HAFLA YA UMODOTZ.BLOGSPOT.COM KUFANYIKA KESHO GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL!!

Blogu ya umodotz.blogspot.com inawakaribisha wapenzi wote wa maswala ya mitindo, urembo na mavazi kwenye onyesho la wazi siku ya Jumamosi, Tarehe 30 Januari 2010 pale Giraffe Ocean View Hotel. Hafla hiyo imeandaliwa na umodotz blog kwa udhamini wa SHEAR ILLUSIONS, TRUWORTHS na GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL.

Hafla itaanza saa 12 jioni na kuisha saa 2 usiku.

Dhumuni kuu la hafla hiyo ni kuukaribisha rasmi mwaka 2010 kibiashara. Kuwatakia kheri wateja, marafiki, na washirika wa blogu pamoja na wadhamini kwa kuonyesha bidhaa mpya na huduma zao. Onyesho ni la wazi, hakuna kiingilio.

Watakaofika wataburudishwa na onyesho kali la mavazi ambalo litafanywa na mamodo 12 wa blog ya Umodotz. Watapita kwenye mavazi ya mbunifu mzoefu KEMMI KALIKAWE wa Naledi Fashions pamoja na mbunifu chipukizi MGESI. Nguo zote zitauzwa papohapo kwa watakaozipenda. Mamodo wamepambwa kichwani na nywele za Shear Illusions kwa mitindo tofauti iliyobuniwa na wataalamu wa urembo kutoka Paradise Uni-sex Salon (www.paradisespalon.cotz)

Shear Illusions itatoa mkataba mnono na wa kihistoria kwenye medani ya mitindo Tanzania kwa mmoja kati ya mamodo 12 wa blog ya Umodo. Mkataba huo ni wa mwaka mzima! Bila shaka utampa modo fursa nyingi za kufahamika kutokana na picha katika jarida la Shear na bango za matangazo.

Mkataba utaenda kwa msichana ambaye ataonyesha ana uwezo mkubwa wa kuwa modo wa kipekee siku hiyo.

Hili sio shindano. Mamodo 12 wa Umodo walipatikana kwa mchakato wa muda mrefu wa kuwachujwa na kuchaguliwa mmoja mmoja hadi kufikia 12.

Blog ya Umodo ilipata ushauri wa watu mbalimbali kama Steven Kanumba(filamu), Slyvia Shao(Urembo) na mbunifu Kemmi Kalikawe (mitindo) ambao wanawakilisha nyanja mbalimbali zinazoshabiiana na maswala ya mitindo.

Umodotz.blogspot.com inawakaribisha wote. Tunatumaini kuwaona mamodo wengi, wabunifu tele, wapenda mitindo, urembo na mavazi, watu maarufu katika nyanja mbalimbali, wafanya biashara, viongozi, watangazaji, waandishi, vijana na watu wazima. Hii ni nafasi nzuri kufahamiana katika jitihada za kukuza fani ya Mitindo Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment