OFA YA KUTEMBELEA MBUGA ZA WANYAMA!!

TTB yatoa ofa za Pasaka kwa wale wanaopenda kwenda kutembelea mbuga za wanyama Mikumi Ruaha, Bagamoyo kwa maelezo zaidi tembelea mtandao wao kwa kubofya hapa

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 122 wa IPU wampongeza Balozi Sisco kwa mapokezi mazuri Thailand!!

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta na Balozi Sisco Mtiro wakibadilishana vitabu vilivyo tiwa sahihi za wajumbe waliohudhuria Mkutano wa 122 wa IPU toka Tanzania na wageni waalikwa kama ishara ya kumbukumbu ya mkutano huo.
(Picha na Afisa Habari wa Bunge Owen Mwandumbya)

Mhe. Dr. Christene Ishengoma naye akitoa Salam za Pongezi kwa mapokezi mazuri kwa balozi Cisco (mwisho kulia) kwa kipindi chote ambacho wamekua nae hapa Bangkok thailand kuhudhuria mkutano wa 122 wa IPU. Katikati ni Mhe. Prof. Idris Mtulia (Mb)

Spika wa Bunge. Mhe. Samuel sitta akitoa shukrani zake kwa Balozi Cisco Mtiro kwa mapokezi mazuri (kulia) kwa niaba ya ujumbe wa Tanzania unaohudhuria mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)
wakati wa chakula cha usiku jana, katika Hotel ya Conrad mjini Bangkok. Balozi Cisco licha ya kuwa Ubalozi wake upo Kuala Lumpar Malaysia, pia anashughulikia nchi ya Thailand ambapo kwa kipindi hiki cha mkutano wa 122 wa IPU naye yupo Bangkok kuratibu ugeni wa Tanzania katika nchi hii.

Mhe. Balozi Sisco Mtiro akitoka nje ya Hotel ya Conrad, Mjini Bangkok Thailand, mara baada ya chakula cha usiku na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki
mkutano wa 122 wa IPU katika hotel ya Conrad, kulia kwake ni Afisa Habari wa Bunge Owen Mwandumba akimsindikiza.

Spika wa Bunge akifurahia zawadi ya Track suite zenye nembo na rangi ya CCM ambazo zimetengenezwa na Mtanzania anayefanya shughuli zake hapa Bangkok Thailand, Bwana Nicholaus Kipalanga (kulia) alipomtembelea jana katika Hotel ya Conrad jana Usiku. Bwana kapalanga anakampuni yake inayojishughilisha na uuzaji madini iitwayo Asili Germs International Co. Ltd ambapo pamoja na madini anafanya biashara za kutengeneza nguo za sare kwa order Maalumu kama vile sare za makampuni, Tshirt na truck suite kwa ajili vyama na kampeni mbalimbali.





ANC wakasirishwa na uamuzi wa mahakama!!

Chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress,ANC kimekasirishwa na uamuzi wa mahakama kupiga marufuku kuimba wimbo wenye maneno "Shoot the Boer" yaani "Kaburu auawe".
ANC imesema kampeni inayofanywa na wanaharakati wa kizungu kuzuia wimbo huo kutumika ni jaribio la kuwapandisha hadhi mawakala wa ubaguzi wa rangi kama wao ndio wanaodhulumiwa.
Kiongozi wa vijana wa ANC Julius Malema aliimba wimbo huo hivi karibuni, iliyosababisha kuwepo na madai ya kuchochea ghasia.
Bw Malema aliimba wimbo huo mjini Johannesburg, na kusababisha mabishano katika nchi ambapo ubaguzi wa rangi bado ni changamoto.
Katibu mkuu wa ANC Gwede Mantashe amesema chama chake kitafikisha suala hilo katika mahakama inayoshughulika na masuala ya katiba.

Waziri wa Fedha apokea msaada wa waathirika wa Kilosa Ikulu jioni hii!!

Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo akipokea shehena ya marobota ya viatu alivyokabidhiwa leo jioni Ikulu kwa ajili waathirika wa mafuriko ya Kilosa. Msaada huo umetolewa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kupokea kutoka Serikali ya China hivi karibuni. Msaada huo ulikabidhiwa na Naibu Katibu wa Rais Ndugu Shabani Gurumo kwa niaba ya Rais.

Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo akiendesha moja ya baiskeli za misaada kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Kilosa baada ya kukabidhiwa na Rais kikwete leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo akionyesha mmoja ya pikipiki alizokabidhiwa leo Ikulu na Rais Kikwete kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko ya Kilosa.

Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo akitoa maelezo leo Ikulu jijini Dar es salaam kwa Naibu Katibu wa Rais Ndugu Shabani Gurumo(kushoto) na Msemaji wa Wizara ya Fedha na Uchumi Bi. Ingiahedi Mduma(katikati) ,jinsi atakavyoigawa misaada ya wathirika wa mafuriko ya Kilosa aliyopatiwa leo Ikulu na Rais Kikwete




RAIS JAKAYA KIKWETE AWAPANDISHA VYEO MAKAMANDA WA POLISI NCHINI

Na Mohammed Mhina na Athumani Mtasha wa Jeshi la Polisi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 42 wa Jeshi la Polisi kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, imesema kuwa waliopandishwa vyeo kuanzia Machi 16, mwaka huu ni pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa tisa, Makamanda watano wa vikosi na Wakuu wa Vitengo mbalimbali vya Jeshi hilo waliopo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam na Zanzibar.
Kamanda Mssika amesema kati ya hao wapo Maafisa wanne wakuu ambao wamepandishwa vyeo kutoka vyeo vyao vya zamani vya Makamishna Wsaidizi Wandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Manaibu Makamishna wa Polisi (DCP).
Walipandishwa kuwa Manaibu Kakamishna wa Polisi (DCP’s) ni Mkuu wa Huduma za Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi SACP Isaya Mngulu, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Afya nchini SACP Neven Mashayo, SACP Rashid Omari Ali, wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACPO Suluiman Kova.
Kamanda Mssika amewataja Makamanda 38 wakiwemo Makamanda wa Polisi wa Mikoa tisa ya Tanzania Bara na Visiwani kutoka Vyeo vya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP ambao sasa kila mmoja anakuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) ambao ni Makamanda Thobias Andengenye wa Morogoro, Henry Salewi wa Kagera, Bi Celina Kaluba wa Singida na Kamanda Lucas Ng’hoboko wa Kilimanjaro.
Wengine ni Kamanda Absalom Mwanyoma wa Pwani, Simon Sirro wa Mwanza, Isuto Mantage wa Rukwa, Michael Kamhanda wa Ruvuma na Yahaya Rashidi wa mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kamanda Mssika amewataja Makamanda wa Vikosi waliopandishwa vyeo kuwa ni Mohammed Mpinga, wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Tresphory Anaclet wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini (FFU), Sospeter Kondela, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Ujenzi, Geofrey Nzoa Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na kupambana na Madawa ya Kulevya na Mkuu wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam Bi. Alice Mapunda.
Wengine ni Mkuu wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini Kamanda Hussein Nassoro Laizer, Mkuu wa Bohari Kuu la Polisi nchini Kamanda Adriano Magayane, Mkuu wa Kikosi cha Usafirishaji cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Kamanda Ali Mlege na Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Jonas Mgendi.
Wengine ni Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania kwenye Ofisi za Interpol Kanda ya nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika Kamanda Goodluck Mongi, Mkuu wa Kitengo cha Picha na Maabala ya Uchunguzi wa Vielelezo vya Makosa ya Jinai nchini (FB) Kamanda Hezron Gyimbi.
Wengine ni Kamanda Jamal Rwambow, Kamanda Lucas Haule na Kamanda Donald Ludamila wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Makao Makuu, Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Lucas Kusima, Kamanda Saidi Juma Hamis kutoka Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu.
Kamanda Mssika amesema kuwa wengine walipandishwa ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mifumo ya Mitangao ya Kompyuta ya Jeshi la Polisi nchini kamanda Anyisile Kyoso, Kamanda Renatus Chalamila, Mwanasheria wa Jeshi la Polisi nchini Kamanda Donald Kaswende na Kamanda mwanamke Adolfina Chialo.
Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Abdulrahman Kaniki, Msaidizi wa Mkuu wa Operesheni Maalum nchini Kamanda Hezron Kigondo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zananzibar Kamanda Mussa Alli Mussa na Kamanda Hamdani Makame wa Ofisi ya Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Mkuu wa Mipango Kamanda Ernest Mangu, , Kamanda Makame Ali Makame, Kamanda Mwalim Ame na Kamanda Mpinga Gyumi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Rais Kikwete na Balozi wa China waweka jiwe la msingi ujenzi wa Taasisi ya Moyo Muhimbili!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(wanne kushoto) na Balozi wa China nchini Bwana Liu Xinsheng(watatu kushoto) wakiweka udongo katika jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa Taasisi ya tiba ya moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MNH leo asubuhi.Wengine katika picha ni Waziri wa Afya Profesa David Mwakyusa(watano kushoto) na kuli ni Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bwana Adolar Mapunda, wapili kushoto ni kiongozi wa ujumbe wa Jamhuri ya watu wa China Bwana Sun Liang (picha na Freddy Maro)

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali akabidhi Ripoti za ukaguzi wa Matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake Kwa Rais Kikwete Ikulu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Ludovick Utouh akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ripoti za ukaguzi wa matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Kushoto ni Msaidizi wa mkaguzi mkuu Bwana Atanas Tarimo(Picha na Freddy Maro)



HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA DIAMOND APRILI 9-10!!

Mratibu wa Mradi wa Harusi Trade Fair Sati Gadhvi akizungumza leo jijini Dar es salaam kuelezea maonyesho ya bidhaa za Harusi yanayotarajiwa kufanyika Aprili 9-10/ 2010 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo washiriki zaidi ya 40 wanaojishughulisha na mambo ya kuandaa harusi wanatarajiwa kushiriki, amesema kiingilio katika maonyesho hayo kitakuwa shilingi 2000 kwa mtu mmoja aliyeko kulia katika picha ni meneja masoko na Mauzo wa Harusi Trade Fair Khamis Omar.

TATIANA DURAO BALOZI WA MATENDE AFRIKA MASHARIKI NA KATI!!

Balozi wa ugojwa wa Matende (ELEPHANTIASIS DISEASE) kwa nchi za Mashariki na Afirica ya kati (Ambassador for Elephantiasis disease in East and Central Africa) ambaye pia ni Mshindi wa pili wa BBA2 Tatiana Durao kutoka Angola , leo jijini Dar es Salaam amezungumza na wandishi wa habari kuhusu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Machi 31, 2010 pamoja na hilo atafanya ziara fupi katika kisiwa cha Unguja pamoja na kuwasaidia watoto wa KIWOHEDE wa jijini Dar es Salaam.
Tatiana Durao z ameongeza kuwa sasa amechaguliwa kuwa balozi wa Matende Afrika ya mashariki na kati na pia ni mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Kiwohede kilichopo jijini Dar es salaam.
Mbali ya kazi zake hizo Tatiana Durao amesema kazi atakayofanya akiwa nchini ni kurekodi kipindi chake kinachoitwa "Oh Tatiana" TV Series kitakachorushwa katika televisheni mbalimbali barani Afrika, amesema katika shughuli zake hizo atasherehekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima wa Kituo cha Kiwohede na kuenda Zanzibar ambako pia anatarajia kurekodi kipindi chake hicho.

Tatiana Durao akiwa katikati akiwa pamoja na meneja wake Alice Mutumba wa kampuni ya True Media ya Uingereza na msaidizi wa Tatiana Ebmenalda Antonio.

Kwikwi globalpublishers


Kuna tatizo la kiufundi ambalo limetokea kwenye mtandao wa www.globalpublisherstz.com na kusababisha mtandao huo kutofunguka kwa sasa.
Tatizo hilo limetokea kwenye server inayo host mtandao huo na hivi sasa wataalamu wetu wako kazini wakilishughulikia tatizo.
Ni matarajio yetu kuwa baada ya saa chache zijazo, utakuwa hewani na habari zake za leo kama kawaida. Tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Asante
Web Master
GPL
"Great achievement, involves great risks"Abdallah Mrisho
www.abdallahmrisho.blogspot.com

NDESAMBURO AVAMIWA NA WANACCM WAWILI KWA MPIGO MOSHI MJINI!!

Bwana Batista Mwendivita ambaye ni Mjumbe wa halmashari kuu ya Wilaya ya Moshi Mjini CCM na Mwenyekiti wa chama cha wenye ulemavu mkoani Kilimanjaro kushoto na MwanaCCM mwingine Gibson Nderangusho wakitangaza mbele ya wanahabari kwa pamoja nia yao ya kugombea ubunge katika jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM, wote kwa pamoja wamesema wana nia hiyo na katiba zote mbili ya Chama Cha Mapinduzi na ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania zinawaruhusu kufanya hivyo na ni haki yao ya kimsingi , marafiki hao wawili walitangaza nia yao leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.

MKURUGENZI MTENDAJI WA ICF AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI JANA!!

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ICF barani Afrika Bw. Omary Issa akizungumza na waandishi wa habari wa vyomba mbalimbali kuelezea mambo mbalimbali yanayofanywa na shirika hilo katika nchi za Afrika katika kushirikiana na nchi hizo kurekebisha changamoto mabalimbali zinazokabili Tasisi za Ushuru na Forodha, akitolea mfano wa nchi ya Senegal ambayo amesema kazi ya kushughulikia malipo ya kodi na ushuru wa mizigo mbalimbali inayotoka nje ya nchi hiyo na kuingia inachukua siku moja tu, lakini akasema kwa Tanzania kwa mfano unapozungumzia utoaji wa mizigo Bandarini unahusisha idara zipatazo saba hivyo idara zote hizo zinatakiwa kwenda kwa kasi moja katika utendaji wa kazi zao ili kuweza kuondoa changamoto hizo, lakini pia amezungumzia mkutano wa mkubwa wa wawekezaji utakaojulikana kama ICF Investiment Climate Summit utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Mei 3-4 2010 na kukutanisha wadau mbalimbali, mkutano huo ulifanyika jana kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.
Waandishi wahabari mbalimbali wakisikiliza mambo mablimbali yalioyoongelewa katika mkutano huo jana

MASHUJAA MUSIC BAND KULA PASAKA UKONGA MAGEREZA!!


Bendi mpya ya muziki wa dansi nchini MASHUJAA BAND, imewaandalia Burudani ya aina yake siku ya Sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa Bwalo la Magereza ambapo pia kutakuwa na Bonanza la aina yake litakaloshirikisha timu mbalimbali za maveterani kutoka mikoani.
Kwa mujibu wa Shaaban Mpalule msemaji wa bendi hiyo burudani itaanza saa tisa mchana ambapo nyimbo mbalimbali zitatumbuizwa ikiwa ni pamoja na kutambuylishwa nyimbo mpya inayotazamiwa kurekodiwa mara tu baada ya Sikukuu ya Pasaka ya Safari yenye Vikwazo mtunzi Jadol Fidifosi (FFU).
Aidha bendi hiyo siku ya leo ipo Woodland kwa jimmy Yombo, kesho itakuwa katika ukumbi wake wa nyumbani wa Mashujaa Pub, ijumaa itatelemka katika ukumbin wa Equatol Grill Temeke Mtoni, jumamosi itafanya onyesho tena katika ukumbi wa Woodland, jumapili itashuka kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Magereza Ukonga..
Katika Maonyesho hayo wanamuziki na Wacheza shoo wote nyota wa kundi hilo watakuwapo, ikiwa ni pamoja na Kiongozi wa bendi Aliston Angai, Despino Malaika, Geran Kissa, Masooud USB, Ngosha Mwanamasanja, Jado Fidifosi, Pasia Budansi, Raja Rado, na wengine wengi.
Kwa upande wa Burudani ya Shoo bendi hiyo imezidi kung’ara zaidi kutokana na juhudi za Sharony Mapozi, Frida Mwanasuka, Sarafina Shotii,Pendo Bonzo, Merisa Maga, pamoja na Etoo Tisa
Wengine ni mpiga gitaa, Amosi Ras, Baba , Flora Bambucha, Sarafina Shotii, Sharoni Mapozi, Neema Mkama, Pendo Boza, Frida Etoo Tisa, huku waimbaji wakiwemo Ibrahimu Milinda Nyeusi, Pasia Budansi Bakiza Mambo(Raja), Desipino Malaika, Masoud USB, Edward Anthony MaliKidogo(jadol Feed Force FFU) na Mwanamuziki na rapper wa bendi SIMONG NGOSHA(ngosha masanja)
Nyimbo zinazovuma kwa sasa ni ule wa Mwanike ulioimbwa kwa mchanganyiko wa makabila ya Kisukuma na Kihaya, ukiwa umetungwa na Ngosha Mwanamasanja na Moshi wa Sigara uliotungwa na mwanamuziki Pasia Budansi.
Viingilio katika maonyesho yote ni vya kuridhisha ili kuwapa mwanya wote kwenda kushuhudia bendi hiyo mpya ya nyumbani inavyokuja kwa kasi katika medani ya muziki wa dansi.

TANZANIA KUPATA BILIONI 322 KUTOKA BANKI YA AFRIKA (ADB)

Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana mjini Dares salaam wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt Sipho Moyo.

Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akibadilishana hati jana jijini Dar es salaam ya makubaliano ya msaada wa kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt Sipho Moyo.

Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) imetiliana saini makubaliano ya msaada wa kifedha na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha sekta ya barabara na reli nchini.
Makubaliano hayo yataiwezesha Tanzania kupata jumla ya bilioni 322.5665 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani 235.49.
Makubaliano hayo yatiwa saini jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi Ramadhan Khijjah kwa niaba ya Tanzania na Mwakilishi Mkazi kutoka ADB Dkt . Sipho Moyo katika Ofisi za Hazina.
Katibu Mkuu huyo alisema kati ya fedha hizo kiasi cha bilioni 319 zitasaidia kuimarisha miradi ya barabara kwa ajili ya kuboresha huduma kwa ajili kuharakisha maendeleo nchini.
Khijja alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha huduma za usafiri wa barabara kati ya Iringa na Dodoma yenye kilimeta 260 na kati ya Tunduma na Namtumbo yenye kilometa 193.
Aliongeza kuwa fedha hizo pia zitasaidia kuboresha usafiri Zanzibar na kuboresha Bandari ya Mtwara ili kuboresha huduma za bandari nchini.
Khijjah alisema kuwa sehemu ya fedha hizo pia itasaidia hatua ya pili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kutoka Isaka kwenda Kigali na Keza -Musonati.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo utasaidia kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji wa mizigo ndani ya nje ya Tanzania.
Kwa upande wa Mwakilishi Mkazi kutoka ADB hapa nchini Dkt.Moyo alitoa wito kwa Serikali ya Tanzania kuharakisha utekelezaji wa masharti kwa ajili ya kukamilisha taratibu za makubaliano ya kupata mkopo huo.
Alisema kuwa kukamilika kwa hatua hizo zitasaidia Tanzania kunifaika na mkopo ambao hatimaye utasaidia kupunguza umaskini sio tu kwa Watanzania bali kuunganisha Tanzania na jirani zake.

MASOFISA SHERIA WAPATA MAFUNZO YA UANDISHI WA SHERIA!!

Katibu Mtendaji wa Tume Japhet Sagasii akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku vyeti Maofisa Sheria wa Tume mara baada ya kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja huko Morogoro
Mhadhiri wa Mzumbe Modesta Opiyo katikati akimtunuku cheti Ofisa Sheria wa Tume Andisya Nalingigwa

Maofisa Sheria, Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) Japhet Sagasii wakigongeshana glasi wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika mkoani Morogoro
Picha zote na Munir Shemweta, Ofisa Habari wa Tume (LRCT)



Bi Shekha Said achomoka na vyombo vya Zantel!

Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini Dr. msengi (kulia) akimkabidhi mshindi wa kwanza wa promosheni ya Zantel chomoka na vyombo Bi. Shekha Said( katikati) zawadi ya jokofu na tv,kulia ni meneja mauzo wa zantel mkoa wa Tanga ndugu nassoro mbilikira.

Gavana wa China kujenga kituo Muhimbili!!

Gavana wa Jimbo la Zhangdong wa nchini China bw.Sun Liang akizungumza na waziri wa afya na ustawi wa jamii Profesa Davi Mwakyusa hayupo pichani kwenye ukumbi wa wizara mara baada ya kuwasili Tanzania.Ugeni huo upo nchini ambapo wanajitolea kujenga kituo cha kutibu magonjwa ya moyo na upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili..
(Picha na Catherine Sungura-MOHSW)

Mafunzo ya wanamitindo ufukwe wa Mbalamwezi!!

Wanamitindo waliopatikana kupitia Kampuni ya Black Fox ya jijini Dar es Salaam wakionesha mavazi yao ikiwa ni mara ya kwanza kuonesha mavazi tangia waanze kushiriki mafunzo hayo ya uanamitindo yanayoendeshwa na Kampuni hiyo, tukio hilo lilifanyika juzi katika ufukwe wa Mbalamwezi uliopo jijini Dar es Salaam.

WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA WA VITABU KUTOKA KWA WATU WA MAREKANI!

Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Mkuu wa shule za maabara za Sayansi, Muhimbili Mr. Colman Msuya vitabu vya maabara za Sayansi vilivyotolewa leo jijini Dar es salaam kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia shule na vyuo mbalimbali vya sayansi nchini.
Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Mkuu wa chuo cha maabara Litembo kilichoko wilayani Mbinga mkoani Ruvuma sista Angelina Marry Kihwili vitabu vya maabara za Sayansi vilivyotolewa leo jijini Dar es salaam kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia shule na vyuo mbalimbali vya sayansi na Afya nchini.Katikati ni mwakilishi wa USG PEPFAR kutoka Marekani Dkt. John Grove.

Wakuu wa vyuo na shule mbalimbali za Sayansi nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya sayansi za maabara kutoka kwa watu wa marekani leo jijini Dar es salaam.Vitabu 1920 vyenye thamani ya shilingi milioni 91 vimetolewa na kukabishiwa kwa wakuu wa vyuo hivyo.

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akiangalia vitabu mbalimbali vya sayansi vilivyotolewa kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia elimu ya Sayansi nchini.Kulia ni mwakilishi wa USG PEPFAR kutoka Marekani Dkt. John Grove.


Urusi yaomboleza rasmi!!


Huku Urusi ikiwakumbuka rasmi na kuomboleza vifo vya watu 39 katika mashambulio ya kujitoa mhanga katika vituo vyake viwili vya treni mjini Moscow siku ya Jumatatu, Rais Dmitry Medvedev amewataka maafisa wa serikali kutunga sheria mpya kupambana na ugaidi.
Ametamka hayo huku Warusi wakiitenga siku ya Jumanne katika kuomboleza.
Warusi wamekuwa wakiwasha mishumaa na kuwacha maua mahali ambako milipuko hiyo miwili ilitokea.
Magazeti ya Urusi yamekuwa yakiilaumu serikali kwa kukosa kuzingatia kikamilifu suala la usalama kwa jumla.

MDAU JANE JOHN WA TBC1 NA MAMBO YA KUBLOG!!

NAITWA JANE JOHN MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI NCHINI TBC .NIMEFUNGUA BLOG AMBAYO ni janejohn5.blogspot.com hivyo nawakaribisha watanzania wote kuangalia ili mjionee mambo mbalimbali ya michezo,burudani na mengine mengi ambayo yatakuelimisha. pia unawezea kutuma maoni.

KARIBU

TBL YAINGIZA MILIONI 850 MASHINDANO YA KILI TAIFA CUP!!

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Tanzania Breweriers Limited (TBL)David Minja akiongea mbele ya wanahabari leo wakati kampuni hiyo ilipotangaza udhamini wa jumla ya milioni 850 kwa ajili ya mashindano ya Kili Taifa Cup yanayotarajiwa kuanza mei 8 aprili mwaka huu.
Davidi Minja amesema vituo sita vitatumika katika mashindano hayo ambavyo ni Arusha, Mtwara, Tanga, Iringa, Mwanza na Dodoma, robo fainali za mashindano hayo zitafanyika kuanzania aprili 22 na fainali zitafanyika aprili 30 mwaka 2010.
Wengine wanaoonekana katika picha kushoto ni Ferdrick Mwakalebela Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF na kulia ni George Kavishe Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambayo ndiyo inadhamini mashindano hayo.
Wanamuziki wa bendi ya Mjomba Band wakiimba wakati wa uzinduzi wa kombe la taifa Kili Taifa Cup uliofanyika katika ofisi za kiwanda cha Tanzania Breweriers Ilala jijini Dar es salaam leo


MPANGO WA TAIFA WA UZAZI WA MPANGO WAZINDULIWA JIJINI!!

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akimsikiliza Angelina Mchome mratibu wa afya ya uzazi wa mpango shirika la PSI wakati alipokuwa akimpa maelezo juu ya viwango vya matumizi ya Kondom aina ya Familia wakati wa uzinduzi wa mpango wa Taifa wa Uzazi wa mpango uliofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es asalaam leo.

TIMU YA TAIFA YA JUDO KWENDA NAIROBI KESHO!!


Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Nchini Idd Kipingu akimkabidhi Bendera ya Taifa Kapteni wa timu ya taifa ya Judo wakati chama cha judo nchini JATA kilipofanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea maadalizi yao na safari yao ya kwenda nchini Kenya katika jiji la Nairobi ambako mashindano ya kanda ya (5) baraza la Afrika katika mchezo wa judo yatayofanyika kuanzia 2-3 na baadaye yatafuatiwa na mazoezi ya pamoja kwa timu zote zitakazoshiriki katika mashindano hayo.
Timu inaondoka kesho alfajiri na inatarajiwa kurejea nchini tarehe 7/4/2010 na wachezaji wanaoondoka ni Omary Yusuf Ngowe, Andrew Thomas, Abuu Selemani, Athuman Abdalla na Zaidi Khamis (uzito wa kg60) wengine ni Fokas Mkude, Mohamed Korogombe, Philip Sabini (uzito kg66), Gervas Leonard, James Mapunda, Richard Martin (Uzito 73kg), Niclaus Mkinga, Gervas Taitas, Seif Malulu (Uzito81kg) na Eduward Nanda Mbambala (Uzito 90kg).
Wasichana ni Mary Francis, Latifa Mbezi (Uzito 63kg) na viongozi ni Kashinde Shaban Katibu Mkuu wa JATA na kocha wa timu hiyo Jose Valdes Silva na Hassan Mlilo Kiongozi wa Msafara, katika picha kushoto ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya judo Jose Valdes Silva.

Champions league to sparkle on SuperSport!!


The UEFA Champions league draw has dished up a plethora of mouth-watering quarter-final clashes.
The drama and intrigue of the first leg of the quarterfinals will be broadcast live on SuperSport on Tuesday and Wednesday (March 31).
In arguably the pick of the last-eight ties, Arsenal tackle reigning champions Barcelona.
The Catalan giants – a side every team surely wanted to avoid – will be a tough proposition with Lionel Messi, the sparkling jewel in their crown, in fine fettle.
But if anyone can match their high-tempo, free-flowing style of play – it’s the Cesc Fabregas-led Gunners.
The first leg will be staged at the Emirates this Wednesday, with Arsenal intent on avenging their 2006 final defeat.
Last term’s losing finalists, Manchester United, face a tricky away tie to the only German side left in the competition, Bayern Munich.
Will Wayne Rooney continue his majestic goal-scoring form, or will Arjen Robben inspire the German giants?
In an all-French clash, Lyon and Bordeaux will battle it out for the rights to be acclaimed France’s premier Champions League side.
The fact that these Ligue 1 rivals have been drawn together ensures the French a semi-finalist for the first time since 2004.
Keep an eye out for Bordeaux’s Moroccan striker Maroune Chamakh, keen to enhance his reputation on the big stage ahead of his proposed summer move to the Gunners.
In another unpredictable clash, Chelsea-beaters, Inter Milan, will be intent on sending first-time quarter-finalists, CSKA Moscow packing.
The enigmatic, ever-colourful Jose Mourinho will be plotting the Russian side’s downfall, with Inter’s impressive defensive rearguard likely to come to the fore in this clash.
The stakes are as high as ever with the semi-final draw having also been unveiled.

The winner of the United and Bayern clash tackle Lyon or Bordeaux, while Inter or CSKA face either Arsenal or Barcelona.
Live every moment of the business end of the Champions League live on Your World of Champions.
Viewers are invited to go to http://www.supersport.com/ or press the OK button on the DStv remote control for additional info, highlights and other match fixtures

Mpendazoe aondoka CCM na kujiunga na chama cha CCJ!!

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ).

Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe (katikati) akitangaza kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam juu ya nia yake ya kuondoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) . Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise na kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCJ Dickson Nghilily.
Picha na Tiganya Vincent-Dar es salaam


Mama Salma Kikwete akiwa ziarani mkoani Mara!!

Mkurugenzi Mkuu wa Singita Grumeti Reserves Bwana Graham Ledger,kulia, akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kazi za taasisi ya WAMA. Makabidhiano hayo yalifanyika katika hoteli ya Grumeti iliyoko katika hifadhi ya Serengeti .

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia mamia ya wananchi wa kijiji cha Nyamuswa, wilayani Bunda mkoani Mara, wakati akielekea mjini Bunda kukagua shughuli mbalimbali za akinamama wajasiriamali wilayani humo.

Rais Bashir aonya wapinzani wake!!


Saa chache kabla ya mkutano wa viongozi wa upinzani nchini Sudan, ambapo wanatarajiwa kutangaza kuwa wanataka uchaguzi uhairishwe, Rais Omar al Bashir ameonya ikiwa watasusia uchaguzi hataruhusu kura ya moani kuhusu kujitawala kwa Sudan Kusini ifanyike mwaka 2011.
Rais Bashir ambaye amekuwa akitoa matamishi makali wiki chache kabla ya uchaguzi huo amenukuliwa na vyombo vya habari nchini humo, akitoa onyo hilo wakati wa kampeni mjini Khartoum.
Chama chake cha National Congress Party ( NCP) kinasisitiza kuwa uchaguzi lazima ufanyike Aprili 11.
Lakini vyama vya upinzani kikiwemo kile cha Sudan's People Liberation Movement (SPLM), kinachotawala kusini mwa nchi hiyo, vinataka shughuli hiyo ihairishwe.
Viongozi wa vyama hivyo wanasema hawaamini kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.
Kundi la waangalizi kutoka shirika linaloongozwa na rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, limekiri kuna matatizo mengi ya utaratibu wa kuandaa uchaguzi huo na wanaunga mkono ucheleweshwe.
Uchaguzi huo unafanyika kulingana na makubaliano ya amani yaliotiwa saini na utawala wa Khartoum na waliokuwa waasi wa SPLA mwaka wa 2005.
Kwenye makubaliano hayo, pande zote mbili pia ziliafikiana kuwa kura ya maoni ipigwe mwaka wa 2011 ili raia wa kusini mwa Sudan waamue ikiwa watajitawala.

TAARIFA KWA UMMA


Tarehe 17 Machi, 2010, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na hivyo Muswada huo kuwa Sheria Kamili. Muswada huo ulipitishwa tarehe 11 Machi 2010 katika Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivi karibuni, Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alitoa madai kwamba kuna kifungu kidogo cha (3) ambacho kimeingizwa katika kifungu cha 7 cha Sheria hiyo isivyo halali au “kinyemela”. Kifungu kidogo cha 7(3) kinaweka masharti yanayohitaji uthibitisho wa wajumbe wanaounda Timu za Kampeni za Wagombea wa Kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani. Mheshimiwa Dk. Slaa anadai kwamba kifungu cha 7(3) hakikuwepo kabisa kwenye Muswada wa Sheria uliojadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.

Kwa kuzingatia madai ya Mheshimiwa Dk. Slaa, Vyombo vya Habari vimekuwa vikitoa maelezo mbalimbali kuhusu suala hili. Katika mazingira haya, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa Taarifa kwa Umma yenye lengo la kufafanua kile kilichotokea Bungeni hususan uandishi wa kifungu cha 7(3) katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Kutokana na marekebisho yaliyopendekezwa na Wadau na Wabunge, Bunge liliagiza Muswada uchapishwe kwa mara ya pili. Baada ya Muswada huo kuchapishwa kwa mara ya pili, kifungu cha 7 hakikuwa na vifungu vya (1), (2) na (3). Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja zaidi zilizotolewa na Wabunge kuhusu makundi ya Sanaa na Viongozi wa Vyama wanaoweza kumsaidia Mgombea wakati wa Kampeni za Uchaguzi, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge) Mhe. Philip S.Marmo, iliandaa Jedwali la Marekebisho ambalo lilifanya marekebisho katika kifungu cha 7.

Marekebisho hayo ni:

(a) kukitaja kifungu cha 7 kilichokuwepo kuwa kifungu kidogo cha (1) katika kifungu hicho hicho cha 7.

(b) kuongeza kifungu kidogo cha (2) ili kuongeza makundi ya sanaa na kundi la watu wanaoweza kufadhiliwa na Mgombea kwa chakula, vinywaji, malazi na usafiri wakati wa Kampeni za Uchaguzi.

Kwa kuwa uamuzi huu ulifanyika wakati wa Kamati ya Bunge Zima, Mwenyekiti aliagiza kwamba suala hilo la kuweka marekebisho hayo, lizingatiwe wakati wa kutoa tafsiri ya maneno “timu ya kampeni”. Kwa kuzingatia mapendekezo ya Mhe. William H. Shellukindo kwamba idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu. Katika kutekeleza hayo, kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati “Timu ya Kampeni” iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika. Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.

Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya “Timu ya Kampeni” ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika “Timu ya Kampeni”. Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa, kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge.

Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. Katika hatua hii, Wabunge wanaweza, kupitia Kanuni ya 86(II) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, kupendekeza mabadiliko katika Muswada. Endapo Waziri ataafiki mapendekezo ya Mbunge yeyote,atamjulisha Mwenyekiti na Mwenyekiti akiridhia atamuelekeza Mbunge aliyetoa mapendekezo asome maelezo anayotaka yaingizwe kwenye Muswada. Ikiwa Mbunge aliyependekeza marekebisho hayo hana maelezo mahsusi, Mwenyekiti atamuagiza Katibu wa Bunge ashirikiane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka maneno au Kifungu kinachoweka masharti yenye maudhui aliyopendekeza Mbunge. Mwenyekiti atawahoji Wabunge kama mapendekezo yakubaliwe au la, wakikubali basi waandishi watakwenda kuandika kifungu kwa namna ambayo inatafsiri nia na uamuzi wa Bunge.

Kwa kuzingatia maelezo haya kuhusu hoja za Wabunge ninaridhika kuwa kifungu cha 7(3) cha Sheria ya Uchaguzi kimezingatia matakwa na maagizo ya Bunge sawa sawa. Kifungu hicho hakikuingizwa kwenye Sheria “kinyemela” au kwa hila. Aidha, mtiririko wa mamlaka za kuthibitisha Timu ya kampeni una mantiki sahihi yenye lengo zuri la kufanikisha shughuli za uchaguzi kwa ufanisi.


Imetolewa na
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
29 Machi, 2010

Kuongezeka kwa malalamiko ya wauguzi katika Hospitali ni changamoto!

Na. Catherine Sungura,MOHSW
Kuongezeka kwa malalamiko kuhusu ubora wa huduma za afya zinazotelewa zikiwemo za uuguzi karibu mikoa yote nchini ni dalili kuwa huduma inayotolewa inakabiliwa na changamoto nyingi.
Hayo yametolewa leo jijini hapa na Waziri wa afya na ustawi wa jamii Profesa David Mwakyusa katika mkutano wa kutoa taarifa kwa wadau juu ya utekelezaji wa mpango wa kuimarisha elimu ya maadili kwa wauguzi na wakunga nchini.
Profesa Mwakyusa alisema kuongezeka kwa malamiko hayo katika sekta ya afya inatokana na wauguzi kutumia kauli mbaya,lugha isiyofaa kwa wagonjwa pamoja na kutozingatia sheria na miongozo iliyowekwa ya uuguzi hivyo kupelekea ufanisi mdogo wa fani hiyo.
“Suala la maadili ni la kudumu hivyo kila wakati lazima lizungumziwe na liwe somo la kutahiniwa katika vyuo vyetu vyote vya wauguzi ili vijana wawe na msingi mzuri wa maadili na wakazane kulisoma kama masomo ya taaluma”.
Aidha aliwasihi wale wote waliopata mafunzo wawe chumvi itakayosambaa kila mahali na kutekeleza mikakati ili huduma za afya ziwe za kurudhisha na kuboreshwa ili kuona malamiko pamoja na vifo vinavyoepukika vinapungua.
“Katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia baadhi ya malaengo yanakwamishwa na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya watendaji wenzetu, kwa kuzingatia kuwa wauguzi na wakunga ni asilimia 50 ya watoa huduma ni wajibu wenu kujituma na kutoa mchango katika kuinua hali ya afya na kuzuia vifo vinavyoweza kuepukika”malengo hayo hatatafikiwa ikiwa hakutakuwa na wauguzi waadilifu na wenye upole, aliongeza.
Hatahivyo aliseam serikali inaendelea kutoa hamasa kwa akina mama kujifungulia katika vituo vya afya na kuwakinga akina mama na watoto na ugonjwa hatari wa malaria kwa kuwapatia hati punguzo za vyandarua vilivyowekwa dawa pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu wa sekta ya afya na vituo vya kutolea huduma hadi katika ngazi za vijiji.
Jumla ya waauguzi na wakunga 304 toka kanda sita nchini ikiwemo mbeya, mtwara, moshi,morogoro, Dodoma na mwanza wamepatiwa elimu ya maadili ya wauguzi na wakunga ambayo yanaratibiwa na baraza la wauguzi na wakunga nchini na kufadhiliwa na mfuko wa uadilifu,uwajibikaji na uwazi,ofisi ya Rais,sekkretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini.

WANARIADHA NA MAKAMPUNI KUSHIRIKI MBIO ZA LIVE EARTH RUN FOR WATER!!


imetajwa kua miongoni mwa moja ya miji ya kimataifa inayoshiriki katika changamoto ya kihistoria yakusaidia kutatua janga la maji ulimwenguni. Aprili 18,2010 Ndani ya masaa 24, nchi mbalimbali ulimwenguni zitashiriki katika tukio liitwalo DOW Live Earth Run For Water litakalojumuisha mfululizo wa mbio/matembezi ya km6 (km6 ni wastani wa umbali ambao wanawake na watoto wengi duniani hutembea kila siku kutafuta maji safi) zikishirikisha matamasha na shughuli zinazoelimisha masuala ya maji yanayolenga kuhamasisha mbinu za kusaidia kutatua janga la maji.
Hapa Tanzania Dow Live Earth Run for Water itajumuisha matembezi ya km6 na mbio za km15 zikianzia na kuishia nje ya uwanja mpya wa taifa ambapo mbio za kukimbiza Mwenge wa olompiki wa mwaka 2008 zilifanyikia. Mazoezi ya kupasha joto mwili yataanza saa 11:30 asubuhi, bendera ya mbio itapeperushwa saa 1asubuhi na bendera ya matembezi itapeperushwa saa 2 asubuhi. Tumepanga kuanza asubuhi na mapema ili baadae washiriki wa mbio na matembezi pamoja na watazamaji waburudike na tamasha la bure likishirikisha wasanii maarufu nchini Tanzania kama WITNESS, MH.TEMBA, CHIDI BENZ, AT, MIKE TEE na DIAMOND MUSICA. Pia kutakuwa na mfano wa vijiji vya maji kusisitizia umma juu ya uvumbuzi wa janga la maji. Tunawapa changamoto wananchi wote ,makampuni,taasi za kiserikali na zisizo za kiserikali kuungana na kuwa sehemu ya juhudi za ulimwengu za kutatua janga hili kubwa linaloathiri karibu moja ya nane ya idadi ya watu duniani.
“Janga la maji ni miongoni mwa kikwazo cha afya‘ alisema Berta Ikua-Akaunti Meneja wa Kampuni ya Spearhead Africa ‘Lakini suluhisho lipo, Tukio la Dow Live Earth Run for Water hapa Dar es Salaam ni moja ya njia ya kukusanya jamii duniani juu ya suala tete la upungufu wa maji na kuwapa wananchi uwezo na nafasi ya kuwa sehemu ya suluhisho’.
Ukosefu wa maji ni suala linaloathiri nchi,jamii na familia mbalimbali duniani kote.Mmoja kati ya watu nane hawana njia ya kupata maji safi na salama.Jamii mbalimbali barani Afrika ,Amerika ya Kusini na Asia zinakabiliwa na vifo vya watu milioni moja nukta nane kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuhara;vifo vya watoto elfu tano( 5000) kila siku kutokana na miundombinu ya maji isiyotosheleza kila sikui. Katika maeneo haya wanawake na watoto hulazimika kutembea kilomita sita (maili 3.7) kutafuta maji ambayo yamkini hayafai kwa kunywa. Hata hivyo janga hili la maji halipo katika nchi zinazoendelea tu,bali katika miji kama vile Los Angeles na Sidney. Pamoja na mambo haya yote , Mabadiliko ya hali ya hewa yanachangia kutokupatikana maji safi na salama duniani kote.
Kila mtu anahesabika katika kusaidia kutatua janga la maji. Dow Live Earth for Water ni mkakati ulimwenguni ambao unalenga kitendo cha kila mtu mmoja kua na uwezo wa kuchukua hatua kushughulikia kikamilifu suala hili. Watu wanapewa changamoto KUANZA kutatua tatizo hili leo, OKOA maji; tumia juhudi ya kuhifadhi maji kuanzia kwenye familia hadi ngazi ya jamii, TOA fedha ili kuchangia miradi ya maji safi na salama na SAIDIA kwa kushirikiana kwa njia moja au nyingine na waratibu wa tukio kuhamasisha kueneza habari nchini Tanzania kuhusu changamoto hii.
Baadhi ya miji inayoshiriki kwenye Dow Live Earth Run for Water ni Buenos Aires- Argentina,Cape Town-Afrika kusini, Chicago-Marekani, Hongkong -China, London- UK , Los Angeles-CA -USA, Melbourne -Australia, Mji wa Mexico ,Mineapolis,-Marekani, Newyork -USA,Rio de jenero- Brazil, Singapore,Stockholm -Sweden.
“Tunafuraha kutangaza kuwa Benki ya Exim Tanzania na TIGO ndio wadhamini wakuu wa Dow Live Earth Run for Water Dar es salaam”,alisema Bertha Ikua. “Ikiwa ni sehemu mojawapo ya malengo yao endelevu ya 2010, wamejitolea kutumia teknolojia kusaidia kutatua baadhi ya vikwazo vikubwa duniani kama janga la maji. Wadhamini wengine ambao tunapenda kuwashukuru ni Cool Blue, Reni International, Davis and Shirtliff, Image Masters, A1 Outdoor, Southern Sun, Hugo Domingo, What’s happening in Dar na Geita Gold Mines, ambao wamechukua hatua kuunga mkono tukio hili kubwa la ulimwenguni.
Lengo mojawapo la tukio hili ni kuwahamasisha kila mmojawetu na makampuni kuchangia kiasi chochote wanachopenda na kuwasajili wafanyakazi wao wengi iwezekanavyo kwa ajili ya mbio na matembezi na sehemu ya fedha za usajili zitazopatikana zitakwenda kwenye shirika lisilo la kiserikali liitwalo PRACTICA FOUNDATION ambalo shabaha yake ni kutengeneza vituo 20 vya maji salama (vinavyofanya kazi )kwa ajili ya watu 3000 Njombe Iringa. Asilimia mia ya michango yote itakwenda PRACTICA FOUNDATION.

BLOGU MPYA YA MUZIKI NA MAISHA IKO HEWANI!

Mimi ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha redio cha 87.8 Ebony fm cha Iringa lakini mimi niko Dar-Mini Studio, naitwa Renatus Kiluvia,ni mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa blog mbalimbali , blog yangu mpya niliyoianzisha inaitwa http://www.muzikinamaisha.blogspot.com/,blog yangu inahusu muziki na maisha katika nyanja tofauti-tofauti,pia itahusika kuzungumzia burudani zingine kama filamu n.k.
Akhsante!!!!!!!!!!!

Rais Kikwete apokea vifaa mbalimbali kutoka China!

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng mara baada ya kuwasili Ikulu leo jijini Dar es salaam kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiweo vifaa vya usafiri, vifaa vya nyumbani na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 51.
Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO.
Rais Jakaya Kikwete akiagalia msaada wa baiskeli zilizotolewa na nchi ya China ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 51 vilivyotolewa na nchi hiyo leo Ikulu jijini Dar es salaam.Kulia kwake ni Balozi wa China Liu Xinsheng aliyekabidhi msaada huo.

Rais Jakaya Kikwete akikagua pikipiki ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na nchi ya China kupitia kwa Balozi wa nchi hiyo Liu Xinsheng (kulia) kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo nchini. Makabidhiano hayo ya vitu mbalimbali vikiweo vifaa vya usafiri, vifaa vya nyumbani na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 51 yamefanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.