TAMASHA LA SAUTI YA KISWAHILI KURINDIMA JIJINI AGOSTI 4-6!!

Khadija Jilala Mhadhiri Chuo Kikuu Huria na wa Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti ya Kiswahili akiongea na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo wakati alipokuwa akitangaza tarehe ya kuanza kwa tamasha hilo litakaloanza Agosti 4-6 mwaka huu na kufanyika katika hoteli ya Giraffe Ocean View Hotel Mbezi pamoja na makumbusho Village jijini Dar es salaam.
Katika tamasha hilo kutatolewa tuzo ya Mama Salma Kikwete kwa washindi ambapo pia mke huyo wa rais Atakuwa Mgeni rasmi ili kufanikisha tamasha hilo, katika picha kushoto ni Yusta Daniel Nyakachala Mkurugenzi wa Art In Tanzania na kulia ni Halima Kinungu Mhadhiri Chuo Kikuu Huria kitivo cha Sayansi na Jamii

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment