RAIS JAKAYA KIKWETE AWAPANDISHA VYEO MAKAMANDA WA POLISI NCHINI

Na Mohammed Mhina na Athumani Mtasha wa Jeshi la Polisi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 42 wa Jeshi la Polisi kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, imesema kuwa waliopandishwa vyeo kuanzia Machi 16, mwaka huu ni pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa tisa, Makamanda watano wa vikosi na Wakuu wa Vitengo mbalimbali vya Jeshi hilo waliopo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam na Zanzibar.
Kamanda Mssika amesema kati ya hao wapo Maafisa wanne wakuu ambao wamepandishwa vyeo kutoka vyeo vyao vya zamani vya Makamishna Wsaidizi Wandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Manaibu Makamishna wa Polisi (DCP).
Walipandishwa kuwa Manaibu Kakamishna wa Polisi (DCP’s) ni Mkuu wa Huduma za Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi SACP Isaya Mngulu, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Afya nchini SACP Neven Mashayo, SACP Rashid Omari Ali, wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACPO Suluiman Kova.
Kamanda Mssika amewataja Makamanda 38 wakiwemo Makamanda wa Polisi wa Mikoa tisa ya Tanzania Bara na Visiwani kutoka Vyeo vya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP ambao sasa kila mmoja anakuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) ambao ni Makamanda Thobias Andengenye wa Morogoro, Henry Salewi wa Kagera, Bi Celina Kaluba wa Singida na Kamanda Lucas Ng’hoboko wa Kilimanjaro.
Wengine ni Kamanda Absalom Mwanyoma wa Pwani, Simon Sirro wa Mwanza, Isuto Mantage wa Rukwa, Michael Kamhanda wa Ruvuma na Yahaya Rashidi wa mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kamanda Mssika amewataja Makamanda wa Vikosi waliopandishwa vyeo kuwa ni Mohammed Mpinga, wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Tresphory Anaclet wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini (FFU), Sospeter Kondela, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Ujenzi, Geofrey Nzoa Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na kupambana na Madawa ya Kulevya na Mkuu wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam Bi. Alice Mapunda.
Wengine ni Mkuu wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini Kamanda Hussein Nassoro Laizer, Mkuu wa Bohari Kuu la Polisi nchini Kamanda Adriano Magayane, Mkuu wa Kikosi cha Usafirishaji cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Kamanda Ali Mlege na Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Jonas Mgendi.
Wengine ni Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania kwenye Ofisi za Interpol Kanda ya nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika Kamanda Goodluck Mongi, Mkuu wa Kitengo cha Picha na Maabala ya Uchunguzi wa Vielelezo vya Makosa ya Jinai nchini (FB) Kamanda Hezron Gyimbi.
Wengine ni Kamanda Jamal Rwambow, Kamanda Lucas Haule na Kamanda Donald Ludamila wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Makao Makuu, Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Lucas Kusima, Kamanda Saidi Juma Hamis kutoka Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu.
Kamanda Mssika amesema kuwa wengine walipandishwa ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mifumo ya Mitangao ya Kompyuta ya Jeshi la Polisi nchini kamanda Anyisile Kyoso, Kamanda Renatus Chalamila, Mwanasheria wa Jeshi la Polisi nchini Kamanda Donald Kaswende na Kamanda mwanamke Adolfina Chialo.
Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Abdulrahman Kaniki, Msaidizi wa Mkuu wa Operesheni Maalum nchini Kamanda Hezron Kigondo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zananzibar Kamanda Mussa Alli Mussa na Kamanda Hamdani Makame wa Ofisi ya Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Mkuu wa Mipango Kamanda Ernest Mangu, , Kamanda Makame Ali Makame, Kamanda Mwalim Ame na Kamanda Mpinga Gyumi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment