SERIKALI KUPOKEA MAANDAMANO YA VYAMA VISIVYOGOMA!!


WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya anatarajia kupokea maandamano ya wafanyakazi kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) yatakayofanyika kesho asubuhi katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Maandamano hayo yatawashirikisha wanachama wa vyama vya wafanyakazi ambavyo havishiriki katika mgomo ulioitishwa na Shrikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA).

Akizungumza na Idara ya Habari(MAELEZO) leo jioni, Waziri Kapuya amesema maandamano hayo yataanzia eneo la Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) eneo la Gerezani.
Miongoni mwa washiriki katika maandamano hayo ni pamoja na wafanyakazi wa Benki za NBC na NMB, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE).

Aidha maandamano hayo yatapitia mtaa wa Sokoine, Azikiwe na Bibi Titi Mohamed kuelekea viwanja vya Mnazi mmoja ambapo Waziri Kapuya atayapokea majira ya saa tatu asubuhi.


IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI ( MAELEZO) DAR ES SALAAM.

NGORONGORO HEROERS YAITANDIKA MALAWI 3-1 UHURU!!


Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroers leo imeitandika bila huruma timu ya vijana wa chini ya umri huo kutoka Malawi kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo hii ambapo katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Malawi timu hizo zilitoka sare ya magoli 2 kwa 2.

Vijana wa Ngorongoro Heroers walipigana vikali kuhakikisha wanaondoka na ushindi mnono dhidi ya wamalawi hao waliokuwa wakicheza mpira wa kiwango cha juu japokuwa umaliziaji wao haukuwa mzuri mara kadhaa walipofika langoni mwa Ngorongoro Heroers.
Iliwachukua dakika tatu tu vijana wa Ngorogoro Heroers kupata goli lililofungwa na mshambuliaji machachari wa timu hiyo Omega Seme ambapo timu hiyo iliendelea kuleta madhara katika lango la Malawi na mara nyingine Thomas Ulimwengu aliipatia goli la pili timu ya Ngorongoro kabla ya kwenda mapumziko.

Katika kipindi cha pili kila timu ilijitahidi kupata goli kwa nguvu zake zote hata hivyo walikuwa ni wamalawi waliopata goli la kufutia machozi katika dakika ya tisini kwa njia ya penati iliyopigwa na mchezaji Lastin Simkonda baada ya wachezaji wa Stars kufanya mazambi langoni mwao.

Goli hilo lilipandisha hasira za Ngorongoro Heroers ambapo ilicheza vizuri katika dakika za lala salama, katika dakika ya 91 mchezaji hatari wa timu hiyo Rashid Issa Rashid aliukokota mpira mpaka wingi ya kushoto na kutoa pasi nzuri kwa Thomas Ulimwengu aliyunganisha mpira huo na kuandika goli la tatu kwa timu ya Taifa Stars Ngorongoro Heroers hivyo kufanya matokeo kuwa 3 kwa Taifa Stars na Malawi 1

President Kikwete attends the 3rd EAC Conference on Investment in Kampala, meets Kenyan Prime Minister Raila Odinga!!

From left The Chairman of the East African Community Heads of State Summit President Jakaya Mrisho Kikwete, the host President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and Kenya's Prime Minister Raila Odinga hold an informal discussion shortly before the conclusion of the 3rd East African Conference on Investment held at Munyonyo Speke Resort in Kampala today afternoon.
President Jakaya mrisho Kikwete delivers his speech during the closing session of the 3rd EAC Conference on Investment held in Kamapala(photos by Freddy Maro)

The Secretary General for the East African Community ambassador Juma Mwapachu consults with the Chairman of the EAC Heads of State Summit President Jakaya Mrisho Kikwete during the closing sesssion for the 3rd EAC conference on investment held in Kampala this afternoon.Others from left President Museveni of Uganda,Kenya's Prime minister Raila Odinga and Rwanda's Prime Minister Bernard Makuza.

a cross section some participants to the 3rd EAC Conference on investment held at the Munyonyo Resort in Kampala.

Some East African Heads of State and representatives of Heads of State who participated in the 3rd East African Community Conference on Investment held at Kampala Uganda pose for a group photograph with some members of their delegation.From left Rwanda's Prime Minister Bernard Makuza,Uganda's President Yoweri Kaguta Museveni,President Jakaya Mrisho Kikwete, Burundi's Vice President Dr.Yves Sahinguvu and Kenya's Prime Minister Raila Odinga.

MVUA IMETUHARIBIA PROGRAMU YA MAZOEZI, HATA HIVYO TUKO TAYARI KWA VITA!!

Kocha wa timu ya taifa Taifa stars MARCIO MAXIMO akionyesha karatasi yene majina ya wachezaji wa timu hiyo wakati alipozungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Shirikisho la mpira wa Miguu nchini TFF Karume kuhusu mchezo wa timu hiyo dhidi ya Rwanda vijana wa AMAVUBI .
Amesema kikosi hicho kipo imara kwa ajili ya mchezo huo wa kufuzu kucheza fainali za michuano ya mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN fainali zitakazofanyika nchini Sudan hata hivyo amesema mazoezi hayakuwa mazuri kutokana na mvua kunyesha bila kukatika.

Amesema licha ya mvua kuharibu programu ya mazoezi hayo lakini timu ipo safi kushinda mchezo huo.

Pia amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya mchezo ili kuwahamasisha wachezaji waweze kufanya vizuri katika mchezo huo.

Taifa Stars inacheza mchezo wa pili baada ya mchezo wa awali kushinda kwa kuifunga timu ya SOMALIA magoli sita kwa bila katika mchezo uliofanyika uwanja wa UHURU JIJINI DSM, katika picha kushoto ni Teddy Mapunda Meneja Mwasiliano na Uhusiano Serengeti Breweriers SBL ambao ndiyo wadhamini wakuu wa timu ya Taifa
Picha kwa hisani ya

KAPUYA ATANGAZA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA KWA SEKTA BINAFSI!!

Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya(kulia) akitangaza viwango vipya vya mishahara kwa kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.Viwango hivyo vya kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi vinazigusa sekta za Afya,Huduma za Kilimo, Viwanda na Biashara, Mawasiliano, Sekta ya Madini, Bandari na sekta ya Uvuvi, Wafanyakazi wa majumbani,sekta ya ulinzi Binafsi na Hoteli. (Picha na Aron Msigwa wa Maelezo)
Ufafanuzi wa viwango hivyo.

1. Huduma za Afya - Tshs 80,000/=
2.Sekta ya Kilimo - Tshs 70,000/=
3.Viwanda na Biashara - Tsh. 80,000/=
4. Usafirishaji na Mawasiliano -Huduma za anga 350,000/=
- Clearing and Fowarding 230,000/=
- Mawasiliano ya Simu 300,000/=
- Usafiri wa nchi kavu 150,000/=

5.Madini - Migodini 350,000/=
- Wachimbaji wadogo -150,000/=
- Wauzaji wadigo na watoa leseni 250,000/=
- Brokers Licenses 150,000/=

6. Maji (Bahari na Uvuvi) - Tsh. 165,000/=

7.Majumbani:
- Majumbani (mabalozi na wafanyabiashara wakubwa)- isiwe chini ya Tsh 90,000/=
- Maafisa wenye sitahili ya kulipiwa huduma hii -isiwe chini ya Tsh.80,000/=
- Wengineo - Tshs 65,000/=

Mahotelini:
- Hoteli kubwa za kitalii - 150,000/=
- Hoteli za kati - 100,000/=
- Hoteli ndogondogo,mabaa, nyumba za wageni na migahawa- 80,000/=
8. Ulinzi Binafsi.
-Makampuni makubwa na makampuni ya kigeni - 105,000/=
- Makampuni mengineyo- 80,000/=
9. Sekta nyingine ambazo hazikutajwa - 80,000/=

SIMBA KUWAFUATA WAARABU JUMAPILI ARFAJIRI!!

Timu ya Simba inayoshiriki katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika CAF inatarajiwa kuondoka jumapili alfajiri ikiwa na msafara wa watu 25 ikiwa ni wachezaji 20 na viongozi 5 ambapo itapiga kambi katika jiji la Cairo kwa muda kabla ya kuondoka Alhamis kuelekea Alexandria ambako itacheza mchezo wake kati yake na waarabu wa Haras el-Hodood(Sawahel) kwa jina la utani wakifundiswa na kocha mzawa Tarek El Ashry kati ya ijumaa, jumamosi au jumapili katika uwanja wa El Max Stadium.

Simba ambayo itaongozwa na Kocha wa timu hiyo mzambia Patrick Phiri na mwenye mafanikio makubwa katika timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi inawahi kwenda huko ili kuzoea hali ya hewa na kusoma mazingira ya Misri kabla ya mchezo wao huo ambapo katika mchezo wa awali kwenye uwanja wa Taifa Simba iliwafunga waarabu hao magoli 2 kwa 1 wiki iliyopita.

Ili kuendelea katika michuano hiyo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote au suluhu ili iweze kuwakilisha vyema Tanzania katika mashindano hayo, hata hivyo timu hiyo ina rekodi nzuri dhidi ya timu za misri na imekuwa ikifanya vyema mara kadhaa inapokutana na timu hizo mfano mzuri ni pale ilipoivurumusha katika michuano timu ngumu ya Zamalek ambayo ilikuwa ni bingwa mtetezi wa Klabu bingwa Afrika mwaka 2003.

MANDHARI YA CHUO KIKUU MUHIMBILI SASA YANAVUTIA HATA KUPIGA PICHA!!

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUAASSO) Yusuph Yahya (kulia alievaa kizibao cheusi ) leo jijini Dar es Salaa ameongea na waandishi wa habai kuhusu matatizo mbalimbali yanayokabili chuo chao.(kushoto) Makamu wake Adriano George.(Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO )
Pamoja na matatizo hayo Rais huyo wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi muhimbili MUAASSO amesifia uongozi wa chuo hicho kwa kukarabati miundombinu na kuwa ya kisasa zaidi kwa sasa jambo ambalo lilikuwa linakera na lilikuwa tatizo hapo mwanzo.
Ameongeza kuwa Majengo ya utawala, Mabweni yamejengwa mapya na kukarabati mengine vitanda vipya, meza na viti kwa ajili ya wanafuzi kukalia na kusomea vyote ni vipya "kwa kweli sasa hivi chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kinavutia manake zamani ulikuwa huwezi hata kutamani kupiga picha katika maeneo ya shule lakini sasa hivi kala mahali panapendeza kwa kupiga picha" Amesema Yusuph Yahya Rais wa MUAASSO.

Waasi 100 wauawa nchini Chad!


Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Chad, amesema wanajeshi wa serikali wamewauawa zaidi ya waasi 100 karibu na mpaka wa nchi hiyo na Sudan katika kipindi cha siku tatu zilizopita.
Waziri wa habari nchini humo amesema mwanajeshi mmoja wa serikali aliuawa na wengine 4 walijeruhiwa kwenye makabiliano hayo kati ya jeshi la serikali na waasi wa the Popular Front for the National Rebirth F.P.R.N.

Waziri huyo alifahamisha BBC kuwa waasi hao, ambao aliwataja kama mamluki wa kigeni, wametoroka kufuatia makabiliano hayo.

Lakini msemaji wa kundi hilo la waasi amepinga takwimu hizo zilizotolewa na serikali na kusema jeshi la serikali ndilo lililoshindwa wakati wa makabiliano hayo.

B'Hitz Music Group Tz Mwana FA New Release (April 2010).



Most successful and still active duo in East Africa. They been doing this for almost ten years and still doing it now. Weather it is a single or an album, these guys can still collect more fans than honey collects flies.

Made a LandMark Hit on their "Habari Ndio Hiyo" Album, now they are back with the 1st single "Usije Mjini" from their Upcoming 2nd Album.

The song unfolds the truth about tricks that are run in Urban areas and conveys a warning to all people that are planning to join a city life, to change their minds as it is not all flowers and honey in the city as the rumours purports.

The duo has also been nominated as solo artists in Kilimanjaro Music Awards along with their longtime producer Hermy B responsible for these nominations.
Click the link below and just one vote will make major success to our industry.
http://www.kilitime.co.tz/ or
http://www.kilitime.co.tz/awards/2009/nominees_2007.php

CREDITS:
Song: Usije Mjini
Artist: Ay & MwanaFa
Composed by: Ay & MwanaFa
Written By: Ay & MwanaFa
Produced & Recorded, and Additional instruments By: Pancho Latino At B’Hits Studio 3,Namanga, Dar Es Salaam.

Mixed and Mastered By: Hermy B At B’Hits Studio 1, Mikocheni, Dar Es Salaam.

Ay, MwanaFa, Pancho & Hermy B appears courtesy of B’Hits Music Group Located In Dar es Salaam Tanzania.

Hope Ya’ll going to have fun.
Life’s Too Short…Make The most of it.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI MKOANI SINGIDA!!

WAkazi wa Singida wakiwa wamebeba bango lililochorwa Picha ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ramani ya mkoa wa Singida ikiwa ni zawadi aliyokabidhiwa Mheshimiwa Pinda katika Mkutano wa hadhara aliouhutubia katika kijiji cha Msungua wilayani Singida Aprili 28, 2010, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Shamba la Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia yam atone la Mokiwa wilayani Singida Bw. Ali Mohamed (kushoto) kususu kitalu cha miche ya nyanya wakati alipotembelea shamba hilo akiwa katika ziara ya mkoa wa Singida

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimwagilia mche wa mti wa kivuli alioupanda mbele ya bweni la wasichana katika shule ya sekjondari ya Issuna wialayani Singida ambaloz lilifunguliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika ziara ya mkoa huo,

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (watatu kulia) wakikagua mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa njia yam atone wa Mkiwa wilayni Singida akiwa katika ziara ya mkoa huo, Aprili 28, 2010. Kulis ni Mkuu wa mkoa huo, Vincent Ole Kone.

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza na Sister Maria Tesha wa Kituo cha Masister wa Kanisa Katoliki cha Ursula cha Mkiwa wilayani Singidaambako ameambatana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda anayeendelea na Ziara ya Mkoa huo

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA BARABARA YA SINGIDA MANYONI!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua jengo la ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni akiwa katika ziara ya mkoa wa Singida Aprili 27, 2010. Wapili kulia ni Mkewe Tunu na kulia ni Mbunge wa Manyoni Mashariki na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Capt. Mstaafu John Chiligati. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara ya Singida – Manyoni iliyojengwa kwa kiwango cha lami akiwa katika ziara ya wilaya ya Manyoni, Aprili 27, 2010. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Manyoni Mashariki, Capt. Mstaafu, John Chiligati, Mkuu wa Wilaya ya Bahi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Betty Mkwasa , Mkuu wa Mkoa wa Simgida, Vincent Ole Kone, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombini, Omar Chambo, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kwambwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Mbunge wa Singid a Kusini, Mohamed Missanga na Naibu Waziri wa Miundombinu na Mbunge wa Chilonwa, Hezekia Chibulunje

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua barabara ya Singida – Manyoni iliyojengwa kwa kiwango cha lami akiwa katika ziara ya wilaya ya Manyoni, Aprili 27, 2010. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Manyoni Mashariki, Capt. Mstaafu, John Chiligati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombini, Omar Chambo ,Mkuu wa Mkoa wa Simgida, Vincent Ole Kone, Naibu Waziri wa Miundombinu na Mbunge wa Chilonwa, Hezekia Chibulubje, Waziri wa Miundombinu, Dk . Shukuru Kawambwa, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Mbunge wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa UWT wa Mkoa wa Singida, Dianna Chilolo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Mbunge wa Singida Kusini, Mohamed Missanga.


Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wanne kushoto) akizungumza na wanwake wa kabila la Wataturu ambao walimzawadia vazi lao la asili na kibuyukatika mkutano wa hadhara uliofanyika Itigi wilayani Manyoni Aprili 27, 2010.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na wanawake wa kabila la Wataturu baaada ya kuvalishwa na wazee wa kabila hilo vazi la asili na kupewa mkuki katika mkutano wa hadhara uliofanyiaka Itigi wilayani Manyoni Aprili 27, 2010.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

B'Hits Music Group Tz New Release (April 2010)

Producer Pancho Latino of B-Hitz Music Group Studio (right) and Mabeste (left)


Local, Loco, Loko Call it how u want it but you will dance, with a smiley face guaranteed. Everything these days seems to go way back, and we are always there to ensure the quality sound cause every human being deserves one.

Mchiriku is one of traditional music in Tanzania that has taken a wave of majority listeners. It is composed of funny and simple lyrics that do not need one to crack head to understand. All one needs to do is to listen to the chant full chorus and jump as randomly as your heart can direct you to.

This song is about Kariakoo and its Notorious tricks of theft and pick pocketing, that most of us have come across them if not recently, maybe back then when you did not even know the name of the place but since then, I doubt if you’ll ever forget it.

This was Produced at B’hits Music by Pancho Latino, as a Launch of its small project of this genre of music, that its on huge demand by majority but the supply is yet to suffice that demand. B'HITS MUSIC has taken upon its self to make this music in bulk singlehandedly, and it is the only production house so far that is struggling to revive this coastal flavored music back in charts. B'HITS MUSIC, EXPECT MORE!
CREDITS:
Song: Kariakoo
Artist: Mataluma
Recorded, Engineered and Additional instruments By: Pancho Latino At B’Hits Studio 1, Dar es Salaam.
Mixed and Mastered By: Pancho Latino At B’Hits Studio 1, Dar es Salaam.
Pancho Latino appears courtesy of B’Hits Music Group Located In Dar es Salaam Tanzania.
Hope Ya’ll going to have fun.
Life’s Too Short…Make The most of it.
Hermes B. Joachim Lyimo (Hermy B)
CEO Bhitz Music Group Ltd.
+255 713 513512.

President Kikwete aarives in Kampala for The East Africa Investment Conference!!

Uganda's Vice President Prof.Gilbert Bukenya welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived at Entebbe International airport for The 3rd East Africa Investment conference.
A young ugandan girl Clarissa Kanyenjeka presents a bouquet of flowers to president Jakaya Kikwete shortly after he arrived at Entebbe International Airport for the EAC investment conference to be held ta Munyonyo Speke Resort in Kampala.

Traditional dancers intertain President Jakaya Mrisho Kikwete and his entourage shortly after he arrived at Entebbe airport for the crucial EAC conference on investment.

Uganda's Vice President Prof.Gilbert Bukenya escorts president Jakaya Kikwete through Entebbe airport shortly after he arrived for the 3rd East Africa Investment conference to be held at Munyonyo speke Resort in Kampala(photos by Freddy Maro)

Tanzania yaongeza muda wa kujiandikisha!!


Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania, imetangaza rasmi kuwa itaongeza siku mbili za ziada kwa ajili ya kufanya daftari la kudumu la wapiga kura kuwa bora zaidi.

Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Lewis Makame akizungumza na vyombo vya habari, amesema tarehe zilizopangwa ni 22-23 May, 2010. Siku hizo zitakuwa ni Jumamosi na Jumapili na vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi.

Kwa mujibu wa Jaji Makame, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefikia uamuzi huo, baada ya shughuli hiyo kumalizika mjini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu, lakini kulikuwa na malalamiko kuwa watu wengi hawakujiandikisha.

Awali tume hiyo iliongeza siku moja ya ziada kutokana na wingi wa watu, ingawa watu wengine walilalamikia utaratibu mbovu, uchache wa wafanyakazi na ukosefu wa vifaa.

Jaji Makame anasema lengo la tume ni kuwapatia fursa wananch wote walio na sifa za kupiga kura kujiandikisha au kurekebisha taarifa zao, na amesema ni vyema wakazi wenye sifa kuonesha ushirikiano wa kujiandikisha au kurekebisha taarifa zao.

Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Miss Arusha City Center kulindima Mei 7!

Vimwana wanaoshiriki katika shindano hilo.

Kampuni ya Sophy Entertainment ya mjini Arusha wameandaa shindano la Miss Arusha City Center linalotarajia kufanyika tarehe 7 mwezi wa tano katika ukumbi wa Naura Spring jijini humo.

Akizungumza na Full Shangwe hivi karibuni kwa njia ya simu, muandaaji wa shindano hilo, Bi. Sophia Urio alisema kuwa shindano hilo linatarajia kuwa na msisimko kwa vile linawashiriki kumi (10) wenye mvuto.

Bi. Urio alisema kuwa kwa sasa warembo hao wapo kambini wakijinoa tayari kujiandaa kwa ajili ya mashindano hayo.

Alitaka mataji yanayotarajiwa kushindaniwa na warembo hao kuwa, kutakuwa na mataji manne (4) ambayo ni kipaji, photogenic, balozi na Miss Arusha City Centre.
“Kiukweli najua mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisimko zaidi maana naona walimu wanawanoa warembo kwa kiwango cha juu zaidi,” alisema Bi. Urio.

Kwa upande wake Rachel Michael ambaye ni mwalimu wa Catwalk alisema kuwa anashukuru sana kuona warembo kuwa wana moyo wa kujituma katika mazoezi.
Nae Doreen Mecky ambaye ni mwalimu wa kucheza (dance) alisema kuwa warembo wamejifua vya kutosha na hana shaka katika kinyang’anyiro hicho.


Bi. Urio aliongeza kuwa katika shindano hilo litapambwa na msanii Prezoo kutoka nchini Kenya, Hussein Machozi pamoja na kikundi cha ngoma za asili kutoka jijini humo.

CAG LUDOVICK UTOUH APOINTED THE CHAIRMAN FOR THE AFRICAN ORGANISATION OF SUPREME AUDIT INSTITUTIONS FOR ENGLISH SPEAKING COUNTRIES (AFROSAI-E)


The Governing Board of the African Organization of Supreme Audit Institutions (AFROSAI-E) has elected Mr. Ludovick.S.L. Utouh, The Controller and Auditor General of the United Republic of Tanzania to be the Chairman of the Governing Board of the African Organization of Supreme Audit Institutions for English Speaking countries (AFROSAI-E).

The election was held on 16th April 2010, during the 7th Meeting of the Governing Board of the African Organization of Supreme Audit Institutions which was held in Maseru, Lesotho from 12-16 April, 2010.

Before Mr. Utouh being elected as Chairman of the African Organization of Supreme Audit Institutions, he was a member of the Governing Board of the African Organization of Supreme Audit Institutions (AFROSAI-E).

Mr. Utouh takes over the chairmanship for a period of three years from Mr. John E. Kandjeke Auditor General of Namibia.

AFROSAI-E is an organization of English Speaking Supreme Audit Institutions, with a membership of 24 countries in Africa which was established on 1st January 2005, for the purpose of promoting and developing the exchange of ideas and experience among the Supreme Audit Institution’s of the African states in the field of the Public sector Auditing.
Currently, the Secretariet of AFROSAI is situated in Pretoria, South Africa.
We congratulate Mr. Utouh for the trust and confidence bestowed upon him and wish him success in his new responsibilities.
Sarah Reuben
INFORMATION OFFICER
NATIONAL AUDIT OFFICER.

Inter yaichapa Barcelona, yatinga fainali..!!

Inter Milan's Alberto Milito Diego (right) and Walter Andrian Samuel celebrate after their UEFA Champions League semi-final second leg match vs Barcelona on April 28, at the Camp Nou stadium in Barcelona. Milan reached the final by beating Barcelona 3-2 on aggregate despite losing the second leg 1-0.
Inter Milan chini ya Jose Mourinho, ilicheza mechi ya kujihami kuizuia Barcelona isifunge zaidi ya goli moja na kufuzu kucheza fainali ya kombe la ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya kwenye mechi iliyochezwa Nou Camp, himaya ya Barcelona.

Wakicheza ugenini na faida ya ushindi wa 3-1 walioupata nyumbani, Inter walilazimika kucheza kwa zaidi ya saa moja wakiwa na wachezaji 10 baada ya Thiago Motta kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi Sergio Busquets.

Lakini Barca walishindwa kufungua milango ya Inter mpaka mkwaju wa Gerard Pique ulipohitimisha mpambano huo mkali.

Maafisa wa ngazi ya juu Kenya mahakamani


Maafisa kumi wa zamani wa serikali nchini Kenya wanafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi juu ya ununuzi wa kipande cha ardhi kwa ajili ya kutenga sehemu ya makaburi.
Washitakiwa hao wanatuhumiwa kwa kutumia zaidi ya dola milioni tatu kwa kununua eneo hilo, ambalo thamani yake ilikuwa asilimia 10 tu ya kiasi kulichotajwa, na pia eneo hilo halikuwa na hati.

Watu hao 10, ambao ni pamoja na aliyekuwa karani wa halmashauri ya jiji la Nairobi na afisa mwingine wa ngazi ya juu wa serikali za mitaa walikamatwa siku ya Jumatano.

Wahisani wamelaani vikali serikali ya Kenya kwa kutopambana na ufisadi.
Watu hao walikamatwa na maafisa wa tume ya kupambana na rushwa ya Kenya (Kacc).
Msemaji wa Kacc, Nicholas Simani amesema uchunguzi huo umeonesha "wizi uliopangwa vizuri na maafisa walioidanganya halmashauri ya jiji".

Amesema ardhi hiyo iliyonunuliwa haifai kwa ajili ya kutengwa kwa ajili ya makaburi.
Inadaiwa kuwa kipande cha ardhi hiyo kilichopo katika wilaya ya Machakos, kilinunuliwa kwa shilingi milioni 283, wakati thamani yake ilikuwa shilingi milioni 24.
Watu wengine tisa pia wanachunguzwa kuhusiana na sakata hilo.

Robi Morro and Jamilla Vera Swai launch their Ready to wear collection!!

Inaugural “Origin Africa Designer Showcase” was held last night on 28 April 2010 in Nairobi at the Laico Regency which saw two Tanzanian Swahili Fashion Week designers Robi Morro and Jamilla Vera Swai Launch their new collection.

Tanzania Cotton Board’s (TCB) Textile Sector Development Unit (TSDU) – through the
Organisers’ of the Swahili Fashion Week – had facilitated the participation of Robi Morro and Jamilla Vera Swai.





The work of the Textile Sector Development Unit has been made possible by support from the Gatsby Charitable Foundation and its associated Tanzania Gatsby Trust (TGT). Tanzania Cotton Board wants to ensure that more Tanzanian grown cotton is transformed into higher value added products in Tanzania

Robi Morro of Mapozi Designs collection is named Garden of Style , which is inspired by the woman.” A woman is like a flower, she blossom well if taken good care of” said Robi. “The pieces are very feminine, flirty, sassy colourful and fun aimed at bringing out the woman's beauty with the use of bold colourful floral prints.” added Ms Morro

Jamila’s Collection is named “Say and Color Zero” Inspired by her daughter of two first school homework “Say and Color Zero”. This became her constant routine for every evening. “Her favourite colors being red and black, I decided working with that by layering them by individual colors, with the print zero” said Jamilla.

RICHARD WAMBURA, MWINA KADUGUDA WAMWAGWA NA TFF UCHAGUZI SIMBA!!

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Deogratias Lyato akitangaza majina ya wagombea liyoondolewa kwenye uchaguzi wa klabu ya Simba baada ya kukosa sifa uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mei 9 mwaka huu, kulia ni Chabanga Dyamwale mjumbe kati ya uchaguzi TFF na kushoto ni msemaji wa TFF Frolian Kaijage
Richard Wambura aliyekuwa mgombea wa Uenyekiti wa klabu ya Simba akiongea na waandishi wa habari baada ya kamati ya mashindano ya TFF chini ya mwenyekiti wake Deogratias Lyato kutangaza kumwengua kutokana na rufaa iliyokatwa dhidi yake kwamba hana sifa za kugombea cheo hicho kutokana na kutotimiza matakwa ya ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF kama ilivyoamuliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF napia kamati ya rufaa ya TFF mwaka 2008 alipoomba kugombea nafasi ya makamu wa kwanza wa rais wa TFF rufaa hiyo ilikatwa na Bw. Daniel Kamna.
Kamati hiyo ya mashindano pia imewaondoa Zakaria Haspope aliyekuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiti pia kwa kuwa yeye aliwahi kuhukumiwa kwa kosa la uhaini na kutoka katika kifungo kwa msamaha wa rais.

Aden Rage ambaye pia alikatiwa rufaa yeye kamati hiyo imemuona hana hatia na anafaa kuendelea kugombea kwakuwa ana sifa za kugombea pamoja na kwamba aliwahi kushitakiwa katika mahaka na kutiwa hatiani lakini alikata rufaa mahakama ya rufaa na mahakama hiyo kumsafisha na tuhuma hizo.

Kamati ya uchaguzi pia imemwondoa katika kinyaganYiro hicho Chano Almasi aliyekuwa akigombea ujumbe wa kamati ya utendaji kwa kutotimiza majukumu yake wakati alipokuwa kiongozi katika klabu hiyo lakini pia majina yake yameonekana kuwa na mkanganyiko.

aliyekuwa katibu mkuu Mwina Kaduguda pia ameondolewa kugombea nafasi ya makamu Mwenyekiti kwa kuwa naye alishindwa kutimiza majukumu yake wakati alipokuwa katibu mkuu wa klabu hiyo katika uongozi unaomaliza muda wake.

Hivyo kinyang'anyiro kwa upande wa mwenyekiti kinabaki kwa Hassan Hasanoo,Andrew Tupa na Aden Rage wakati kwa upande wa makamu Mwenyekiti amebaki Godfrey Nyange Kaburu peke yake.

Fredrick na Dorothy Wanameremeta huko A. Town!!

Mr & Mrs Fredrick Mtui wakimeremeta katika Garden ya Kibo Palace Hotel Jijini Arusha Bwana Harusi ni mfanyakazi wa Kampuni ya Tanzania Breweries Limited ya Jijini A Town
Mr & Mrs Fredrick Moses Mtui katika picha ya pamoja na Marafiki zao katika Garden ya Hotel ya Kibo Palace jijini Arusha.

Kutoka kushoto ni Bestman Bw.Joseph Kisamo na Bi.Eva wakiwa na Mr & Mrs Fredrick Moses Mtui baada ya kufungu ndoa hivi karibuni jijini Arusha.

CHAMA CHA MADALALI WAMUUNGA MKONO JAKAYA KUHUSU SHERIA YA MAKAMPUNI YA SIMU!!

Mwenyekiti wa Chama Cha Madalali wa Soko la Hisa , Tanzania (TSEBA - Tanzania Stock Exchange Brokers Association) Leandri Tairo -Urasa (kulia) akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu chama chake cha Madalali wa soko la Hisa la Dar es Salaam kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kuweka mbele maslahi ya taifa na kusaini Sheria ya Makampuni ya simu ya mwaka 2010. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
Baadhi ya viongozi wa Makampuni yenye Hisa waloihudhuria na kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu nia yao ya kumuunga mkono na kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kuidhinisha sheria ya Makampuni ya Simu 2010. (Kutoka kulia) ni Mkurugenzi Mkuu (CEO) wa kampuni ya Solomon Securities Ltd Kisali Solomon, (CEO - Care Securities Ltd) George Fumbuka, (Mwenyekiti wa TSEBA pia ni CEO wa Tanzania Securities Ltd Bw, Leandri Tairo -Urasa, (General Manager wa Rasilimali Ltd Bw. Arphaxad Masambu na (CEO wa Orbit Security Ltd ) Laurean Malauri. (kushoto Picha zote na mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

Wete watwaa Kombe la Muungano!!

Naibu Waziri Kiongozi na ambaye pia Waziri wa Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamhuna, akimkabidhi Kombe Nahodha wa Timu ya Wete, Ali Badru, baada ya fainali ya Kombe la Muungano linalodhaminiwa na Vodacom Tanzania, katika mchezo huo, Wete ilishinda 3-0 na kutwaa kombe hilo.
Mkurugenzi wa Masoko wa VodacomTanzania, Ephraim Mafuru akimvisha medali ya Shaba mmoja wa wachezaji wa Timu ya MUCOBA ya Mufindi baada mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano linalodhaminiwa na Vodacom Tanzania kati ya timu hiyo na Wete ya Pemba katika mchezo huo, wete ilishinda 3-0.

Wachezaji wa Wete wakishangilia ushindi wa baada kutwaa Kombe la Muungano baada ya kuikandamiza bila huruma timu MUCOBA ya Mufindi.

Kazi ni kazi tu muhimu ni kuichangamkia!!

Huyu anayekimbia si mwizi bali ni Muuzaji wa kuku katika kijiji cha Bande mkoani Dodoma akikimbilia wateja walio safarini kutoka mkoani humo kuelekea jijini Dar es salaam walopo kwenye basi halipo pichani hivi karibuni Picha na mdau Mwanakombop Jumaa wa Idara ya Habari Maelezo.
ukihangaika hutolala na njaa na Mungu atakusaidai. Vijana wa Gairo Dodoma wakisaka riziki kwa kuuza vitu mbalimbali kwa wasafiri wanaotoka mkoani humo na kuelekea maeneo mbalimbali ya nchi vijana hawa walinaswa hivi karibuni na Kamera ya Mwanakombo Jumaa wa Idara ya Habari Maelezo


TAMKO LA CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI KUHUSU MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI DAR ES SALAAM!!

Mwenyekiti wa chama chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho Ilala leo katikati ni katibu mkuu wa chama hicho Samuel Ruhuza na mwisho ni Mwenyekiti wa idara ya wanawake NCCR Mageuzi Amina Suleiman.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia akizungumza na mwanablogu John Bukuku nje ya ofisi hiyo mara baada ya kumalizika mkutano, kulia na Mwandishi kutoka gazeti la Changamoto Suleiman Msuya.

Leo Chama cha NCCR-MAGEUZI tumewaomba tukutane , ili tuweze kujadiliana kwa pamoja tatizo la msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Wengi tumekuwa tukizungumzia hali hii ya msongamano wa magari katika ngazi ya kero. Mvua ya masika inayonyesha sasa inatuonesha kwa vitendo, kwamba hali hii tuliyojitengenezea siyo kero tena bali ni tatizo linanohitaji utatuzi wa haraka katika muda mfupi na utatuzi wa muda mrefu.
Kwa kushirikiana na wanataaluma na wanaharakati wa mambo ya Mipango Miji, Afya ya Binadamu, Haki za Binadamu na Tabia nchi tumebaini kwamba hili ni tatizo la kitaifa. Hoja hii inajidhihirisha pia katika katika majiji mengine nchini. Kwa mfano jiji la Arusha na jiji la Mwanza nayo yameshaanza kukerwa na hali hii ya msongomano wa magari barabarani.

NCCR-Mageuzi tumetafakari na kuona kwamba tunahitaji kuweka nguvu zetu zaidi katika kupata utatuzi, kuliko kutumia muda katika kulalamika au kutafuta chanzo cha tatizo kwani inafahamika haya ni matokeo ya mifumo ya isiyojali utu, inayodumaza ustawi wan chi zinazojulikana kama nchi zinazoendelea.

Tunafahamu kwamba historia ya ujenzi wa majiji katika ukanda wa bahari katika nchi ambazo zinaendelea haitofautiani sana. Mfano ni majiji kama Lagos nchini Nigeria na Cape Town nchini Afrika Kusini, yalikumbwa au yanakumbwa na tatizo hili na wameweza au wanatafuta utatuzi wake.

Utatuzi endelevu kwa tatizo hili la jiji la Dar es Salaam itatokana na dhamira yetu ya pamoja kama taifa, inayojali masilahi ya wote bila ya kumsahau mama yetu dunia.

Masilahi ya wote ni muhimu. Kwani kwa kukokotoa takwimu endelevu tumeweza kubaini kwamba, kwa wastani kero hii ya msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam inaligharimu taifa letu zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni 4 kila siku. Kiasi hiki cha thamani kinatokana na:

· Asilimia 30 ya muda wa Wanajiji la Dar es Salaam unatumika katika kusafiri kutoka na kurudi kwenye makazi yao kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli binafsi au kazini;
· Nguvu ya ziada ya nishati inayotumika; na
· Hewa mkaa (carbon dioxide) ya ziada itokayo kwenye magari.

Gharama hii ya shilingi za Kitanzania bilioni 4 haijumuishi gharama ya msongo (stress) inayowakumba Wanajiji la Dar es Salaam, itokanayo na tatizo hili.

Mfano: Tukitumia ulinganisho, tunaona kwamba shilingi za Kitanzania bilioni 4 kwa siku, zinaweza kutumika kununua madawati 80,000 kwa bei ya shilingi 50,000 kwa dawati kwa matumizi ya watoto wetu. Au gharama ya kujenga Kituo kimoja cha Afya cha kisasa ni shilingi za Kitanzania bilioni 2. Hivyo kwa kutumia ulingano, kila siku tatizo hili la msongamano wa magari hapa jijini Dar es Salaam linatugharimu ujenzi wa vituo vya afya viwili vya kisasa. Ambapo huu ni ustawi hasi kwa taifa letu.

Takwimu hizi zinatuumbua tunapolalamika kila siku, kwamba sisi ni maskini. Takwimu hizi zinatupa nafasi ya kushirikiana katika kutafuta utatuzi wa tatizo hili. Tunaomba tuweke mbele masilahi ya pamoja kama tiafa katika kupata haraka utatuzi wa tatizo hili.

Leo NCCR-Mageuzi tunatoa mchango wetu kwa kutoa mapendekezo yafuatayo:-

1. Kusimamisha au kutoendelea kutoa vibali vya kujenga ofisi, maduka makubwa na madogo katikati ya jiji;

2. Wataalamu wetu wakutane mara moja ili kuboresha utaratibu uliopo wa usafiri jijini na wapewe nyezo za kukarabati miundo mbinu ya barabara zilizopo sasa;

3. Uwezekano upo wa kutumia treni kutoka Pugu – Gongolamboto – Vingunguti – Buguruni mpaka Kituo Kikuu cha Kati. Pia kutoka Ubungo mpaka Kituo Kikuu cha Kati;

1. Uwezekano upo wa kutumia njia ya Boti kutoka Bagamoyo – Mbweni – Tegeta – Mbezi – Msasani mpaka Bandarini;

2. Serikali igharamie mradi usio wa kibiashara wa mabasi ya kisasa kwa jiji la Dar es Salaam;

3. Ghala la kuhifadhi mizigo kutoka bandarini lijengwe nje ya jiji, kwa mfano Chalinze;

4. Soko Kuu la chakula lijengwe nje ya jiji, kwa mfano Kibaha;

5. Tunapendekeza ofisi zifuatazo zihamishiwe nje ya jiji au hata nje ya mkoa. Mfano Wizara ya Ardhi, Wizara ya Elimu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Utalii, Mahakama Kuu ya Tanzania, Magereza, na Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na uwanja wa ndege;

6. Kujenga eneo la kuengesha magari la kisasa lenye uwezo wa kuegesha zaidi ya magari 10,000; kwa mfano eneo la Jangwani; na

7. Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifanyiwe kazi ili mfumo wetu wa sheria uweze kufanya kazi ipasavyo;

Ufafanuzi wa kina wa utekelezaji wa mapendekezo yetu upo, na tupo tayari kushirikiana na idara zinazohusika kwa utekelezaji. Kukata tamaa ni dhambi. Tunaomba tujitambue, kwamba Haki hupiganiwa. Uwezo wa kupata haki zetu tunao.
Aksanteni sana kwa kunisikiliza.
Mungu Ibariki Afrika !
Mungi Ibariki Tanzania !
Ndimi Mtumishi Mtiifu,

James Francis Mbatia
MWENYEKITI TAIFA