SIMBA YAFIKISHA POINTI 42 BAADA YA KUIBANJUA TOTOAFRICA!!

Kikosi cha Simba.
Latika mfurulizo wa michezo ya Ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba ya jijini Dar es salaam Leo ikicheza na timu ya Toto Africa ya mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba imeibanjua timu hiyo magoli 2-0 katika mchezo mkali uliochezwa jijini humo.
Timu ya simba katika kipindi cha kwanza ilitoka bila kupata goli kutokana na wachezaji wa Toto Africa kucheza kwa nguvu katika kipindi chote huku wakiikosesha raha za mapema timu ya Simba iliyokuwa ikipata upinzania kwa nguvu katika kipindi hicho.
Hata hivyo katika kipindi cha kwanza Simba iliingia uwanja kwa nguvu na ari kubwa kitu kilichopelekea wachezaji wake Muss Hassan Mgosi na Ramadhan Chombo Redondo kupachika magoli katika dakika za 50 na 54 hivyo timu hiyo kuibuka kidedea katika uwanja huo mgumu kwa timu ya Simba.
Katika mchezo wa leo Simba imejikusanyia pointi tatu muhimu hivyo kuifanya izidi kupaa katika msimmamo wa Ligi kuu ya Vodaco kwa kuwa na jumla ya pointi 42.

WAZIRI WA ULINZI DR. HUSSEIN MWINYI NA MBUNGE HAMAD RASHID!!

Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Wawi(CUF) Hamadi Rashid akibadilishana mawazo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi(kulia) katika viwanja vya Bunge Mkutano wa 18 wa Bunge unaendelea mjini Dodoma leo.

PIUS MSEKWA AWASIMIKA MAKAMANDA WA CCM!!

Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa akiwahutubia vijana jana mjini Dodoma juu ya umuhimu wa kushikamana na kujenga umoja wakati wanaelekea katika Uchaguzi Mkuu. Msekwa alisema hayo mara baada ya kuwasimika Makamanda wa UVCCM wa wilaya zote za Dodoma na yule wa Mkoa katika Sherehe zilizofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Taifa mjini Dodoma
Makamanda wa CCM wa wilaya na Mkoa wa Dodoma .kKutoka kulia ni Hezekiah Chibunje,huyo ni Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, anyefuata ni Zabein Mhita yeye ni Kamanda wa UVCCM Kondoa Kaskazini, Job Ndugai , Kamnda wa UVCCM Kongwa na Laurent Hoya yeye anakuwa Kamanda wa UVCCM Chamwino.


Mourinho: No red carpet for Eto'o!!

Samuel Eto 'o.

Inter Milan coach Jose Mourinho has warned Samuel Eto'o he will have to fight for his place after returning from Africa Cup of Nations duty.
Diego Milito, new arrival Goran Pandev and Mario Balotelli have made sure Cameroon talent Eto'o has not been missed over the last month and Mourinho has not called Eto'o up for the leaders' visit to Parma today.
The trio's efforts have helped champions Inter to stretch their lead over second-placed AC Milan, who have played one game fewer, to nine points, with Milito and Pandev scoring the goals in last week's 2-0 win over their city rivals.
Balotelli scored the last-gasp goal that took Inter into the Italian Cup semi-finals with a 2-1 win over Juventus on Thursday.
And Mourinho warned Saturday: "There will be no red carpet waiting for Eto'o. That might have happened with someone else, but not with me.

There will be no red carpet waiting for Eto'o. That might have happened with someone else, but not with me.
Inter Milan coach Jose Mourinho
"Samuel has to get back to 100 per cent and that's why, if he has not recovered from all the fatigue of the (Africa Cup of Nations), it's better to wait because it is very hard to start up front for Inter at the moment."
Eto'o did not train with his team-mates on Saturday, but had physiotherapy on a knock to his right foot that he suffered at the Africa Cup of Nations, the club reported.
Mourinho said he expects the visit to 12th-placed Parma to be especially tough, partly because of the team's recent exertions in beating Milan and Juventus, and partly because of Parma's "cunning" coach, Francesco Guidolin.
"It'll be a difficult match," said the Portuguese. "Guidolin is cunning, in the good sense of the word. He knows how to play with the players he has. Sometimes he adapts to the opposition, sometimes he changes formation, but he also knows how to build a team capable of playing (good football)."

Wamarekani wazuiliwa Haiti!!

Clint Henry mchungaji wa kanisa hilo!!
Serikali ya Haiti imewatia kizuizini Wamarekani kumi ambao inasema walikuwa wakijaribu kuwasafirisha nje ya nchi watoto wadogo bila idhini ya serikali.
Msemaji wa serikali ya Haiti, Yves Christallin, alisema Wamarekani hao walikamatwa na zaidi ya watoto thelathini kwenye mpaka na Jamhuri ya Dominica, ambako walisema walikuwa na kituo cha watoto yatima.
Msemaji huyo alisema Wamarekani hao hawakuwa na hati zinazothibitisha ikiwa watoto hao walikuwa ni yatima kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti hivi karibuni.
Wamarekani hao ni kutoka kanisa lenye makao yake katika jimbo la Idaho.
Mchungaji katika kanisa hilo, Clint Henry ameiambia BBC kuwa kundi hilo la Wamarekani limekuwa na hati zote zinazohitajika kufanya shughuli zao.

HAPPYWHITNER AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA UMODO!!

Mshindi wa shindano la UmodoHappywhitner Gumbo lililoandaliwa na blogu ya
www.umodo.blogspot.com inayoendeshwa na Taji Liundi akiwa katika picha ya pamoja na mama yake mzazi mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi jana, mwanamitindo huyo aliyeibuka kidedea kwenye shindano hilo amefanikiwa kujipatia mkataba wa mwaka mmoja kutoka kampuni ya Nywele na vipodozi ya Sheal Ilution ya jijini ambapo atakuwa akilipwa shilingi laki mbili kila mwezi hivyo zawadi yake kwa ujumla ikiwa ni milioni 2.4 pamoja na kupewa huduma za urembo katika duka hilo zenye thamani ya shilingi laki moja pia atakuwa akifanya kazi za kampuni hiyo.
Yusuph Mlela akiongea mbele ya mashabiki wa mitindo wakati wa shindano la Umodo lililofanyika jana kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View katikati ni Sylivia na mwisho ni mchezaji wa filamu Kanumba.

Na huu pia
Angalia mtindo huu wa nywele
Hawa ndiyo wanamitindo wenyewe hapa wakipiga picha kuonyesha mitindo yao ya Nywele.
Wadau Carolin kushoto na Upendo kutoka kampuni ya TSN inayochapisha magazeti ya Dairlynews na Habari leo.
Yusuph Mlela kushoto na Kanumba ndiyo walikouwa majaji katika kuwapata wanamitindo walioingia fainali ya Umodo.

Wadau Neema kushoto na Jack kutoka Sheal Ilution kampuni iliyodhamini shindano hilo la Umodo lililofanyika kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach Jana.

Wadau wa chama cha wanamitindo Tanzania wakionyesha pozi zao katika picha.

Mbunifu wa mavazi Farha, Kemi na mwanamitindo Mgesi wakiwa katika picha ya pamoja.

JERRY MURRO ADAIWA KUNASWA NA POLISI KWA RUSHWA!!

Mwandishi wa habari Bora wa jumla mwaka 2009 kutoka Televisheni ta TBC Jerry Murro inadaiwa amekamatwa na polisi na yuko kituo cha polisi kati (Central) jijini Dar es salaam kwa mujibu wa blogu ya Issamichuzi.blogspot.com Jerry Murro alikamatwa leo jijini akitaka kupokea kitita cha shilingi milioni 10 kutoka kwa mwananchi mmoja katika mtego uliokuwa umetegwa dhidi yake
Kamanda wa polidi wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova anatarajiwa kutoa taarifa wakati wowote kuhusiana na sakata hilo na tutawaletea taarifa zaidi mara baada ya kupata taarifa zaidi.

President Kikwete meets Vietnam Prime Minister in Davos!

President Jakaya Mrisho Kikwete(right) in conmversation with Vietnam Prime Minister Nguyen Tan Dung(centre) and the chariman of the New Delhi Television Roy Prannoy(left) who was also the moderator during the debate on Global Food Security held at Davos Congress Hall yesterday evening(photos by Freddy Maro)

President Kikwete meets Bill Gates in Davos

President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the the Microsoft founder and Chaiman of the Bill and Melinda Gates Foundation, Bill Gates shortly after participating in a debate on improving Food Security held in at Davos Congress Hall, yesterday afternoon.(photos by Freddy Maro)


President Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a debate on improving agriculture production to boost food Security during the World Economic forum in Davos yesterday.On the left is Ellen Kullman Chair and CEO of of the US based DuPont company and on the right is Microsoft Founder and Chairman Bill Gates.

President Kikwete mets WTO Director General Pascal Lammy

President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with World Trade Organisation WTO Director General Pascal Lammy at Davos Congress hall in Davos yesterday evening during the last session of the World Economi Forum held in Davos Switzerland(photo by Freddy Maro).

President Kikwete meets ILO Director General Juan Somavia in Davos Switzerland this morning!

President Jakaya Mrisho Kikwete meets International Labour Organisation Secretary General Juan Somavia in Davos Switzerland this morning 30 January 2010, where he is attending the annual World Economic Forum, a forum committed to improve the state of the World economy.
A small tourist resort town of Davos Switzerland covered with snow this morning as delegates including distinguished world peronalities and celebrities attend the annual World Economic Forum.
(Photo by Freddy Maro)

MATUKIO YA BUNGENI DODOMA JANA!

Mwenyekiti wa Bunge Jenista Mhagama (kushoto) akibadishana mawazo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto, Magreth Sitta(katikati) na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Mary Nagu jana mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha 4 cha mkutano wa 18 wa Bunge uanoendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Habari , Utamaduni na Michezo Captain George Mkuchika (kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa CCM jimbo la Tandahimba Juma Njwayo jana mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha 4 cha mkutano wa 18 wa Bunge uanoendelea mjini Dodoma.
Picha zote na Tiganya Vincent, Dodoma

Anasema "message hii ifike kwa wachezaji na viongozi wa simba"

Mshabiki huyu wa Simba kutoka mkoa wa Mbeya katutumia ujumbe wake kwa viongozi wa timu ya Simba, wachezaji na mawakala na wanasimba kwa ujumla wake, akielezea juu ya kuwafanyia mipango ya kucheza mpira wa kulipwa wachezaji wa timu hiyo na zingine za hapa nyumbani hebu usome ujumbe wake alafu tutumie maoni yako mdau.

NDUGU WANASIMBA NI MIMI YULE YULE MDAU WENU WA SIMBA TAFADHALI MNAPOTAFUTA TIMU NJE PAMOJA NA KUTUMIA MAWAKALA PIE MUENDE WENYEWE, NCHI KAMA UINGEREZA, HISPANIA, UJERUMANI, UINGEREZA NA UFARANSA PAMOJA MUWE MNATUMIA INTRODUCTION MUENDE WENYEWE KWENYE HIZO TIMU MUWAMBIE TUMETOKA KLABU FULANI KAMA YA KWETU SIMBA NA MTACHUKULIWA TU KUTOKANA NA MIPIRA YENU NI YULE YULE RAFIKI YENU FRANCIS HENRY MULUNGU TEL 0755169421 OR 0754447495 THIS IS FOR MY MUMMY PAMOJA NA MAWAKALA PIA MJARIBU KUFANYA INTRODUCTION MTACHEZA TU KLABU KUBWA KAMA MONACO REAL MADRID MANCHESTER UNITED NA ZINGINEZO ZINAZOFAHAMIKA .GOOD LUCK NDUGU MWANDISHI BUKUKU NAOMBA MESSAGE HII UNIFIKISHIE KWA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA SIMBA .FRANCIS HENRY MULUNGU BOX 2553 MBEYA TANZANIA

HAFLA YA UMODOTZ.BLOGSPOT.COM KUFANYIKA KESHO GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL!!

Blogu ya umodotz.blogspot.com inawakaribisha wapenzi wote wa maswala ya mitindo, urembo na mavazi kwenye onyesho la wazi siku ya Jumamosi, Tarehe 30 Januari 2010 pale Giraffe Ocean View Hotel. Hafla hiyo imeandaliwa na umodotz blog kwa udhamini wa SHEAR ILLUSIONS, TRUWORTHS na GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL.

Hafla itaanza saa 12 jioni na kuisha saa 2 usiku.

Dhumuni kuu la hafla hiyo ni kuukaribisha rasmi mwaka 2010 kibiashara. Kuwatakia kheri wateja, marafiki, na washirika wa blogu pamoja na wadhamini kwa kuonyesha bidhaa mpya na huduma zao. Onyesho ni la wazi, hakuna kiingilio.

Watakaofika wataburudishwa na onyesho kali la mavazi ambalo litafanywa na mamodo 12 wa blog ya Umodotz. Watapita kwenye mavazi ya mbunifu mzoefu KEMMI KALIKAWE wa Naledi Fashions pamoja na mbunifu chipukizi MGESI. Nguo zote zitauzwa papohapo kwa watakaozipenda. Mamodo wamepambwa kichwani na nywele za Shear Illusions kwa mitindo tofauti iliyobuniwa na wataalamu wa urembo kutoka Paradise Uni-sex Salon (www.paradisespalon.cotz)

Shear Illusions itatoa mkataba mnono na wa kihistoria kwenye medani ya mitindo Tanzania kwa mmoja kati ya mamodo 12 wa blog ya Umodo. Mkataba huo ni wa mwaka mzima! Bila shaka utampa modo fursa nyingi za kufahamika kutokana na picha katika jarida la Shear na bango za matangazo.

Mkataba utaenda kwa msichana ambaye ataonyesha ana uwezo mkubwa wa kuwa modo wa kipekee siku hiyo.

Hili sio shindano. Mamodo 12 wa Umodo walipatikana kwa mchakato wa muda mrefu wa kuwachujwa na kuchaguliwa mmoja mmoja hadi kufikia 12.

Blog ya Umodo ilipata ushauri wa watu mbalimbali kama Steven Kanumba(filamu), Slyvia Shao(Urembo) na mbunifu Kemmi Kalikawe (mitindo) ambao wanawakilisha nyanja mbalimbali zinazoshabiiana na maswala ya mitindo.

Umodotz.blogspot.com inawakaribisha wote. Tunatumaini kuwaona mamodo wengi, wabunifu tele, wapenda mitindo, urembo na mavazi, watu maarufu katika nyanja mbalimbali, wafanya biashara, viongozi, watangazaji, waandishi, vijana na watu wazima. Hii ni nafasi nzuri kufahamiana katika jitihada za kukuza fani ya Mitindo Tanzania.

President Jakaya Mrisho Kikwete meets Tsvangirai in Davos!

President Jakaya Mrisho Kikwete meets Zimbabwean Prime Minister Morgan Tsvangirai in Davos yesterday evening.
President Jakaya Mrisho Kikwete contributes during a debate on Catalyising a New Vision for Agriculture held in Davos Switzerland during the on going World Economic Forum.On the left is former UN Seceretary General Koffi Annan and centre is a participant who could not immediately be identified.
President Jakaya Mrisho Kikwete leads a discussion during a Business Interaction Group on Tanzania held at Davos Congress Centre in Switzerland.From left are other delegates accompanying the President at the World Economic Forum, they include The Minister for Agriculture Steven Wassira, The minister for Health and Social Welfare Prof.David Mwakyusa, The discussion Moderator Mrs.Maria Ramos, President Kikwete, Minister for Home Affairs Lawrence Masha and the Central Bank Governor Beno Ndullu(photo by Freddy Maro)

SAFARI MOJA IKAANZISHA NYINGINE KWA JAMAA HUYU!!

Mkazi mmoja wa jiji la Dar es alaam ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa ameshikilia chupa yake ya bia aina ya safari lager na glasi ya pombe hiyo huku akiwachekesha wapita njia katika mtaa wa Samora, haikufahamika kama pombe hiyo alitoka nayo kwenye klabu gani iliyo karibu na jengo la IPS mtaa wa Samora tukio hilo limetokea leo asubuhi majira ya saa 4:30.

WATANI WA JADI KUSAKA POINTI WIKIENDI HII!!

Watani wa jadi Simba na Yanga.

Timu za Simba ya Jijini Dar es salaam na Yanga ya jijini pia ambao ni watani wa jadi katika mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini zinatarajia kushuka dimbani wiki hii katika viwanja tofauti ikiwa ni mfurulizo wa michezo ya Ligi kuu ya Vodacom mzunguko wa pili.
Wakati Simba itakuwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ikitifuana na timu ya Toto Afrika ya mkoani humo siku ya jumapili , Yanga itakuwa ikimenyana na timu ya Majimaji kutoka mkoani Ruvuma kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam hapo kesho siku ya jumamosi .
Afisa habari wa Timu ya Simba inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 39 akizungumza na mwandishi wa FULLSHANGWE kwa njia ya simu Cliford Ndimbo, amesema timu ya Simba imejiandaa vyema ili kuikabili timu ya Toto Africa, na wachezaji wote wako katika morali ya ushindi wa mchezo huo ili kujiwekea mazingira bora ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2009/2010, isipokuwa mchezaji Amri Kiemba ambaye ni majeruhi na amebaki Dar es salaam kwa matibabu.
Naye Msemaji wa timu ya Yanga Louis Sendeu amesema japokuwa baadhi ya magazeti yameripoti kwamba timu yake ina majeruhi sio kweli, kwani hakuna majeruhi hata mmoja na timu iko tayari kuisasambua timu ya Majimaji ya Songea ili kuhakikisha tunajiwekea mazingira mazuri ya kuwafikia wapinzani wetu Simba.

MTOTO HAKUI KWA MAMA JAMANI!!

Mchezaji wa NBA Memphis Grizzlies HasheemThabeet,akionyesha upendo kwa mama yake mzazi.Don't miss the GAME TODAY: Memphis Grizzlies Vs San Antonio Spurs, Jan 29 8:30pm at ET.source
www.Mohammeddewji.com/blog

TCCIA SME-SMS HELPLINE!


Blair kuelezea mashambulizi ya Iraq!

Waziri mkuu mstaafu wa Uingereza Tony Blair.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair anatarajiwa kutoa ushahidi mbele ya kamati inayochunguza kuhusika kwa Uingereza kwenye vita vya Iraq vya 2003.
Bwana Blair atahojiwa kwa muda wa saa 6 kuelezea sababu zake za kuunga mkono uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka wa 2003.
Uingereza iliunga mkono vita hivyo kwa misingi kuwa Iraq ilikuwa na silaha za maangamizi makubwa. Blair anatarakiwa kueteta uamuzi wake kuwa rais Saddam Hussein alikuwa na uwezo na nia ya kuunda silaha za maangamizi ya halaiki.

Siku ya ukoma duniani kuadhimishwa moani Morogoro!

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Dr. AishaKigoda akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tamko la sikuya ukoma duniani.Kilele cha siku ya ukoma itaadhimishwa wilayani Kilombero mkoani Morogoro, tarehe 31 januari,2010.(Picha na CatherineSungura-MOHSW
Waandishi wa habari za Bunge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afyana Ustawi wa Jamii, Mh.Dr. Aisha Kigoda wakati akitoa tamko la siku yaukoma duniani,mjini dodoma.

TBL YAKARABATI SHULE YA VIZIWI!

Mhandisi Ujenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), John Malisa (kulia) akimwelekeza fundi Umeme, Imma Maembe jinsi ya kuweka taa katika moja ya vyumba vya madarasa vya Shule ya Viziwi ya Buguruni, Dar es Salaam jana, inayokarabatiwa kwa msaada wa TBL
Fundi rangi, Bakari Yusufu akimalizia jana kupaka rangi jengo la vyumba vya madarasa katika Shule ya Viziwi Buguruni, Dar es Salaam, linalokarabatiwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Kushoto ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa.


Ajali ya ndege, kisanduku chaonekana!

Maafisa wamesema kisanduku cheusi maalum kwa kurekodi mambo yote yanayotokea hasa kwenye ajali katika ndege ya abiria iliyoanguka kwenye pwani ya Lebanon siku mbili zilizopita imeonekana.
Kikosi kilichokuwa kikifanya msako kimekikuta kisanduku hicho cha ndege ya Ethiopia takriban kilomita 1.3 chini ya maji, kilomita 10 magharibi mwa mji mkuu wa Beirut.
Maafisa wa usalama wa Lebanon wamesema kikosi hicho sasa kinajaribu kukitoa.
Watu wote 90 waliokuwemo kwenye ndege ya Ethiopia wanaaminiwa kufariki dunia kutokana na ajali hiyo.
Mpaka sasa takriban miili ya watu 24 imeopolewa katika bahari.

MATUKIO BUNGENI DODOMA WIKI HII!

Waziri wa Miundo Mbinu Dr. Shukuru Jumanne Kawambwa (kushoto) akibadlishana mawazo na Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM Zainabu Vulu (kulia) mjini Dodoma jana. ambapo Mkutano wa kumi na nane wa bunge la jamhuri ya Tanzania unaendelea.
(Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO-Dodoma)

ZAIN YAANZISHA PROMOSHENI YA "NIPE NIKUPE"

Meneja Masoko wa Zain Kelvin Twisa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski juu ya faida watakazozipata wateja wa kampuni hiyo katika ofa mpya ya Nipe Nikupe wenginer katika picha kutoka kushoto ni Group Manager Steve Torade,Managing Director Khaled Muhtadi,pamoja na Ahsan Syed.
Wateja wa Zain Tanzania nchi nzima sasa watarudishiwa papo kwa papo pesa yoyote watakayotumia kuzungumza kwenye simu zao zao mkononi kupitia ofa kabambe ya Nipe Nikupe.
Zain, kampuni inayoheshimika zaidi nchini Tanzania imethibitisha leo kwamba mteja wa Zain atarudishiwa shilingi 200 papo kwa papo kwa kila shilingi 200 atakayotumia kuzungumza kila siku. Hii inamaanisha kwamba kila shilingi 200 inayotumika kuzungumza kwenye mtandao wa Zain inakurudishia kiashi hicho hicho ili uweze kuendelea kuzungumza kwenye mtandao wa Zain.
inamrudishia teja akitumia shilingi 200 kwenye simu ya kutoka mtandao wa Zain kwenda Zain atarudishiwa kiasi hicho cha pesa ili akitumie kwenye mtandao mwingine. Ofa hii sio kwa simu zinazopigwa kutoka mtandao wa Zain kwenda Zain tu, bali hata zile zinazopigwa kutoka Zain kwenda kwenye mtandao mwingine wowote ule nchini. Kwa kila 200 utakayotumia kupiga simu kwenda kwenye mtandao mwingine, utarudishiwa kiasi hicho hicho papo papo ili uendelee kupiga simu kwenda kwenye miandao mwingine.
Ofa hii kabambe ni ya kwanza ya aina yake nchini Tanzania na inaweka historia katika sekta ya mawasiliano nchini na kudhihirisha hatua zinazochukuliwa na Zain kuongoza nchini katika kuanzisha mawasiliano ya gharama nafuu kati ya mitandao ya simu za mkononi.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Nipe Nikupe Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khaled Muhtadi alisema kuanzia leo wateja wote wa Zain walio katika mpango wa Malipo Kabla watakao jisajili katika mpango huu watarudishiwa muda wa maongezi waliotumia papo papo na wanaweza kuutumia kupiga simu za kwenda mtandao wa Zain au mtandao wowote mwingine ule nchini.

Ofa ya Nipe Nikupe itaendelea kutoa fursa kwa wateja wa Zain wanaohitaji kuwasiliana na ndugu na familia au kufanikisha mahitaji yao ya biashara nchini kote kunufaika na mtandao mpana wa Zain ulioenea maeneo mengi zaidi nchi kuliko mtandao mwingine wowote pamoja na bidhaa za ubunifu wa hali ya juu. Wateja wa Zain wataweza kutumia bonasi walizopata kupiga simu kwenda Zain au mtandao mwingine wowote siku hiyo hiyo kabla muda wa bonsai haujaisha saa sita usiku.

Kujisajili katika Nipe Nikupe mteja wa Zain anapaswa kutuma SMS ya neno NIPE mara moja tu kwenda 15444 na ujumbe huo utagharimu Tshs 500 tu ambayo itatozwa mara moja tu.

Rais Obama ahutubia Marekani!

Rais wa Marekani Barack Obama.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa katika bunge la Congress Rais wa Marekani Barack Obama amezungumzia matatizo ya kiuchumi yanayoikumba nchi hiyo.
Amekiri kuwa mpango wake wa kufufua uchumi wa Marekani haukuwapendeza baadhi ya wananchi lakini akasema hatua hiyo ilikuwa muhimu na kwamba kama haingechukuliwa ukosefu wa ajira ungeongezeka.
Amesema anaweka lengo jipya la kuimarisha soko la bidhaa za Marekani nje ya nchi.
Rais Obama pia amesisitiza nia yake ya kutekeleza mabadiliko katika sekta ya afya nchini humo.
Kuhusu sera ya kigeni,Rais Obama amezitaja silaha za nuclear kama tishio kubwa zaidi ambalo linaikabili Marekani.
Amesema kuwa juhudi za kidplomasia zinaendelea kukabiliana na tishio hilo na kuonya kuwa Iran itachukuliwa hatua iwapo itaendelea kupuuza swala la nuclear.
Rais Obama pia amezungumzia swala la kuongezwa kwa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan.

Wamjua Sporah wa Sporah Show

Anaitwa Irene Sporah Njau katikati . Akiwa kijana wa Kitanzania mjasiriamali ambaye anatangaza kipindi cha Sporah Show kinachorushwa na Ben TV huko Uingereza.Sporah ni nani? yuko wapi na anafanya nini? Ungana na Spoti na Starehe kwa kugonga hapo chini ili kujua hayo na mengineyo katika mahojiano haya. http://spotistarehe.wordpress.com/2010/01/27/sporah-wa-the-sporah-show/

International Day of Commemoration in Memory of the Victims of the Holocaust!

UN Secretary Ban Ki Moon.

27 Jan 2010, UN Information Centre (Dar es Salaam) : Today, the UN Information Centre(UNIC) organized a special learning session for primary and secondary schools in Dar es Salaam as part of observance to mark International Day of Commemoration in Memory of the Victims of the Holocaust. The theme for the Day was The legacy of survival. This day is observed by the United Nations on 27 January each year, in accordance with mandate given by the General Assembly in its resolutions 60/7 adopted on 1 November 2005. The resolution condemns all manifestations of religious intolerance, incitement, harassment or violence against persons or communities based on ethnic origin or religious belief, whenever they occur. The commemoration was held at UNIC Library and was attended by 80 students from Academic International School, Makongo High School, Tusiime Secondary School, Loyola Secondary School, Olympio Primary School, Hazina International School, Oysterbay Primary School, St Mary’s International School and St Anne Marie Primary School. The learning session which included statement from the UN Secretary General, video show of the holocaust and survivors stories and discussions, aimed to help young people understand the persecution of the Jewish people during the Holocaust and what the consequences of hatred and prejudice are today. In his message to mark the Day, The UN Secretary General, Ban Ki-moon said survivors carry a crucial message for all of us. A message about the triumph of the human spirit. A living testament that tyranny, though it may rise, will surely not prevail. Mr Ban’s message was presented by the UNIC’s Information Office, Ms Usia Nkhoma Ledama. He said Survivors also play a vital role in keeping the lessons of the Holocaust alive for future generations. “Holocaust survivors will not be with us forever – but the legacy of their survival must live on. We must preserve their stories – through memorials… through education… most of all through robust efforts to prevent genocide and other grave crimes,” The UN Secretary General added.

Athari za mazingira zinazingatiwa kabla ya ujenzi wa Hotelli ya Kitalii!!

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige.
Na Tiganya Vincent, MAELEZO, Dodoma
Serikali imesema kwamba tathmini za kimazingira zimekuwa zikifanyika kabla ya kutolewa vibali vya ujenzi wa hoteli za kitalii ambapo hatua huchukuliwa kwa ujenzi unaofanywa kinyume cha utaratibu.
Pamoja na hatua Serikali pia imeendelea kuwaelimisha wawekezaji wapya na wa zamani wa sekta ya Hoteli za kitaalii umuhimu wa kuzingatia ubora ili kuhakikisha kuwa hoteli zinazojengwa zinakuwa na ubora unakubalika ndani na nje ya nchi.
Hatua hiyo inafuatia Wizara ya Maliasili kupata vigezo vinavyoonyesha na kugawa daraja za nyota kwa Hoteli za kitalii vilivyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ilitolewa jana Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekeil Maige wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum (CCM) Cynthia Ngoye aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa katika kudhibiti wageni na wasio wageni wanaojiita kuwa wawekezaji wa hoteli za nyota kuchukua ardhi ya wananchi kando kando ya Bahari Hindi na kujenga Hoteli za gharama ndogo na kuezeka kwa makuti.
Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushauri kwa wawekezaji katika hoteli za kitalii ili kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa zinalingana na daraja lake na sio vingingevyo.
Maige alisema kuwa Wizara hiyo ufanya ukaguzi wa hoteli zilizokamilika na kuziweka katika daraja na kisha taarifa huwasilishwa katika Kituo cha Uwekezaji(TIC) ili kuhakikisha kuwa uwekezaji umefanyika kwa mujibu wa mikata ya uwekezaji.
Aidha , Naibu Waziri huyo alisema kuwa suala la uezekaji wa kutumia makuti katika hoteli huzingatia zaidi aina ya hoteli inayojengwa , pamoja na madhari ya eneo na kuongeza kuwa uwekezaji wa makuti sio nafuu kama wengi wanavyodhani na unafaida nyingi za kimazingira.
Kwa upande mwingine Naibu Waziri huyo aliliambia Bunge kuwa ni jukumu la kila Mkoa hapa nchini kuainisha maeneo ya vivutio vya utalii kwa ajili kuvitafutia wawekezaji watakaosaidia kuweka miradi itakayowavutia watalii kutoka nje nandani ya nchi kutembelea maeneo husika.

Waziri mkuu mpya aanza kazi Guinea!

Jean Marie Dore waziri mkuu mpya wa Guinea.

Waziri mkuu mpya wa muda wa Guinea, mwenye jukumu la kuandaa uchaguzi utakaomaliza utawala wa kijeshi ameanza kazi rasmi.
Jean Marie Dore aliteuliwa na kiongozi aliyepo madarakani, Sekouba Konate, baada ya serikali ya kijeshi kukubali kuachia madaraka.
Dore alitoa hotuba fupi akielezea mambo aliyokusudia kutekeleza, kurekebisha jeshi la Guinea ikiwa ni jambo alilolipa kipaumbele.
Hata hivyo, hatua hiyo si jambo rahisi kwa nchi iliyodhibitiwa na jeshi kwa miongo kadhaa.
Serikali iliyopo sasa iliingia madarakani Desemba 2008 baada ya kifo cha Lansana Conte, yeye mwenyewe akiwa mwanajeshi aliyepindua serikali miaka 24 kabla ya kifo chake.

MOHAMED RAZA AFAGILIA AZIMIO LA BUTIAMA!

Aliyewahi kuwa mshauri wa Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salmin Amour Bw. Maohamed Raza akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Satrlight jijini Dar es salaam leo wakati alipompongeza Makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume kwa kukubaliana na kuendeleza uamuzi wa azimio la Butiama lililokuwa limependekeza serikali ya pamoja visiwani Zanzibar na kamati maalum ya CCM ili kudumisha amani katika visiwa vya Zanzibar.
Raza pia amempongeza katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF kwa kumtambua Rais Karume na kwamba huo ni mwanzo mzuri wa amani visiwani Zanzibar na hii ni furaha kwa wazanzibari wote, watanzania wote na jumuiya za kimataifa.
Akizungumzia kuhusu rais Karume kuongezewa muda wa urais amesema rais karume mwenyewe amekataa na amesisitiza kuwa muda wake wa kuiongoza Zanzibar umekwisha kikatiba, hata hivyo Mohamed Raza amesema kuhusu suala la kuongeza muda au kuunda serikali ya pamoja ni suala la kikatiba ambalo linahitajika kupelekwa kwa wananchi wote ili wapate muda wa kulijadili na watakalopendekeza ndilo lifanyiwe kazi kikatiba .
Pia akawataka Wawakilishi wa baraza la wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Cahama cha Mapinduzi kuwa makini na mjadala wa suala hilo, hivyo wanatakiwa kufanya maamuzi yao huku wakijua kuwa wanaiwakilisha CCM na wanachama wa chama hicho kwa ujumla

Serikali kupeleka gari la polisi wilayani Ngara ili kukabiliana na ujambazi!

Balozi Khamis Kagasheki Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.
Na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dodoma
ILI kukabilina na kasi ya ujambazi wilayani Ngara Wizara ya Mambo ya Ndani imeahidi kupeleaka gari la polisi litakalowasiadia kupambana na wahalifu hao.
Ahadi hiyo ya Serikali imekuja kufuatia swali la mbunge wa Ngara Prof. Feetham Banyikwa (CCM), aliloliuliza bungeni mjinini Dodoma jana na kuiomba Serikali kupeleka magari ya kutosha Ngara ili kumaliza adha ya usafiri.
Mbunge huyo alisema kuwa kuwepo kwa wimbi kubwa la ujambazi katika baadhi ya kata wilayani Ngara jambo ambalo linahatarisha usalama wa raia na mali zao.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Balozi Khamis Kagasheki alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kupeleka gari katika kituo hicho na kuahidi kupeleka gari moja kabla ya mwezi April mwaka huu.
Alisema kwa sasa wilaya ya Ngara inazo pikipiki tatu na magari mawili vifaa ambavyo havitoshelezi ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wilaya kwa kuzingatia ukubwa wa wilaya husika na jiografia yake.
Balozi Kagasheki alisema jambo jingine linaloonyesha kuwepo kwa umuhimu kwa kupeleka gari katika wilaya hiyi ni kuwepo kwa tishio la kiusalama kutokana na wilaya hiyo kupakana na nchi jirani.
Alisema Serikali itaendelea kuongeza idadi ya vitendea kazi katika vituo vya polisi kwa wilaya mbalimbali nchini kulingana na upatikanaji wa fedha kwani ni nia ya Serikali kuhakikisha kuwa hakuna tatizo la usafiri katika jeshi la polisi.
Balozi Kagasheki alisisitiza kuwa licha ya kukosekana kwa vitendea kazi madhubuti kama usafiri katika wilaya ya Ngara, Polisi mkoani Kagera wataendelea kutoa msaada kwa wilaya hiyo na kutimiza majukumu yake ipasavyo wakati Serikali ikiendelea kushughulikia suala hilo.

Ashimba Live with his band at Alliance Française!


After some time touring in Europe and preparing for the new album,
Ashimba is now back at stage with his band in Dar es Salaam.
Don't miss this fantastic show with one of the most talented
singer-songwriters in Tanzania !

Ashimba with band
Thursday the 28th of January,
Doors open at 20:00
Entrance: TSH 5000