HAWA NDIYO TMK UNITY WA KWELI, WAMWAGA NYARAKA HADHARANI!!

Hili ndiyo kundi halisia la TMK UNITY likiwa katika picha ya pamoja kuanzia kulia ni Issa Mussa, Hassan Mashaka, Nyembo Ayubu na Abdalla Rashid aliyechuchumaa, kwa habari zaidi shuka chini upate ukweli wa mambo mdau.
TMK UNITY katika pozi la mauzo si mchezo wadau

Kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Unity lenye makazi yake Wilayani Temeke limesema halitakubali mtu mwingine au kikundi chochote kitumie jina lao hilo kwani wao ndiyo wenye jina halisi na wana haki nalo kisheria.
Akizungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE meneja wa kundi hilo Bw. Ashraf Mosha amesema wao kama kundi wakati walipokuwa wakianzisha kundi lao miaka kadhaa iliyopita walijua kwamba watu wanakawaida ya kuchukua majina ya wenzao ili kufaidika kibiashara hivyo walifuata taratibu zote na wakasajiri BASATA, BRELLA na COSOTA kwa hiyo wana haki zote za kutumia jina la TMK UNITY kisheria na yeyote atakayejaribu kulitumia jina hilo ana makosa kisheria ni wizi .
Hivi karibuni wasanii wawili waliokuwa katika kundi la TMK wanaume Family Y. Dash na Y. P walitangaza katika mkutano na wanahabari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo kwamba wamejitoa katika kundi hilo na kuazisha kundi lao linaloitwa TMK UNITY kitendo ambacho kiliamsha hasira kwa wasanii wenye jina halisi la TMK UNITY na kuchukua hatua ya kwenda katika vyombo vya habari ili kuweka wazi nyaraka mbalimbali zinazowapa uhalali wa kutumia jina hilo.
Meneja huyo amewaonyesha wakuda wa FULLSHANGWE nyaraka mbalimbali zikiwemo za BASATA, BRELLA na COSOTA kitu ambacho kiliwafanya wakuda hao wa FULLSHANGWE kufunga safari mpaka COSOTA ili kujua imechukua hatua gani juu ya sakata hilo lakini waliambulia patupu baada ya kuambiwa na mmoja wa wafanyakazi wa ofisini hapo kuwa maafisa wote ambao wangetoa majibu sahihi wako nje ya ofisi kikazi.
Kundi hilo linaundwa na wanamuziki kamaIssa Mussa Sir G., Hassan Mashaka BMC, Nyembo Ayubu UB,Abdalla Rashid NEM na meneja wao Ashraf Mosha na wana Albam moja inayoitwa Haitoshi yenye nyimbo 9 ambazo ni Haitoshi yenyewe, Usione Soo, Napendwa, Kaburi la Dunia, Futi Sita, Kwenye Tv, Tulia, Paulina na Dira na tayari wana video moja inayochezwa katika vituo mbalimbali vya Redio inayoitwa Haitoshi na wana mpango wa kuingiza sokoni albam yao hivi karibuni kaeni mkao wa kula wadau

MEWATA NA JERRY MURRO WATUNUKIWA TUZO YA LEADERSHIP EXCELLENCY AWARD!!

Mkurugenzi wa The Leadership Forum Hebron Mwakagenda akizungumza na wanahabari wakati alipokuwa akitangaza shirika lake kutoa tuzo maalum ya Leadership Excellency Awrd kwa MEWATA na Mwandishi Jerri Muro ambao wametunukiwa Tuzo hiyo kutokana na uwajibikaji wao kwa jamii katika kupambana na saratani ya akina mama kwa upande wa MEWATA na mapambano dhidi ya Rushwa kwa upande wa Jerry Muro kupitia kipindi chake maalum kiitwacho Ripoti Maalum hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kushoto ni Seif Nakuchima meneja mipango wa The Leadership Forum.
Mkurugenzi wa shirika la The Leadership Forum Hebron Mwakagenda aliyesimama kulia akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliopewa tuzo maalum ya Leadership Excellency Award na shirika hilo kwa uwajibikaji katika jamii ambapo mwaka huu wamepewa MEWATA na mwandishi wa habari kutoka ITV wanaofuatia ni Mary Charles mweka hazina wa MEWATA Jerri Muro wa ITV Serafina Mtuwa mjumbe wa kamati kuu ya MEWATA na Seif Nakuchina meneja wa mipango The Leadership Forum .

"NO RETREAT, NO SURRENDER" MH. LUCAS SELELII (MB NZEGA)

Mbunge wa Nzega Mh. Lucas Selelii akisisitiza jambo wakati alipoongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuzungumzia juu ya anaodai kuwa mafisadi wenye lengo la kumchafua kutokana na mapambano yake dhidi ya watu ambao amedai ni warafi wanaokula bila kusaza pia mbunge huyo ametoa siku saba kwa Gazeti la kila siku la Mwananchi kumuomba ladhi kutokana na habari ambazo zimedaiwa na mbunge huyo kuwa zilichapishwa katika gazeti hilo zikidai amejihusisha na kuingiza mambo ya udini katika moja ya mikutano yake aliyowahi kufanya jimboni kwake hivi karibuni Mh. Selelii ametangaza kuendelea na mapambano dhidi ya mafisadi mpaka kieleweke, kushoto ni Bw. Tiganya afisa kutoka Maelezo .

FULLSHANGWE INAWAPA HONGERA SANA!!

Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Hongereni kwa kutimiza miaka 20 ya ndoa yenu FULLSHANGWE tunawapa pongezi na mungu awabariki sana katika maisha yenu.

Zain Afrika Challenge yaanza!!


Meneja Masoko (Kitengo cha Wateja), Ellen Lupilli (kushoto) akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza
kuanza kwa mchuano wa kitaaluma unaoshirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu
Afrika wa Zain Afrika Challenge. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Zain
Tanzania, Beatrice Mallya.

JAFARAI AWAMWAGIA MASHABIKI WAKE "WALI NAZI"!!

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Jafarai amesema tayariamekamilisha Albam yake mpya inayokwenda kwa jina la Wali Nazi ambayo itakuwa na nyimbo 9 Jafarai amezitaja nyimbo zilizomo kwenye albam yake hoyo mpya kuwa ni Wali Nazi yenyewe, Msijisahau, Jafarai, Saa Nyingine, Unapenda, na Ye na Mimi, amesema kuwa nyimbo zote zimerekodiwa katika studio za Fish Crub za hapa jijini huku akiwa amewashirikisha wanamuziki Naazizi kutoka Kenya, Lamaa ambaye pia ni Producer wa albam hiyo na Wateule, albam hiyo itakuwa sokoni wakati wowote kuanzia sasa na itapatikana kote nchini.

Vodacom Regatta 2009 yafana

Washiriki wa mashindano ya mashua ya Vodacom Regatta 2009 wakishindana katika bahari ya Hindi mwishoni mwa wiki,Mashindano hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.



MWANAUME MKALI ZAIDI BONGO 2009 AMEPATIKANA HAPA!!

Mpambano wa kumtafuta mwanaume mkali zaidi Bongo 009 ‘The mosthandsome man Tanzania" ulifanyika juzi katika Hoteli ya New Africa katikati ya Jiji la Dar es Salaam ambapo kijana Khalid Mohamed amliibuka kidedea kati ya vijana 11 waliokuwa wakichuana. Kwa maana hiyo jamaa atakamata Dola 1000 na kufanyiwa Shoping katika maduka ya Zizzou Fashion. Shindano hilo liliandaliwa na Angels Entertainment na kudhaminiwa na British Council, C2C Television ‘Mtukwao’, I&R Identity, Ijumba Enterprises, Wapi na Michuzi Blog. NA HIVINDIVYO WANAUME WA SHOKA WALIVYOCHUANA:










KISUMA BAR NDIYO WACHOMAJI BORA WA (NYAMACHOMA) 2009 TZ!!

Mwakilishi wa Kisuma bar akipokea zawadi ya shilingi milioni 1 kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar es alaam Abbas Kandoro baada ya baa hiyo kuibuka kidedea katika uchomaji wa nyama. kulia ni Maneno mbegu meneja uhusiano wa kampuni ya bia TBL na kati ni Fimbo Butala meneja wa kilaji cha Safari Lager kilichodhamini shindano hilo.
Msndo bandi wakitoa burudani katika fainali hizo zilizoshirikisha baa tano ambazo ni Madrid Pub, Kisuma Bar, Africentre, Nguruko Bar na Titanic Bar Kisuma baa walishinda katika shindano hilo na kijinyakulia shilingi milioni 1 taslimu.

Majaji mwa shindano hilo wakionja nyama kutoka kwa mabanda matano yaliyoingia katika fainali kutoka kulia ni Doglas Sakibu, Clement Talawa na Lawrent Salvi.

Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam Abbas Kandoro katikati aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali za nyama choma 2009 katika viwanja vya Leaders jana akipata maelezo ya shindano hilo kutoka kwa meneja uhusiano wa TBL Maneno Mbegu kushoto ni Meneja wa kilaji cha Safari Lager Fimbo Butala.




FULLSHANGWE INAKUMUVUZISHIA MATUKIO YA USIKU WA NCHINGA SOUND MDAU, HEBU PATA VITU!

Wanengaji hawa walitisha sana wakati wakiwa na bendi hii kulia ni Amina Rusha Roho na Queen Vero wakiongoza mashambulizi jukwaani huku Rogat Hega na Muumini Mwinjuma wakichombeza kwa taratiibu kwa nyuma katika onyesho la usiku wa Nchinga lililofanyika kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza usiku wa kuamkia leo onyesho hilo lilikutanisha wanamuziki wote waliowahi kupiga muziki na bendi ya Nchinga Sound na lilikuwa maalum kwa kumpa pole aliyekuwa mlezi wa bendi hiyo
Mh. Mudhihir M. Mudhihir kutokana na kupoteza mkono wake mmoja katika ajali ya gari iliyotokea miaka kadhaa iliyopita jimboni kwake wakati akiwa katika shughuli za kijamii, onyesho lilikuwa zuri na la kuvutia na watu wengi walitamani bendi hiyo iendelee kufanya maonyesho mengine, Tovuti FULLSHANGWE pia inampa pole Mh. Mudhihir Mudhihir lakini pia inawapongeza wanamuziki hao kwa kukubaliana na kufanya onyesho hilo maana limetukumbusha mbali sana, kwa matukio mbalimbali ya onyesho hilo shuka chini ili upate uhondo zaidi mdau.
He! naye mamaa Maimartha mwana wa Jesse kutoka televisheni ya Afrika Mashariki EATV akafanya mambo makubwa ili kuweka kumbukumbu ya usiku huo wa Nchinga kama unavyomuona katika picha akiwa ameshika kinasa sauti akijiandaa kuongea na watu mbalimbali ukumbini hapo ili kuelezea hisia zao juu ya usiku wa Nchinga uliofanyika kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza usiku wa kuamkia leo.

hapa alikuwa hakamatiki mtu kwa shangwe mdau kila mtu alijipa raha vyakutosha.
Ilikuwa si haba manake watu walipata burudani walioitarajia kutoka kwa vijana hao wa Mh. Mudhihir M. Mudhihir enzi hizo.

Vimwana hawa wakaselebuka vyakutosha kwa shangwe za usiku wa nchinga.

Hapa kama kawaida yake Muumini Mwinjuma ameshawapandisha mzuka mashabiki wa bendi hiyo yaani nilitamani iendelee kufanya maonyesho kila wiki mdau.

Prince Muumini Mwinjuma akipandisha mzuka wa mpiga kinanda Deo Mwanambilimbi.


Kikosi cha Nchinga Sound kikianzisha mashambulizi kikiongozwa na Prince Muumin Mwinjuma, kwakweli lilikuwa ni bonge la onyesho kwa maana kwamba Nchinga ile ya zamani ilirudi kwa nguvu na kasi mpya.
Dada yake na Mbunge wa Nchinga Mh. Mudhihir M. Mudhihir Zuhura M. Mudhihir akitoa shukurani zake kwa waliokuwa wanamuziki wa Nchinga Sound kwa kumuenzi kaka yake kutokana na mchango aliokuwa akiutoa katika bendi hiyo Zuhura alimuwakilisha Mh Mudhihir ambaye hakuwepo kwenye onyesho hilo kutokana na sababu za kiafya.

Mkurugenzi wa TOT Plus John Komba kulia akiteta jambo na mwanamuziki mwalikwa wa Kalunde Band Kasaloo Kyanga kushoto ni mpiganaji Ojuku Abraham.
Wana Kalunde wakishambulia jukwaa kuanzia kulia ni Queen Vero, Junior, Rola Maganga, Deo Mwanambilimbi na Tunu.

Mwanamuziki mwalikwa wa bendi ya Kalunde Kasaloo Kyanga akifanya mambo makubwa na mnenguaji wa bendi hiyo Queen Vero kabla ya kuanza kwa onyesho la Usiku wa Nchinga kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza.

UKITAKA KUTOKA BRINGBRING NENDA ZIZZOU FASHION VICTORIA!!

Unataka kutoka Bringbring! nenda kwa Zizzou Fashion mambo yote kuhusu mavazi ya kiume na ya kike pamoja na kunyoa kwa puande wa wanaume utakuwa Freshi ukitokwa kwa Zizzou Fashion pale Victoria Petrol Station

UKATILI HUU UNAOFANYWA NA BAADHI YA WANAWAKE KWA WATOTO WAO MPAKA LINI?

Maiti ya kitoto kichanga ikiwa imetupwa ndani ya jalala la shule ya Mtoni Sifa haikufahamika ni mwanamke gani ambaye amekitupa kichanga hicho FULLSHANGWE inaomba Radhi kwa kutumia picha hii lakini huu ndiyo ukweli wa ukatili unaofanywa na baadhi ya wanawake kwa watoto wao hii inasikitisha na sijui ukatili huu utaisha lini.
Wakazi wa Mtoni sabasaba wakiangalia maiti ya kitoto kichanga kilichotupwa na mwanmke ambaye hakufahamika katika jalala la shule ya msingi Mtoni Sifa jioni hii kuekuwepo na matukio mengi ya kutupa wattoto katika jiji la Dar es alaam.

WABUNGE WA CCM WAPAMBANA KWA AHADI FAINALI ZA NSSF!!

Uhuru wakishangilia mara baada ya kutwaa ubingwa wa NSSF leo.
Fainali za kombe la NSSF zilizofanyika kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe leo ziligeuka uwanja wa mapambano kati ya wabunge wa CCM, katika fainali hizo ambapo zilikuwa zikicheza timu mbili za vyombo vya habari ambazo ni Uhuru Publication na New Habari Cooparation.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute kulitokea mashindano makubwa ya wabunge ambao ni Mh Rostam Azizi, Dr. Harrison Mwakyembe, mwanamama Anne Kilango na katibu mkuu wa chama hicho mzee Yusufu Makamba.
Mpambano huo kati ya wabunge hao ulianza baada ya Mbunge na mmiliki wa kampuni ya New Habari Cooparation Rostam Azizi kutuma ujumbe kwa mmoja wafanyakazi wa kampuni hiyo Muhingo Rweyemamu na kuahidi kuipa timu yake shilingi milioni 2 mbali ya zawadi itakayotolewa na NSSF endapo itaifunga Uhuru Publication tangazo hilo lilipotangazwa ndipo naye Dr. Harrison Mwakyembe alipotuma ujumbe wa kuipa timu ya Uhuru Publication Shilingi milioni 6 kama wataishinda New Habari.
Mpambano wa wabunge hao haukuishia hapo naye mama Anne Kilango aliahidi kuipa Uhuru Publication Milioni 2 na hatimaye katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba aliahidi kuipa timu hiyo shilingi Milioni 1 ikiwa itachukua ubingwa ahadi hizo zilionekana kuwapa nguvu Uhuru ambao walicheza kwa kujituma na kujipatia magoli matatu kupitia kwa wachezaji wake Emanuel Mushi, Jamal Rashid na Tuzo Jackson hivyo wakajizolea milioni mbili na nusu na kikombe pamoja na shilingi milioni 9 ambazo ziliahidiwa na wabunge Dr. Harrison Mwakyembe, Anne Kilango na Yusuf Makamba na kwafanya waibuke na kitita cha shilingi milioni 11.5 goli pekee la New Habari limefungwa na mchezaji Said Makala na kuondoka na shilingi milioni 2 na kikombe, katika fainali hizo pia kwa mchezo wa netiboli zilicheza timu za Busness Printers na NSSF ambapo NSSF waliibuka mabingwa katika mchezo huo
Wachezaji wa Timu ya New Habari wakipozi na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa.
Mh.Joel Bendera akiteta na Dr. Ramadhan Dau

Mh. Joel Bendera Naibu Waziri Mkuu wa Habari Utamaduni na Michezo akikagua timu ya New Habari Cooparation kabla ya kuanza kwa kipute cha Fainali ambapo Uhuru Pablication walishinda magoli 3-1.
Mgini wa Rasmi Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera akikagua timu ya Uhuru Pablications kabla ya pambano la Fainali kati kati ni mkurugenzi wa NSSF Dr. Ramadhan Dau.

Taji Liundi mkurugenzi wa TBC International kushoto na Antony Katona wa Media Solution ambao walikuwa ni wajumbe wa kamati ya mashindano ya NSSF wakipozi kwa picha mara baada ya kumalizika kwa fainali hizo kwa mafanikio.
Nao mashabiki wa Uhuru Publications hawakuwa nyuma kuisapoti timu yao.

Mashabiki wa New Habari Cooparation wakifuatilia kwa makini mpambano wao wa fainali kati yao na Uhuru Publications katika viwanja vya TCC Chang'ombe leo.

MAGEMBE ATANGAZA WALIOFAURU KUINGIA KIDATO CHA TANO 2009!!

Waziri wa Elimu na Mafunzo Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha tano na katika vyuo vya ufundi kwa mwaka wa masomo 2009. Kushoto ni Kaimu Kamishina wa Elimu Leonard Musaroche na kulia ni Msaidizi wa Waziri Alfred Kilasi.

MTAMBO WA SONGAS KUANZA UZALISHAJI NDANI YA WIKI MBILI!!

Waziri ngeleja akiongea na wana habari katika moja ya mikutano yake.
Na Anna Nkinda – Maelezo
28/03/2009 Dar es Salaam Serikali imesema kuwa ndani ya wiki moja kuanzia leo mtambo wa kuzalisha umeme wa Kampuni ya Songas ulioharibika utakuwa tayari na kuanza kufanya kazi kama kawaida.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alipofanya ziara ya kutembelea mitambo hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam ili kuona maendeleo ya matengenezo ya mitambo miwili iliyosababisha upungufu wa megawati 50 za umeme katika gridi ya Taifa.
“Kwa taratibu za kawaida matengenezo ya mtambo huu yangechukua miezi mitatu hadi minne ila mafundi wanafanya kazi ya matengenezo kwa bidii na hatua waliyofikia watachukua muda mfupi kumaliza kazi hii”, alisema waziri Ngelleja.
Aliendelea kusema kuwa mgao unaoendelea ni kutokana na ajali ya kuharibika kwa mtambo mmoja kwani mtambo mwingine uko katika matengenezo ya kawaida ila baada ya kuharibika kwa mtambo huo ndiyo tatizo limeongezeka zaidi.
Ngelleja alisema kuwa, “Serikali haina mpango wa kuwafanya wananchi waishi gizani zipo hatua nyingi ambazo wanazichukua na watazitolea ufafanuzi kadri siku zinavyokwenda”.

Mtambo wa pili wenye uwezo wa kuzalisha megawati 35 ambao uko katika matengenezo ya kawaida unatarajia kuanza kazi baada ya wiki mbili tangu kuanza kwa matengenezo hayo.
Hivi sasa mtambo ulioharibika umefumuliwa na kuanza kutengenezwa upya na una uwezo wa kuzalisha megawati 20 za umeme kama utaanza kazi utakuwa umepunguza makali ya mgao wa umeme kwa kiasi fulani.
Kuanzia Alhamisi wiki hii jijini Dar es Salaam kumeanza mgao wa umeme ambao unaleta usumbufu kwa wananchi hii ni kutokana na kuharibika kwa mitambo hiyo .

KANDORO MGENI WA HESHIMA FAINALI YA NYAMA CHOMA LEADERS!!

Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam Mh. Abbas Kandoro anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima katika shindano la Safari Lager Nyama Choma 2009 linalotarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Leaders Kinondoni jumapili ijayo machi 29, katika shindano hilo mabaa mbailmbali yenye majiko ya kuchoma nyama yatashindana lili kumpata mshindi wa shindano hilo kwa mwaka huu wadau wote mnakaribishwa ili mpate ladha tofauti ya nyama choma katika picha ni mkuu wa mkoa akiongea na wananchi katika moja ya mikutano yake. Majaji wakionja nyama katika moja ya vituo viliyotumika kufanya mchujo ili kupata nwashiriki washiriki wa shindano hilo litakalofanyika jumapili ijayo.


Waziri Ardhi Namibia atembelea Kisarawe!!

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kept.John Chiligati akimwonyesha daftari la kutunza kumbukumbu za usajili wa ardhi wilayani Waziri wa Ardhi wa Namibia Alpheus Naruseb
Na Zawadi Msalla- Maelezo
SERIKALI ya Tanzania imepongezwa kwa kuwa mfano mzuri katika mipango ya matumizi ya ardhi.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Ardhi wa Namibia Alpheus Naruseb alipotembelea wilaya ya Kisarawe kijiji cha Mitengwe kwa madhumuni ya kujifunza Mipango ya Ardhi inavyoendeshwa nchini.
Naruseb alisema tofauti na nchini kwake Namibia , Tanzania imeonesha kufanikiwa katika kupanga ardhi na kugawia wananchi hati.
‘Kwetu sisi Namibia Ardhi inamilikiwa na wananchi hivyo kujenga tabaka la wenye ardhi na wasio na ardhi” Alisema Naruseb
Aidha akieleza mipango hiyo Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kept.John Chiligati amesema uamuzi huo wa kupanga mipango ya matumizi ya ardhi imetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi yenye utawala bora na serikali yake inahakikisha kuwa wananchi wake wanapata ardhi na hati miliki ili kuondoa migogoro midogomidogo ya ardhi.
Akitoa ufafanuzi wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini waziri Chiligati alisema lengo la serikali ni kuhakikisha nchi nzima inafanyiwa mpango wa ardhi katika vijiji.mpaka sasa baadhi ya mikoa imeshaanza kutekeleza sera hiyo mikoa hiyo ni pamoja na Iringa,na Pwani.
Kwa upande wa wa kazi wa Kijiji hicho cha Mitengwe Waziri aliwashauri watendaji wake kuharakisha upimaji wa mashamba ili kuwapatia hati miliki wananchi.
Chiligati alisisitiza kuwa ni ilani ya CCM inayotekelezwa kwa sasa na Kisarawe imekuwa mfano mzuri ambapo mpaka sasa Kisarawe imeweza kupanga vijiji 8 kati ya vijiji 78 vilivyo katika mpango.
Wakisoma risala yao wakazi wa Mitengwe walisema serikali ya kijiji imekwisha tekeleza mipango mizuri ya ugawaji ardhi kwa shughuli za kilimo ,ufugaji,maeneo ya ujenzi,viwanja vya michezo na sehemu ya mnada wa mifugo.
Licha ya kujifunza mambo mbalimbali ya ardhi kutoka Tanzania Waziri huyo wa Namibia alipatiwa zawadi mbalimbali zikiwemo shoka,kigoda,mgolole na kupewa uzee wa kijiji na jina la Pembe hayaga likiwa na maana ya Pembe haipotei.Pia aliweka jiwela msingi la serikali ya kijiji hicho.

Ukiitaka hii Honda ichukue!!

Honda CR-V short specifications (2004 UK model)
Color: Silver
Odometer: 71,000 Km
Steering: Right
Seating Capacity:
5
Towing Capacity:
1500 lbs (680 kg)
Cargo volume:
with rear seats up:with rear seats folded
33.5 cu. ft (949 liters)72.0 cu, ft (2039 liters)
Engine:
2.4-Liter, DOHC 16-Valve, Aluminum Alloy 4-cylinderwith i-VTEC (Intelligent Variable Valve Timing and Lift Electronic Control with VTC and VTEC) 160 hp @ 6,000 rpm, 162 lb-ft @ 3,600 rpm
EPA Fuel Economy:
2WD Automatic:4WD Automatic:4WD Manual:
city: 23 MPG (10.2 L/100km)hwy: 29 MPG (8.1 L/100km)city: 22 MPG (10.7 L/100km)hwy: 26 MPG (9.0 L/100km)city: 21 MPG (11.2 L/100km)hwy: 25 MPG (9.4 L/100km)
Recommended Fuel:
Regular Unleaded - Gasoline
Fuel Tank Capacity:
58 liters
Engine Oil capacity
(with filter):
5.0 liters
Safety Specifications: Air Bags
Imported: From United Kingdom Serious Buyer Call 255 764 856 680 -255 714 238 070