Waziri Ardhi Namibia atembelea Kisarawe!!

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kept.John Chiligati akimwonyesha daftari la kutunza kumbukumbu za usajili wa ardhi wilayani Waziri wa Ardhi wa Namibia Alpheus Naruseb
Na Zawadi Msalla- Maelezo
SERIKALI ya Tanzania imepongezwa kwa kuwa mfano mzuri katika mipango ya matumizi ya ardhi.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Ardhi wa Namibia Alpheus Naruseb alipotembelea wilaya ya Kisarawe kijiji cha Mitengwe kwa madhumuni ya kujifunza Mipango ya Ardhi inavyoendeshwa nchini.
Naruseb alisema tofauti na nchini kwake Namibia , Tanzania imeonesha kufanikiwa katika kupanga ardhi na kugawia wananchi hati.
‘Kwetu sisi Namibia Ardhi inamilikiwa na wananchi hivyo kujenga tabaka la wenye ardhi na wasio na ardhi” Alisema Naruseb
Aidha akieleza mipango hiyo Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kept.John Chiligati amesema uamuzi huo wa kupanga mipango ya matumizi ya ardhi imetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi yenye utawala bora na serikali yake inahakikisha kuwa wananchi wake wanapata ardhi na hati miliki ili kuondoa migogoro midogomidogo ya ardhi.
Akitoa ufafanuzi wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini waziri Chiligati alisema lengo la serikali ni kuhakikisha nchi nzima inafanyiwa mpango wa ardhi katika vijiji.mpaka sasa baadhi ya mikoa imeshaanza kutekeleza sera hiyo mikoa hiyo ni pamoja na Iringa,na Pwani.
Kwa upande wa wa kazi wa Kijiji hicho cha Mitengwe Waziri aliwashauri watendaji wake kuharakisha upimaji wa mashamba ili kuwapatia hati miliki wananchi.
Chiligati alisisitiza kuwa ni ilani ya CCM inayotekelezwa kwa sasa na Kisarawe imekuwa mfano mzuri ambapo mpaka sasa Kisarawe imeweza kupanga vijiji 8 kati ya vijiji 78 vilivyo katika mpango.
Wakisoma risala yao wakazi wa Mitengwe walisema serikali ya kijiji imekwisha tekeleza mipango mizuri ya ugawaji ardhi kwa shughuli za kilimo ,ufugaji,maeneo ya ujenzi,viwanja vya michezo na sehemu ya mnada wa mifugo.
Licha ya kujifunza mambo mbalimbali ya ardhi kutoka Tanzania Waziri huyo wa Namibia alipatiwa zawadi mbalimbali zikiwemo shoka,kigoda,mgolole na kupewa uzee wa kijiji na jina la Pembe hayaga likiwa na maana ya Pembe haipotei.Pia aliweka jiwela msingi la serikali ya kijiji hicho.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment