M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 11 (Thursday July 29, 2010)

It’s day 11 on M-Net’s Big Brother All Stars --- and Big Brother housemates took on the ‘Horror Island’ task! The 14 All Stars had to negotiate a bowl of cockroaches, a diabolical cocktail, buzzing flies, wax tattoos, and a Golden Snake challenge! Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Pictured here: Sammi and Mwisho

FIESTA JIPANGUSE 2010 ILIVYOFANA MJINI MUSOMA !!

Farid Kubanda a.k.a Ngosha akishusha mistari ya nguvu mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 lililofanyika Musoma Hotel juzi ,ambapo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya Bia ya Serengeti.
(Picha kwa hisani ya Michuzijunior wa Jiachie).

Wasanii Chege na Mh Temba wote kutoka kundi la Wanaume TMK wakikamua jukwaani,huku washabiki wao wakiweka mikono juu kuashiria kukunwa vyema na nyimbo zao.

Mmechisho safi kabisa wa Mfalme wa raha kamili

Mdau akiwa amepozi Wafamle wa raha kamili





Corporate Golf day 2010.


Rais karume alipopiga kura ya maoni zanzibar jana!!

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid
Karume,akitumbukiza kura yake,katika kituo cha kupigia kura ya Maoni, ya kuwezesha Uundwaji Serikali ya Kitaifa ya Zanzibar,katika Skuli ya Msingi ya Kiembesamaki Wilaya Magharibi jana,Uundwaji wa Serikali hiyo ya Kitaifa ni baada ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Octoba mwaka 2010.

MABALOZI WA MALARIA WATOA MSAADA WA VYANDARUA KWA WAJAWAZITO MWANZA!!

Mtangazaji wa Clouds FM B dozen kwa niaba ya wasanii wenzake akizungumza machache mbele ya Wazazi ndani ya wodi ya wazazi ndani ya hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure mara baada ya kuwakabidhi vyandarua leo jioni ,yote hiyo ikiwa ni kwenye mpango mzima wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa malaria iliyozinduliwa hivi karibuni ya ZINDUKA.

Shoto ni B Dozen,Young D,Rebeca kutoka kituo cha THT,Mwasiti pamoja na waja wazito katika picha ya pamoja jioni hii,mara baada ya kuwakabidhi Vyandarua vya msaada kupitia mpango mzima wa kampeni ya kupambana na malaria nchini wa ZINDUKA.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao wapo kwenye ziara ya tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,ambao pia ni mabalozi wa Malaria hapa nchini,Mwasiti pamoja na Chege wakiwakabidhi Vyandarua Muuguzi mkuu (kushoto) Bi.Eva Mudayi pamoja na afisa muuguzi wa wodi hiyo Bi Adelina jioni hii,yote hiyo ikiwa ni kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria kupitia mpango wa ZINDUKA.

Mtangazaji wa Clouds FM Hamis Mand a.k.a B Dozen akiwakabidhi Vyandarua Muuguzi mkuu (kushoto) Bi.Eva Mudayi pamoja na afisa muuguzi wa wodi hiyo Bi Adelina jioni hii,yote hiyo ikiwa ni kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria kupitia mpango wa ZINDUKA.

Mabalozi wa Malaria nchini wakiwa wamepozi picha ya pamoja na waja wazito jioni hii mara baada ya kuwakabidhi Vyandarua vya msaada kupitia mpango mzima wa kampeni ya kupambana na malaria nchini wa ZINDUKA.

BASI LA NAJMUNISA LAPATA AJALI NA KUSABABISHA VIFO KADHAA!!

Ajali ya Kanegele - Fuso na Super Najimunisa Kahama Mkoani Shinyanga jana kama unavyoona picha mbalimbali zilizochukuliwa eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo inayodaiwa kusababisha vifo vya watu 18 . Cha ajabu ajali imetokea mita 10 kutoka katika kizuizi cha askari wa maliasili wanaokagua mazao ya maliasili.
Katika ajali hiyo inasemekana askari aliyekuwa akisindikiza basi hilo alikatwa kicha baada ya fuso kuharibiwa vibaya na basi. hebu Jionee mwenyewe picha zilizopigwa katikaajali eneo la tukio huko Kanegele kama inavyoonekana Sura ya Basi la Super Najimunisa baada ya Ajali.(Picha na Bernard Kinte wa mtandao wa Wanabidii)
Waokoaji wakitafuta maiti ndani ya Fuso.

Eneo la ajali-Kwenye kizuizi cha Kanegele.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia ajali hiyo wakichungulia Maiti zilizopakjiwa ndani ya magari aina ya Toyota Landcruiser hardtop.

Askari wa usalama Barabarani katika eneo la ajali.

HAKIKA UKIONA FILAMU HII HUTOAMINI KAMA NI MIMI NIMECHEZA..... NI CRAZY LOVE (KANUMBA)

Filamu hii hata mimi mwenyewe japo nimecheza lakini naipenda sana na naisubiri kwa hamu,ni moja kati ya filamu ngumu nilizowahi kucheza na nikamudu sawia nafasi yangu, Filamu hii itakuwa mtaani mwezi ujao (wa nane) ili kunifanya nimudu vyema na kuuvaa uhusika wangu ilinichukua mwezi mzima kusoma vitabu mbalimbali vya wasomi na watu mashuhuri duniani kama vile PLATO, KARL MAX, ALEXANDER THE GREAT, SAMUEL TAYLOR nk, lakini pia Ilinibidi kuwa karibu sana na waalimu kadhaa wa vyuo vikuu ili kujua tabia zao. ili kuiweka sawa kabla ya kucheza filamu hiyo.
TAFADHALI FILAMU HII SI YA KUKOSA,PATA NAKALA YAKO ORIGINO,, FILAMU HII IKITOKA NAOMBA MNIAMBIE KWA KUNITUMIA E MAIL MBALI ILI KUNIPA MAONI KAMA MUIGIZAJI WA BONGO AMBAYE NIMEWEZA KUCHEZA UHUSIKA HUO?NINA UHAKIKA MAONI YENU YATAKUWA CHANGAMOTO KWANGU KATIKA KUCHEZA FILAMU NYINGINE NGUMU NA NZURI ZAIDI YA HII. Hapa akionekana katika taswira nyingine ya Crazy Love.
Hapa Steven Kanumba akijipa raha huko Zanzibar hivi karibuni.

Hapa ni kivazi cha jioni, akiwa amejipigilia suruali yake ya kiaina fulani kama wenzetu kutoka kule bara la Asia.

TIMU YA TAIFA YA MISRI KUIPA SOMO TAIFA STARS!!

Timu ya taifa ya wanaume Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Misri Augasti 11 mwaka huu nchini Misri ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na michezo ya kutafuta tiketi ya kushiriki fainali za kombe la DUNIA nchini BRAZIL.

Msemaji wa TFF FLORIAN KAIJAGE amesema katika harakati za kutafuta timu wamefanikiwa kupata timu ya Misri.

Mchezo huo unatambulika na FIFA kwani siku hiyo ya mchezo ni siku iliyopangwa na FIFA kwa ajili ya mechi za kirafiki za FIFA.

Wakati stars ikijiandaa na mchezo huo tayari kocha wa timu ya stars JAN PAULSEN anatarajia kuwasili jumamosi usiku kuja kukinoa kikosi cha Taifa Stars. Habari na

M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 11 (Thursday July 29, 2010)

It’s day 11 on M-Net’s Big Brother All Stars --- and Big Brother housemates took on the ‘Horror Island’ task! The 14 All Stars had to negotiate a bowl of cockroaches, a diabolical cocktail, buzzing flies, wax tattoos, and a Golden Snake challenge! Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Pictured here: Mwisho

M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 11 (Thursday July 29, 2010)

It’s day 11 on M-Net’s Big Brother All Stars --- and Big Brother housemates took on the ‘Horror Island’ task! The 14 All Stars had to negotiate a bowl of cockroaches, a diabolical cocktail, buzzing flies, wax tattoos, and a Golden Snake challenge! Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Pictured here: Paloma and Tatiana.

RAIS JAKAYA NA ASKOFU WA KKKT MOROGORO NA WAZEE WALIOPIGANA VITA MKUU YA PILI YA DUNIA!!

Rais Jakaya Kikwete Akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee waliopingana vita vikuu vya pili vya Dunia. Rais Kikwete aliwaalika wazee hao Ikulu jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo nao, Wa kwanza kushoto ni Katibu mkuu wa wizara ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Bw, Andrew Nyumao wa tatu kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa Dar es salaam Mh,Said Meck Sadick Ikulu 30.7.2010 PICHA NA JUMA KENGELE
Mkazi wa Sokoine Morogoro. Justine Shamba Kubwa akipongezwa na Rais Jakaya Kikwete Baada ya kuchangia shilingi Laki Mbili taslimu (200,000) wakati wa Harmbee ya Ujenzi wa shule ya sekondari ya Ebenezeri Lutheran Junior Seminary High school iliyopo Morogoro. Kulia ni Askofu Jacob Mameo Ole Paulo wa Dayosisi ya KKKT ya Morogoro aliyesima kulia kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa Morogoro Kanali mstaafu Issa Machibya

Rais Jakaya Kikwete Akipokea Zawadi ya Kinyago kutoka kwa Askofu Jacob Mameo Ole Paulo wa KKKT Dayosisi ya Morogoro wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Sekondari ya Ebenezeri Lutheran Junior Seminary High School ya Morogoro

CD "Jakaya Kikwete 2010" kutoka kwao "Ngoma Africa Band" yatua nchini!!


Hayawi !Hayawi ! Sasa yamekuwa ile CD inayozungumziwa na washabiki wengi kila kona duniani Sasa imeshatua nchini .




CD hiyo yenye jina "JAKAYA KIKWETE 2010" Kutoka kwao "The Ngoma Africa Band" bendi yenye maskani yake huko Ujerumani, Sasa unaweza kupata kopi za CD hiyo kwa ANKAL Muhidin Issa Michuzi aka Mzee wa Libeneke, kwa simu 0754271266 wa blogu ya jamii.




Pia kwa yeyote yule anayetaka atumiwe mp 3 au kuweka nyimbo hizo katika mlio wa Simu za viganjani tafadhali usisite kuwasiliana na Ankal Michuzi kwa simu namba 0754271266 CD hiyo yenye muziki mtamu unaosindikiza ujumbe muhimu kwa watanzania zaidi ya milioni 40.




Hivi sasa CD hiyo ipo nchini na unaweza kupata kopi yake na kuitumia katika sherehe ,mitaani,katika biashara yako,ndani ya mabasi,harusini,sokoni n.k, ili upate raha na ujumbe uliomo katika CD "Jakaya Kikwete 2010" utunzi wake Ebrahim Makunja a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU wa Ngoma Africa Band.




Pia Jumamosi ya 31-07-2010 saa 4 asubui Ras Makunja atahojiwa na radio Free Africa ya Mwanza tafadhali tega sikio.

Emirates Cup live on SuperSport

SuperSport, available on DStv, has acquired the rights to broadcast this weekend’s popular Emirates Cup tournament from London.TV details (all times CAT): Saturday 31 July 20103pm (SS3, Maximo): Celtic vs Lyon (live)5.15pm (SS3, Maximo): Arsenal vs AC Milan (live) Sunday 01 August 20105.15pm (SS3, Maximo): Arsenal vs Celtic (live)11pm (SS3, Maximo): AC Milan vs Lyon (delayed)

MWAKA HUU VIJANA WAMEVAMIA BUNGENI, NI KAZI KWELI KWELI!!


Na Hillary Shoo,Singida.


KATIBU wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya (UNA) United Nation Asociation iliyopo kwenye jengo la umoja wa mataifa jijini Dare s salaam Fancy Nkuhi (25) amechaguliwa kuwa mmoja wa wagombe Ubunge kundi la vijana kutoka mkoani Singida.


Fancy aliibuka kidedea kwa kupata kura 16 kati ya kura 29 zilizopigwa jana na wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoani hapa.Katika uchaguzi huo mshindi alipata upinzani mkali kutoka kwa msindi wa pili Jamila Hasan aliyepata kura 10 huku Vailet Eliasi ambaye ni mfanyakazi wa ofisi ya UVCCM makao makuu akiambulia kura 3.



Mjasiriamali kutoka Kinondoni Mosi Ntandu aliambulia patupu baada ya kupata kura sifuri.Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo Fancy mwenye shahada ya sheria kutoka chuo kikuu huria,alisema matarajio yake ni kuhakikisha fursa wanazopata vijana katika nyanja mbalimbali zinafanikiwa.



Alisema atahakikisha kuwa fursa hizo zinapata msimamizi mwenye uwezo wa kuzitetea katika bunge pindi atakapochaguliwa kushika nafasi hiyo.Hata hivyo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Pascal Mabiti aliwataka vijana hao kuunganisha nguvu ya pamoja na kuvunja makundi ili kuhakikisha mwakilishi huyo kutoka mkoani hapa anaibuka mshindi katika awamu ya pili Mkoani dodoma Agosti 3 mwaka huu.

The French Government has provide 14 scholarship to Tanzanian!


Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam


The French Government has provide 14 scholarship to various Tanzanian teachers to undergo in France a one month course on French language and training programme of French as a Foreign language.


The scholarship under a French project on Assistance in teaching of French in Tanzania has been allotted to teachers from Secondary School, University of Dar es Salaam and from the college o Business Education.


According to the French Embassy Communication Officer Joseph Kithama, other educationists to have been awarded a scholarship are inspectors of Primary and Secondary School and Curriculum planes from Tanzania Institute of Education (TEI).


Since 2008, Ministry of Education and Vocational Training in collaboration with the French Government is implementing a comprehensive action plan to enhance the teaching and learning of French in Tanzania. The French government is committed to assist education and wasters sectors in Tanzania through specific interventions agreed under a bilateral agreement between the two countries. French Ambassador to Tanzania Hon.


Jacques Champagne de Labriolle is scheduled to host a brief reception on July 30th, 2010 to departing Tanzanian educationist.”Bon Voyage”. In November 2009, a batch of 23 Tanzanians teachers went to France for a similar course, aimed at improving their level of French and their capacity to teach the language.

TAMASHA LA SAUTI YA KISWAHILI KURINDIMA JIJINI AGOSTI 4-6!!

Khadija Jilala Mhadhiri Chuo Kikuu Huria na wa Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti ya Kiswahili akiongea na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo wakati alipokuwa akitangaza tarehe ya kuanza kwa tamasha hilo litakaloanza Agosti 4-6 mwaka huu na kufanyika katika hoteli ya Giraffe Ocean View Hotel Mbezi pamoja na makumbusho Village jijini Dar es salaam.
Katika tamasha hilo kutatolewa tuzo ya Mama Salma Kikwete kwa washindi ambapo pia mke huyo wa rais Atakuwa Mgeni rasmi ili kufanikisha tamasha hilo, katika picha kushoto ni Yusta Daniel Nyakachala Mkurugenzi wa Art In Tanzania na kulia ni Halima Kinungu Mhadhiri Chuo Kikuu Huria kitivo cha Sayansi na Jamii

HAYA NDIYO MAMBO YA DR. WILBROD SLAA LEO JIONI JIJINI ARUSHA!!

Mgombea wa urais wa Jamhuri wa Muungano kupitia Chama cha Deomkrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, akiwahutubia maelefu ya wakazi wa mji wa Arusha, ambao walijitokeza kumdhamini, katika Uwanja wa NMC leo. Picha kwa hisani ya Joseph Senga.

SIMBA YAMNASA TENA KOCHA MSERBIA MILOVAN CURKORVIC!!

Afisa Uatwala wa Klabu ya Simba Evodias Mtawala akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo leo wakati alipotangaza mkataba mpya na kocha Milovan Curkovic wa Serbia kushoto ni Cliford Ndimbo Msemaji wa klabu hiyo.

Timu ya Simba leo imetangaza kuingia mkataba mpya wa miaka miwili na kocha Mserbia Milovan Curkovic ambaye atawasili wakati wowote kuanzia sasa ili kuja kuinoa timu hiyo, awali kocha huyo aliwahi kuja nchini na kufundisha timu ya Simba kabla ya kurudi kwao Serbia kutokana na kutoelewana katika baadhi ya vipengele kwenye mkataba wake wa awali


Simba imetangaza azma hiyo baada ya kusumbuliwa mara kwa mara na kocha wao Mzambia Patrick Phiri ambaye amekuwa msumbufu kwa muda mrefu mara inapotokea anakwenda lilikizo kwao Zambia, hivyo vitendo vya kocha huyo kupelekea kuwachosha wanasimba, jambo lililofanya uongozi kufikia uamuzi wa kutafuta kocha mwingine.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi Afisa Utawala na Kaimu Katibu mkuu wa klabu hiyo Evodias Mtawala, amesema hata hivyo kabla ya yote wamemtumia barua ya kumtaka kujiuzuru Kocha Patrick Phiri kutokana na kukiuka makubaliano na klabu hiyo hivyo kuifanya klabu hiyo kuhangaika katika suala zima la mwalimu.


Wakati huohuo Mtawala amesema Simba inatarajia kufanya tamasha lake la Simba Day Agosti 8 mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru ambapo timu za Express ya Uganda zimealikwa pamoja na timu ya Azam FC ya jijini, wakati Express ikicheza na Simba siku hiyo Azam itacheza na Simba B katika mchezo mwingine katika kufanikisha tamasha hilo.




ASHA ROSE MIGIRO ATEMBELEA TUME YA HAKI ZA BINADAMU.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Asha Rose Migiro (kulia) na kushoto ni Kamishina Mstaafu wa Haki za Binadamu Mhe. Jaji Amir Manento akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Haki za binadamu na Waandishi wa Habari ,ambao hawapo kwenye picha alipotembelea Tume hiyo mjini Dar es Salaam leo.
(PICHA NA ANNA ITENDA -MAELEZO)

M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 9 (Tuesday July 27, 2010)

It’s day 9 on M-Net’s BIG BROTHER ALL stars --- and with last week’s surprise fake eviction behind them, plus the news from Big Brother of a deduction from the prize money due to a violation of the rules of the game, the housemates must now be contemplating alliances, strategy and weeks ahead. The game looks set to become more strategic…with the threat of nominations and evictions always present. And the housemates must also be wondering…what other surprises Big Brother has in store? Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother.

Kapumzike kwa amani mpiganaji mwenzetu Primtiva Pancars.!

Mume wa Marehemu Primtiva Pancras ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa kampuni ya New Habari Cooparation 2006 Bw. Joachim Mushi akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya mke wake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam,
Marehemu Primtiva alifariki juzi mkatika Hospitali ya Lugalo baada ya kuugua ghafla na kupoteza uhai wake,Marehemu atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuandika habari na makala zenye mguso kwa jamii hivyo kujipatia heshima kubwa kwa wasomaji wake ingawa alikuwa bado mchanga kwa kiasi fulani katika fani hii ya uandishi.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Primtiva Pancars AMEN.


Waombolezaji wakibeba Jeneza lililowekwa mwili wa Marehemu Primtiva Pancras tayari kwa mazishi katika makaburi ya Kionodoni leo.

Bw. Joachim Mushi ambaye ni Mhariri wa makala wa Gazeti la Jambo Leo akiuaga mwili wa marehemu mke wake Primtiva Pancras kwa majonzi makubwa wakati wa ibada ya kuaga mwili huo iliyofanyika kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni jijini Dar es salaam.
Hawa ni wakurugezni wa Gazeti la Jambo leo kulia ni Juma Pinto na kushoto ni Benny Kisaka wakishiriki katika ibada ya mazishi ya Mwandishi Primtiva Pancras, Marehemu Primtiva alikuwa ni mke wa Mwandishi wa habari na Mhariri wa makala wa Gazeti la Jambo leo Joachim Mushi.
Mpiganaji John Badi kutoka gazeti la This Day naye ameshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Primtiva, ni kweli Primtiva alikuwa mtu wa watu.

Mpiga picha wa New Habari Cooparation 2006 Anthony Siame pamoja na muombolezaji mwingine wakimsaidia mmoja wa waombolezaji aliyeshindwa kujizuia mara baada ya kuona mwili wa marehemu Primtiva Pancras na kupoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni leo.

Mdau Jerry Muro mbele kulia na mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima Absalom Kibanda nyuma pamoja na waombolezaji wengine wakiwa aktika ibada hiyo ya mazishi leo.
Mwanahabari Robert Komba ambaye ni mfanyakazi wa New Habari Cooparation 2006 kama mhariri wa Mtanzania Jumapili akiwapa pole wafanyakazi wenzie kushoto ni Mwandishi Siddy Mgumia na Mwanaharusi Pongwa ambaye pia ni mfanayakazi wa kampuni hiyo katika kitengo cha matangazo baada ya kuondokewa na kipenzi chao, mfanyakazi mwenzao Primtiva Pancras.
Ulikuwa ni wakati wa majonzi kwa ndugu na jamaa wa marehemu Primtiva Pancras wakati wa ibada ya kuaga mwili leo.
Waombolezaji na waandishi mbalimbali wakishiriki katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu Primtiva Pancras kwenye kanisa Katoliki la Hananasifu Kinondoni.

Rais amteua Balozi Malambugi kuwa Balozi Mpya nchini Brazil!!


Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Balozi Francis Malambugi kuwa Balozi wa Tanzania Brasilia nchini Brazil .


Uteuzi wa Balozi Malambugi umefuatia kutokana na aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Balozi Daktari Joram Mkama Biswaro kuteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika.


Balozi Malambugi ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria na Mwanadiplomasia alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 1/1/1978 kama Wakili wa Serikali na amewahi kufanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Angola, Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Geneva, Ujerumani,Ethiopia na Ubelgiji.

Jaji Eliamani Mbise afariki dunia

Kumradhi wasomaji wetu tumeondoa picha tuliyoichapisha katika habari hii kwa kuwa tuliiweka kimakosa kwani picha hiyo siyo ya marehemu Eliamani Mbise tunaomba radhi kwa usubufu wote alioupata mhusika katika picha hiyo lengo letu lilikuwa ni zuri katika kupasha habari makosa ya kiutendaji yalifanyika.
Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Eliamani Mbise amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa. Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Msajili wa Mahakama ya Rufani Francis Mutungi imesema Jaji Mbise imesema Jaji Mbise amefariki majira ya saa nne na nusu tarehe 29/7/2010 .


Taarifa hiyo imesemakuwa taratibu za mipango ya Mazishi ambayo yatafanyika Arusha itatolewa baadae baada ya utawala kuwasiliana na ndugu wa marehemu.




Aidha Bwana Mutungi amesema msiba umewekwa kwa muda nyumbani alipokuwa akiishi marehemu Mikocheni kwenye nyumba za viongozi wa Serikali.


Marehemu Mbise alikuwa akifanya kazi katika kituo cha kazi cha Mahakama kuu ya Tanzania .

WAFANYAKAZI WIZARA YA HABARI WAKUTANA.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Seith Kamuhanda (wa pili kutoka kulia mstari wa kwanza) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 7 wa Baraza hilo leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine Bw. Seith Kamuhanda ametoa wito kwa watumishi wa umma kuepuka ubaguzi na upendeleo katika utoaji wa huduma.

Baadhi ya wajumbe wakichangia agenda mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.