BENDERA - TANZANIA YARUDISHIWA UANACHAMA MCHEZO WA NGUMI


NA MAGRETH KINABO NA BENJAMIN SAWE- MAELEZO, DODOMA

SERIKALI imesema kwamba Shirikisho la Ngumi za RidhaaTanzania (BFT) imerudishiwa uanachama wake katika Chama cha Ngumi Dunaini(IFB),hivyo tayari ina timu ya ngumi na imeaajiri makocha kutoka Cuba kwa ajili ya maandalizi ya Olimpiki yatakayofanyika nchini India. Aidha Serikali imesema kuwa timu hiyo pia itashiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Uingereza.

Hayo yalisemwa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo , Joel Bendera wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge Nantumbo (CCM)Vita Kawawa liliouliza kuwa na nini hatima ya BFT baada ya viongozi wake kukumbwa na kashfa ya dawa za kulevya. Waziri Bendera akijibu swali hilo alisema Serikali baada ya kuona mchezo huo ni muhimu imejitahidi kuomba chama cha IFB kuirudisha uwanachama wake Tanzania ,hivyo sasa hivi timu ya ngumi na chama hicho, kimerudishiwa heshima yake na mchezo huo unaendelea wakati kesi iko mahakamani.

Akijibu swali lingine la nyongeza la Mwanawetu Zarafi , Mbunge wa Viti Maalum (CUF) lililouliza kuwa kuwafundisha watoto mchezo huo ni kiunyume na sheria na ni wa hatari , Waziri Bendera alisema kiutaratibu mchezo huo au wa aina yoyote unafundishwa katika ngazi ya utoto.

Hivyo hata siku moja huwezi ukamfundisha mtu aliyekomaa mchezo kwa sababu ataumia. Aliongeza kwamba kitaalamu unaanza ngazi ya utoto na mashindano hayo yako katika umri mdogo pia. Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maaalum Lucy Owenya alilioliuza kuwa ni taasisi zipi zinazoratibu mchezo wa ndondi alisema zipo taasisi mbili,ambazo ni Chama Cha Ndondi za Ridhaa(BFT) na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa(PST).Mwisho.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment