilio cha shilingi elfu tatu wakubwa na watoto shilingi mia tano.

Wakazi wa Tegeta na maeneo yanayokaribiana mmetakiwa kufika siku hiyo ili kushuhudia burudani hizo, ambapo zawadi mbalimbali zimeandaliwa kwa mashabiki 50 wa kwanza watakaowahi kuingia kukaa katika sehemu zao. Mashujaa Musica kwa sasa imekamilisha kurekodi nyimbo sita ambapo wanatazamia kufanya uzinduzi wa Album yao ya kwanza yenye nyimbo Mwanike, Moshi wa Sigara, Safari ya Vikwazo, Deodata, Mama Mi Nashangaa, sambamba na Intro ambazo zinaendelea kutesa katika sehemu mbalimbali za vyombo vya habari, Radio, Magazeti, na Tv.

Ratiba ya wiki Mashujaa Musica Jumatano –Mashujaa Pub Vingunguti Kiingilio KinywajiIjumaa - woodland kiwalani kwa jimmy kiingilio 3000 Jumamosi –Mashujaa Pub Vingunguti Kiingilio shilingi elfu 2000Jumapili - Nyama Chabez Tegeta Kiingilio Shilingi 3000 wakubwa na watoto 500.

MB DOGG NA ZIARA YAKE UINGEREZA!!


Mb dog amesafiri kwenda katika uk tour.mb Dogg iliyoanza tar. 25/6 asubuhi kuelekea Uingereza kwa ajili ya maonyesho ambayo yatachukua takriban wiki tatu, akiwa huko atafanya maonyesho katika miji tofauti
Ukiwepo milton keynes,bss onx bristol,pia birmingham.pia hakuwaacha bure wabongo amewaachia traki yake ambayo iko katika albam yake ya pili ya akili yangu traki inaitwa "Kilio changu".kwasasa.
Mb. Dogg yuko katika hatua za mwisho kumalizia albam yake ya tatu na si muda mrefu atatambulisha singo yake mpya ambayo amemaliza kurekodi usiku wa kuamkia tar 25.Mb Dogg anaashukuru mashabiki wake wote wanaomsapoti katiki game

Luanda ,Angola mji ghali zaidi duniani


Utafiti wa kimataifa umebaini kuwa LUANDA,mji mkuu wa ANGOLA ndiyo mji wenye gharama ya juu kwa wataalamu wanaotoka nje na kwenda kufanya kazi huko.

Ripoti iliyonadiwa na kampuni ya masuala ya kifedha ya - Mecer imesema gharama za kupanga nyumba mjini Luanda ni mara dufu ikilinganishwa na jiji la London.

Mji wa Luanda umetajwa kuwa ghali zaidi, ukifuatwa na Tokyo, Ndjamena na Moscow. Bara Afrika lina miji mitatu miongoni mwa miji kumi ambayo ni ghali duniani.

Jiji la Libreville, Gabon likishikilia nafasi ya saba. Uchunguzi ulifanyiwa katika miji 214 katika mabaraza yote matano. Mambo yaliyoangaziwa ni pamoja na gharama za maisha ikiwemo usafiri, chakula, mavazi na starehe.

Tiketi moja ya kutazama filamu mjini Luanda inauzwa dola 13. Licha ya raia wengi wa Angola na Gabon kuishi katika lindi la umasikini, hali ni tofauti kwa wageni ambapo gharama za maisha miongoni mwa wafayikazi wa kampuni za mafuta zinaambatana na usalama wao pamoja na ada ya kuagiza bidhaa kutoka nchi zao.

Gharama za juu zimawalazimu wenyeji wengi kuondoka mijini kwani hawawezi kukimu maisha.

MR II A.K.A JOSEPH MBILINYI AACHIWA KWA KUJIDHAMINI MWENYEWE!!



Msanii wa muziki nchini MR 11 ,JOSEPH MBILINYI .

Baada ya msanii MR 2 kukamatwa majira ya asubuhi leo hii katika ofisi za BASATA wakati wa PRESS TALK akiwa anaongelea masuala ya muziki, msanii huyo ameachiwa huru na kituo cha upelelezi cha polisi.
Akizungumza kwa njia ya SIMU 2 amesema alikamatwa na polisi baada ya mmoja wa viongozi wa radio clouds RUGE MUTAHABA kumshitaki mwanamuziki huyo kuwa anamtishia maisha kupia wimbo wake wa AUNT VIRUS.
MR 2 amesema baada ya kukamatwa alipelekwa katika kituo cha polisi cha upelelezi kwa ajili ya mahojiano,lakini baada ya muda MR 2 alitoka kwa kujidhamini mwenye.
Lakini mwamuziki huyo ametakiwa kuripoti tena kesho kutwa katika ofisi hizo kwa mahojiano zaidi. habari kwa hisani ya

REDDS MISS KINONDONI KUBEBA MILIONI 1.5 IJUMAA!!

Mwenyekiti wa kamati ya Redds Miss Kinondoni Bw. Boy George wa pili kutoka kulia akiongea mbele ya waandishi wa habari leo kwenye mgahawa wa Hadees wakati alipotangaza zawadi kwa washindi watakaopatikana katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Boy George amesema mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 1.500.000 zitakazotolea na wadhamini ambao ni Giraffe Ocean View Hotel wakati mshindi wa pili atapata shilingi milioni 1.000.000 zitakazotolewa na Tanga Beach Resort, mshindi wa tatu atapata shilingi laki 800.000 mshindi wa nne na wa tano watapata kiasi cha shilingi laki 300.000 kila mmoja na washiriki wengine kila mmoja atapata kifuta jasho cha shilingi 150.000.
Taji jipya la mrembo mwenye akili, kujiamini na uwezo wa kujieleza yaani Miss Rolls and Skills litatolewa na Jarida la Namba 10 na mshindi atapewa shilingi laki 500.000 na mshindi wa taji la kipaji atajipatia shilingi 200.000 wakati mrembo mwenye nidhamu atapata shilingi elfu 50.000.
Burudani itatolewa na Bendi ya THT na Sebene la nguvu kutoka bendi ya African Stars wana wa kutwanga na kupepeta, huku kiingilio katika shindano hilo kikiwa shilingi elfu 50.000 kwa VIP na shilingi 20.000 kwa viti vya kawaida.
Katika picha kulia ni Selemani Mbuguni mratibu habari wa shindano hilo na Rahma George mkurugenzi wa Miss Kinondoni wa tatu kutoka kulia pamoja na mwalimu wa warembo Lulu Ibrahim ambaye ndiye Miss Kinondoni 2009 pamoja na warembo wanaoshiriki shindano hilo.

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 28, 2010. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Lediana Mng'ong'o kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Al- Qaem ya Mjini Dodoma ambao walitemblea Bunge.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wnafunzi wa kidato cha nne katika shle ya Sekondari ya Al- Qaem ya Mjini Dodoma ambao walitembelea Bunge.

H. BABA AKICHEKELEA DAFU MARA BAADA YA KUNASWA NA WANAFULLSHANGWE!!

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva H. Baba akitaka kuingia mitini wakati aliponaswa na mtambo wetu wa Satelite akijipatika kinywaji cha tunda asili aina ya Dafu huku akiwa ameshikili chupa ya wine, wakati wa tamasha la miaka 10 ya bendi ya muziki wa dansi ya African Stars lililofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam kama unavyomuona mdau wetu.

SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA AFYA!


NA MAGRETH KINABO NA BENJAMIN SAWE – MAELEZO.

SERIKALI imesema kwamba inachukua juhudi za makusudi kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo kwa kuviboresha na kuongeza idadi ya watumishi wa kada mbalimbali. Hayo yalisemwa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Esther Nyawazwa( CCM) lililouliza kuwa hospitali ya Wilaya ya Geita inahudumia kata 33 na ina madaktari bingwa wawili na upanuzi wake unasuasua je ni lini Serikali itarekebisha matatizo hayo.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM) inachukua juhudi za makusudi kuimarisha vituo hivyo katika mwaka wa fedha wa 2010na 2011. hivyo hospitali hiyo inatarajia kupta madakatari wawili na madaktari wasaidizi watatu. Dk. Kigoda aliongeza kwamba ili kuboresha huduma za afya ziendane na ongezeko la idadi ya watu na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya. halmashauri ya wilaya ya Geita imejenga kituo cha faya cha Nyankumbu kilichopo mjini Geita na kimeanza kutoa huduma za afya. Alisema vituo viwili vya Kharumwa na Nzera vinaendelea kufanyiwa ukarabati ili kuvipanua viweze kuhudumia wagonjwa wengi zaidi.

Hata hivyo alisema kuhusu tatizo na utawala mbovu katika hospitali ya Geita Serikali inalifuatiali na kuhahakikisha watumishi wanafanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa. Hospitali hiyo ina watumishi wenye taaluma mbalimbali 218 kati ya watumishi 504 wanaohitajika sawa na asilimia 56.7.

Kazaula akabidhi mashine ya kuchuja maji hospitali ya Kagera!!

Peter Kazaula akikabidhi mashine ya kuchuja maji aliyoitoa kwa hospitali kuu ya mkoa wa Kagera yenye thamani ya zaidi milioni 8 yenye uwezio wa kuchuja lita 6,500 kwa siku ambayo haitumii aina yoyote ya nishati.
Katika piha hiyo kulia kwa Kazaula ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa Dr Amri Byalugaba na kushoto kwake ni mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya mkoa Johansen Rutabingwa.

Burundi kufanya uchaguzi wa urais bila upinzani!!


Raia wa Burundi wanapiga kura katika uchaguzi wa urais ikiwa ni wazi kuhusu anayetazamiwa kutwaa ushindi.

Hii ni baada ya vyama vya upinzani kuwaondoa wagombea wake na kumuacha kiongozi wa sasa Pierre Nkurunziza akiwa mgombea wa pekee.

Uchaguzi huu ndiyo wa kwanza tangu serikali na kundi la mwisho la waasi FNL kuafikiana mkataba wa amani . Kundi hilo liliitikia kushiriki katika mpango wa kisiasa nchini humo.
Hata hivyo wadadisi wameonya kwamba nchi hiyo inakabiliwa na tisho la kurejelea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.Mwezi jana chama tawala kilitwaa ushindi kwenye uchaguzi wa mabaraza uliosifiwa na waangalizi wa kimataifa.

Hata hivyo makundi ya upinzani yalilalamikia udanganyifu hali iliyopelekea muungano wa vyama vya upinzani kutangaza kujiondoa kwenye mchuano wa urais.Mpinzani mkuu wa rais Nkurunziza Agathon Rwasa ametoroka nchini na anadaiwa kukimbilia mafichoni katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika kipindi kizima cha kampeini misururu ya milipuko ya gruneti ndiyo iliyotawala ambapo watu watano walipoteza maisha na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa. Matukio haya yanatilia shaka mstakabali wa mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2006.

Dunga predicts championship match


Brazil coach Dunga is expecting a real "championship match" when his side tussle with Chile in their South American derby at the FIFA World Cup tonight. The Selecao have enjoyed plenty of success against their opponents over the years with their 65 meetings yielding 46 wins for the five-time world champions, while their rivals have come out on top just seven times.

With the latest winning sequence dating back nearly 10 years, Dunga believes there is plenty of motivation for their opponents to try to change the record. "I think that the motivation of any sportsman is to actually try to breach a pattern," he said. "We cannot spend our time comparing ourselves with our opponents. We have to try and improve as much as possible and that is exactly what Chile will do."

The Brazil boss is not expecting any motivation issues for his players. He continued: "My players always know that it's the next game that is the most important one. For now our next game is going to be against Chile, so we will prepare as we do against any other team. In the knockout stages it's all or nothing. Every game can be counted as a championship game.

In the knockout stages it's all or nothing. Every game can be counted as a championship game.
Dunga, Brazil coach

"Chile has been improving a lot with coach (Marcelo) Bielsa. Since he's taken over, it's a competitive team. It's a team that really fights until the very end and is able to get the best out of its players. So they are a difficult opponent and what's happened in the past is finished."

Dunga also felt that five teams from South America in the last 16 showed that football on the continent was in a healthy state. He added: "There are five South American teams playing in the round of 16. Uruguay are already in the quarter-finals which leads us to believe that South American football is extremely competitive and has great players."

Opposite number Bielsa felt there was no point for his side to sit back at Ellis Park, saying they would rather go out attacking against a team they have recently struggled against. "Our match tomorrow is an all or nothing match and we will do our very best to ensure the game is played in a manner that is convenient for us," he said. "We hope we can win. I think the psychological aspect is always very important in a competition. It's more of a factor of motivation for us in my point of view. We have the chance to reverse a historical negative trend for Chile."

Asked whether he was worried about the threat posed by Kaka, he added: "Of course, we have to be extremely careful with him. All the players in Brazil are very good and Kaka is an emblem for them. So no team playing against Brazil can ignore him, but I stress, Kaka has extremely talented team-mates playing with him."

GERALD HANDO APEWA ZAWADI NA MREMBO SALMA ALLY MSHIRIKI MISS KINONDONI!!

Mtangazaji wa kipindi cha powerbreakfast kinachorushwa na radia ya Cluods kila siku asubuhi akionyesha zawadi yake aliyopewa na Mrembo Salma Ally kwenye shindano la kipaji la Redds Miss Kinondoni lililofanyika jana kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi jijini Dar es salaam bango hilo lina ujumbe unaomhamasisha mwanamke kupambana na ugonjwa wa ukimwi na lina alama iliyochorwa kwa viganja vya mrembo huyo, viganja hivyo vinaandika alama "W" ambayo mrembo huyo ameelezea kuwa hiyo ndiyo nembo inayomuwakilisha mwanamke katika mapambano ya ukimwi hivyo katika jamii, hivyo Bw. Gerald Hando nadhani atautumia vyema ujumbe huo na kuueneza sehemu mbalimbali nchini hasa ukizingatia kwamba ni mtangazaji wa kituo cha redio kinachokubalika na rika zote katika jamii yetu hapa nchini.

WASHEREHESHAJI (MCS) WAFANYA MKUTANO NA KUJADILI MATATIZO YAO!!

Washereheshaji wakiwa kwenye pozi wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano huo. Kutoka kulia ni Adella Ngaya (MC), Mwajuma (mpishi wa keki), Angel Rasta Renza (mpambaji) Prisca Charle (mpambaji).CHAMA cha washereheshaji nchini, Sherehe Arts Association (SAA), kinaendelea na mkutano wake mkuu katika Hoteli ya Lion, Sinza, jijini Dar es Salaam. Wadau wa mkutano huo ambao ni ma-MC, ma-DJ, wapambaji, wapishi, wapiga picha pamoja na washereheshaji wengine, wanajadili maendeleo ya chama chao ikiwa ni pamoja na kufungua chama cha kuweka na kukopa (SACCOS). Picha kwa hisani ya
http://www.globalpublishers.com
Wajumbe mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.

HII NDIYO TANO BORA YA SHINDANO LA KIPAJI LA REDDS MISS KINONDONI!!

Hii ndiyo tano bora ya shindano la kipaji la Redds Miss Kinondoni lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyoko Mbezi jijini Dar es salaam warembo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya jaji mkuu Gerald Hando kutangaza matokeo, kutoka kulia ni Irene Hezron, Salma Ally, Alice Lushiku, Caroline Mbembo na Tamara Ally.

Hapa majaji wakiwa makini ili kuhakikisha kazi yao inakwenda vizuri katika shindano hilo.
Huyu yeye alichora bango lenye ujumbe wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi kama bango lake linavysomeka.

Huyu alitangaza lakini anelekea yuko sawasawa na kama kuna redio inahitaji mtangazaji hebu jaribuni kuongea na huyu anaweza kuwafaa.
Huyu akalimwaga sebene la kukata na shoka.
Huyu naye akacheza nyimbo ya Kiarabu.
Shindano la kipaji lilianza kwa mrembo huyu kucheza.
Mh! wadau hawa utamu wa Redds uliwadatisha kidogo hebu wacheki mdau.
Mwanaharakati na Muelimishaji Mama Sadako Kulia akiwa na mwanaye anayempenda Aziza nao walijimwaga ukumbini ili kujua kilichojiri katika shindano hilo.
Wanamuziki wa bendi ya Kalunde kutoka kulia ni waimbaji Mwabi Mwapwani, Sarafin Mshindo, Debora Nyangi pamoja naye mpiga gitaa la sollo mpya wa bendi hiyo Eddo wakipozi kwa picha.
Kutoka kulia ni katibu mkuu kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel na Mwenyekiti wa kamati ya Miss Kinondoni Boy George na Mkurugenzi wa kamati ya Miss Kinondoni Rahma George.
Wadau hawa kutoka kanda ya Pwani na Kitongoji cha Sinza walikuwepo kwenye shindano la kipaji la Redds Miss Kinondoni.