Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania, imetangaza rasmi kuwa itaongeza siku mbili za ziada kwa ajili ya kufanya daftari la kudumu la wapiga kura kuwa bora zaidi.
Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Lewis Makame akizungumza na vyombo vya habari, amesema tarehe zilizopangwa ni 22-23 May, 2010. Siku hizo zitakuwa ni Jumamosi na Jumapili na vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi.
Kwa mujibu wa Jaji Makame, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefikia uamuzi huo, baada ya shughuli hiyo kumalizika mjini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu, lakini kulikuwa na malalamiko kuwa watu wengi hawakujiandikisha.
Awali tume hiyo iliongeza siku moja ya ziada kutokana na wingi wa watu, ingawa watu wengine walilalamikia utaratibu mbovu, uchache wa wafanyakazi na ukosefu wa vifaa.
Jaji Makame anasema lengo la tume ni kuwapatia fursa wananch wote walio na sifa za kupiga kura kujiandikisha au kurekebisha taarifa zao, na amesema ni vyema wakazi wenye sifa kuonesha ushirikiano wa kujiandikisha au kurekebisha taarifa zao.
Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment