HIVI JAMANI POOZI HILI SI NTAPATA PICHA!


Mama kibanda wa Zanzibar akipiga picha

MR SIMPLE ARUDI KIVINGINE!

Mr Simple katika poozi


Ilikuwa ni miaka ya mwishoni mwa tisini ambapo kundi la Love Forever lililokuwa linajumuisha wasanii Mr Simple na Marine Man lilikuwa juu sana baada ya nyimbo zao kama 'Umbo' na 'Shory' kuwa gumzo na kupigwa sana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni na redio nchini.

Baadaye waliachia albam ambayo kwa hakika haikuweza kuuza mpaka kufikia malengo yao hivyo wakaamaua kukaa benchi huku wakiusoma mchezo unavyokwenda.

Mwaka 2005,Renatus Pamba au kama anavyojulikana kama Mr Simple aliamua kutoka yeye kama yeye na kuona ya kwamba anaweza akafanya kitu na watanzania kupendenzwa nacho.Ndipo alipoachia wimbo wake mwenyewe akiwa kama mwanamuziki wa kujitegeemea uliokuwa unaitwa 'Mr Simple' aliomshirikisha mwanadada Jackline.

Wimbo huo uliokuwa kwenye mahadhi ya dancehall nao uliweza kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini.
Mwaka uliofuata,Simple aliachia nyimbo nyingine mbili kwa mpigo,'Father Of Dancehall' na 'kamata chati mbambali.

Tokea kipindi hiko chote,Mr Simple aliamua kupumzika kuhusu masuala ya muziki na kuamua kujishughulisha na shughuli nyingine.

“Niliamua kupumzika masuala ya muziki kidogo ili niweza kufanya shughuli zangu nyingine ambazo nilikuwa nahitaji muda mwingi kuzitekeleza na ndiyo maana sikuweza kusikika kwa takribani miaka mitatu.”Simple

Mwaka huu Mr Simple amedhamiria kufnaya mapinduzi halisi kwenye muziki wa dancehall nchini na mashabiki wake.
Mwanamuziki huyu aliongea na starehe na kusema ya kwmaba anarudi kwa nguvu zote mpaka aone ya kwmaba muziki wa aina ya dancehall unakubalika kama aina nyingine ya muziki hapa nchini.

“Nimerudi na sasa kwa nguvu zote,nawahakikishia ya kwamba nitafanya mapinduzi halisi,nataka kuutangaza vyema muziki wa dancehall nchini,sio kila siku tunang’ang’ania aina moja ya muziki,dancehall ni muziki bora ambao unahitaji kukubalika”Alisema.

Alipoulizwa ya kwamba kwa nini anasema ya kwamba dancehall ni muziki bora kuliko aina nyingine ya muziki,Simple alijibu ya kwmaba muziki huo ni bora kwasababu unachezeka na vilevile haupitwi na wakati kamwe.

“Sijawahi kusikia dancehall umepitwa na wakati,leo ukiwekewa nyimbo ya Sean Paul ya kwanza kabisa utasimama na kucheza,na ndiyo maana naamini ya kwamba dancehall ni muziki bora zaidi kulikko aina nyingine ya muziki .



“Ukifanikiwa kusikiliza nyimbo zangu mpya,utaamini haya nayosema kwakuwa kuna ladha flani ambazo lazima zitakuamsha kutoka kwenye kiti chako na kuanza kucheza,nyimbo zangu zote zinachezeka na sisiti kujisifia hilo kabisa kwakuwa naamini kile kitu ambacho nachokifanya”Alisema.

Albam ya Mr Simple itakayoijulikana kwa jina la ‘Father Of Dancehall’ ambayo anatarajia kuiachia mapema mwakani inatarajia kuwa na vibao nane vikiwemo vingine kama ‘Naapa’,’Senorita’ pamoja na ‘Nimestuka’ wimbo ambao ndio ataanza kuuachia kwanza.

Aliweza kufafanua kwanini ameamua kuiita albam yake hiyo ‘Father Of Dancehall’ kwamba anaamini yeye ndiye mkubwa wa muziki huo wa dancehall nchini na ndiyo maana ameamua kuiita albam yake jina hilo.

“Mimi ndiye ‘Father Of Dancehall’ hakuna ubishi kuhusu hilo hapa nchini,na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyosababisha niite albam yangu jina hilo”Simple.
Mbali na hayo yote,Simple alisema ya kwamba kamwe hawezi kufanya aina yeyote ya muziki zaidi ya dancehll kwakuwa ndio muziki ambao upo kwenye hisia zake saa zote hivyo hajawahi kuimba muziki wowote tofuati na dancehall na hatowahi kujaaribu kufanya hivyo.
Kabla ya kuwa mwanamuziki,Mr Simple alianza kwa kuwa Disko Joka,au kwa kifupi DJ huko mkoani Shinyanga na baadaye kuamaua kuacha kazi hiyo na kujikita kwenye muziki huku akiungana na mwezake kwa pamoja wakaunda Love Forever ambalo liliweza kudumu kwa takribani miaka sita na baadaye kuvunjika mwaka 2005.

Simple alipenda kuwashauri wanamuziki nchini kutokata tamaa labda baada ya kuona nyimbo zao hazipigwi kwenye redio,kwani alisema kila kitu kina muda wake muafaka hivyon watulize vichwa na kuanza upya.

“Wale wote waliojaribu kuimba na kukata tama,nawashauri watulize vichwa na kuangalia uystaarabu mwingine wa kutoka,nasema hivi kwasababu nina maana yangu,muziki hauhitaji pupa,wengie wameingia kwa pupa sasa hivi hawasikiki tena”Alisema.

Shukrani zake kwa dhati zinamuendea Mwenyezi Mungu kwani anaamini ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyemfikisha hapo alipo leo,hivyo kama asipomshukuru atakuwa hatendi haki na vilevile mashabiki wake wote.

De Plaizir amsifu Banana zoro!
Mwanamuziki kutoka nchini Congo,Blanchard De Plaizir anayefanyia shughulizake na muziki nchini Uingereza,aliyewasili nchini wiki iliyopita,amsifiamwanamuziki Banana wa nchini baada ya kusikiliza kazi zake palealipohudhuria moja ya shoo za B Band,Hunters.

Mwanamuziki huyo alisema ya kwmaba Tanzania imejaliwakuwa na wanamuziki wenye vipaji hivyo wanatakiwa kufanyia kazi vipaji hivyo ili waweze kusikika kimataifa.Aliweza kumtolea mfano mwanamuziki Banana kwa kusema ya kwamba Banana nimwanamuziki mzuri lakini anahitaji kusikika zaidi nje ya Tanzania ili aweze kukubalika.

“Nimeweza kushuhudia wanamuziki mbalimbali kwa muda niliokaa nao,nimependa jinsi Banana anavyofanya kazi zake,kwani ni mwanamuziki aliyebarikiwa kuwa na kipaji.Mbali na hayo, De Plaizir atarekodi nyimbo moja na mwanamuziki huyo pamoja na baadhi ya wanamuziki kutoka bendi ya Akudo kwakuwa anahitaji kupata kumbukumbu ya wanamuziki kutoka nchini.

“Narekodi ngoma na Banana pamoja na baadhi ya wanamuziki wa Akudo ili tu niweze kuweka kumbukumbu yangu hapa nchini,wimbo utakuwa bora na wakimataifa zaidi,kaeni tayari”Alisema.Mwanamuziki huyo ambaye anatarajia kuondoka nchini wiki hii baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi na wanamuziki hao.

WACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU!

Mrs. na Mr. Pascar Mhindi wakimwangalia mtoto wao Philip aliyeshikwa na baba wa ubatizo Bw Honory Lemasani mara baada ya kubatizwa katika kanisa katoliki la mtakatifu Martha mikocheni B. jijini jumapili iliyopita.

UNATISHA MZEE!

Mwimbaji mahiri wa Bendi ya FM ACADEMIA Jose Mara ambaye kwa sasa anatisha na anafananishwa na mwimbaji Farii Ipupa kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya kongo aliyekuwa akiimba katika bendi ya Quatar te Latin ya Kofii Olomide, kutokana na uwezo alionao katika kubadilibadili sauti yake anapoimba .

AH! SIYO FUNDI WA KUPIGA GITAA TU HATA KULEA NAWEZA



Elistone Angai wa Vibration Band akiwa amembeba mtoto ambaye jina lake halikufahamika

WADAU WA MULTCHOICE NA BENNY KISAKA


Kuanzia kushoto Revina Bandiai, Baraka Shelukindo, Benny Kisaka na Furaha Samalu wakibadilishana mawazo

WANAMUZIKI KUFAIDIKA NA CELLULANT


Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Cellulant Tanzania Bw Jide Harisson akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo itakayojihusisha na uuzaji wa milio ya simu za mkononi kwa kutumia nyimbo za wanamuziki wa hapa nyumbani jana 25/09/2008 kwenye Hotel ya Southern Sun jijini

Msemaji mkuu wa kampuni ya Cellulnt Bw. Khamis Dacota akielezea jambo kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa kampuni hiyo itakayojihusisha na uuzaji wa milio ya simu za mkononi kwa kutumia nyimbo za wasanii wa hapa nchini kampuni hiyo ipo katika nchi kadhaa za Afrika kama Nigeria, Ghana, Kenya Uganda na sasa Tanzania uzinduzi huo ulifanyika kwenye Hotel ya Southern Sun Jijini Jana 25/09/2008

Producer Ally Baucha kutoka Baucha Records hakubaki nyuma ili kujua haki za msanii katika kampuni ya Cellulant wakati itakapoanza kuingia mikataba na wasanii katika kutumia nyimbo zao kwenye milio ya simu za mkononi.

Noora akiuliza swali kutaka kupata ufafanuzi zaidi juu ya kazi za Cellulant na ushirikiano wake kwa wasanii katika kufanya kazi pamoja ili msanii pia afaidike na muziki.


Wasanii Mkoloni na Noora wakipata kinywaji laini huku wakionekana kuwa makini ili kuona kilichokuwa kikiendelea hapo Southern Sun

KKutoka kulia Babu Tale katikati Muli B. (Bling Bling) kutoka Kachumbari Fleva na mwisho B. 12 kutoka Clouds wakisikiliza kwa makini maelezo ya maofisa wa Cellulant.

Kulia Suka, katikati Slim Producer kutoka Bongo Potrait na mwisho Dully Sykes Msanii na Mkurugenzi wa Dhahabu Records hawa nao walikuwepo kushuhudia Uzinduzi wa Cellulant kampuni itakayouza milio ya sauti za simu za mkononi ikihusisha nyimbo za wanamuziki mbalimbali hapa nchini.

MAMBO KUJIPA SHANGWE TU!

Jide naye kwa kuwarusha watu weekend, hajambo!.


Mkuu wa Huduma kwa wateja wa Benki ya Satandard Charted Bw. Ralph Watungwa akimkabidhi tiketi ya ndege ya kutoka Dar es alaam kwenda Beijing na kurudi Bw. Eneliko Luvanda ambaye ni mmoja wa washindi waliopatikana katika Droo ya mwisho ya bahati nasibu iliyokuwa ikendeshwa na benki hiyo makabidhiano yamefanyika katika tawi la kariakoo. kati ni meneja wa tawi hilo Gaudence Shawa na kushoto ni Awaichi Mawala.


Kulia Ralph Watungwa Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja kulia Meneja wa tawi la Standard Charted Kariakoo kati na Awaichi Mawala ofisa katika kitengo cha masoko benki hiyo wakiwa tayari kutoa zawadi kwa washindi.


Mkurugenzi wa kitengo cha huduma katika Benki ya Standard Charted Bw. Ralph Watungwa katikati Bi Hoyce Temu afisa wa Benki hiyo kitengo cha mawasiliano kulia na meneja wa tawi benki hiyo kariakoo Bw. Gaudence Shawa kushoto wakiwa katika hafla yakukabidhi zawadi kwa washindi wa bahati nasibu iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo

BIGBROTHER 111 IMENIONGEZEA UMAARUFU!


Latoya akizungumza na wapasha habari hapo Southen Sun Jijini Dar

MAMBO YALIKUWA KUJIPA RAHA TU, NILIENJOY!

Latoya akifafanua jambo pembeni dada Furaha Samalu Meneja Masoko Multchoice.

LATOYA LYAKURWA USO KWA USO NA WAANDISHI


Aliyekuwa Mshiriki wa BigBrother 111 Latoya Lyakurwa kati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Hotel ya Southen Sun leo 24/09/2008 mara baada ya kurejea nyumbani kuliani meneja masoko wa Multchoice Furaha Samalu na kushoto ni Meneja huduma Ronald Sherukindo.

MATONYA NDANI YA BUJUMBURA


Msanii wa Muziki wa Bongofleva maarufau kwa jina la Matonya anatarajia kuwa na Ziara ndefu ya kimuziki katika Afrika mashariki Ulaya na Marekani ambapo anatarajia kuanzia nchini Burundi.
Matonya ametutonya kwamba katika sikukuu ya Idd atakuwa mjini Bujumbura kwa maonyesho kadhaa ya kimuziki kabla hajarejea nyumbani na kujiandaa kwa maonyesho mengine hapa nyumbani kabla ya kuanza ziara nyingine kama hiyo katika bara la Ulaya na Marekani mwishoni mwa mwaka huu.
Hakutaka kutaja kampuni ambayo ameingia nayo mkataba wa maonyesho hayo kwa madai kuwa wakati ukifika ataitaja lakini amesema kila kitu kiko sawa na akitoka burundi anarudi kujiandaa na tamasha kubwa la Fiesta litakalofanyika huko Tanga tarehe nne mwezi ujao na mikoa mingine kisha yataanza maandalizi ya safari ya Ughaibuni akianzia na Uholanzi, Ujerumani na baadae Marekani.
Sawa Matonya sisi Tunakutakia Maandalizi Mema na Safari Njema!

MALOU STOUNCH AREJEA FM ACADEMIA

Mwanamuziki wa siku nyingi na maarufu hapa nchini anayejulikana kwa jina la Malou Stounch na aliyeahi kutamba na kundi la Fm Acadimia (wajelajela) amerejea katika kundi la muziki la Fm Academia (Original) habari zilizoifikia FULLSHANGWE zinasema mwanamuziki huyo atatambulishwa rasmi katika onyesho la sikukuu ya Eid El Fitr litakalofanyika kwenye kijiji Cha makumbusho kijitonyama.
Akizungumzia zaidi Meneja wa Bendi hiyo Mujibu Khamis amesema katika onyesho hilo pia Bendi hiyo itatambulisha mtindo wake mpya unaoitwa (Zombolo na Matembele) Yaani kwa Kiswahili (Samaki na Matembele)
Mujibu ameongeza kuwa mtindo huo utakuwa tishio kama wanavyojulikana Fm Academia kwa kutoa burudani kali hilo mashabiki watashuhudia wenyewe hapo makumbusho katika sikukuu ya Idd
Wakati huohuo Mujibu amesema mwanamuziki Nguli wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo General Def Defao anatarajia kutoa buruda ni ya kukata na shoka katika mikoa ya kandaya Ziwa katika mikoa ya Mwanza Kagera na ambapo katika sikukuu ya idd Mosi atakuwa Mwanza na Idd pili atakuwa Bukoba na Idd tatu atakuwa Geita wakazi wa huko kaeni mkao wa kula burudani hiyoooo! inakuja


MAMA MALKOMITO!
Paulin Zongo AKA Mama Malkomito


Mwanamuziki Paulin Zongo ambaye aliwahi kutamba akiwa na Bendi ya TOT Yuko mbioni kukamilisha Albam yake itakayokuwa na nyimbo Nane.


Akizungumza na FULLSHANGWE jijini Zonga amaesema tayari amekwisharekodi nyimbo Sita na sasa hivi yuko mbioni kumalizia nyimbo mbili zilizobaki, amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Umechezea Bahati, Kifo cha mama,Mimi na wewe Daima,Dunia ni ndogo Remix, Safari Remix, Hatuendi hivyo na Usibahatishe Pia Heshima ambazo ndiyo anamalizia kuzirekdi studio,


Zongo ameongeza kuwa albamu hiyo itawaonyesha mashabiki wa wake kuwa bado yupo kwenye Gemu na uwezo wa kufanya kazi nzuri upo na ninajua wayapata burudani murua kupitia albam yangu hiyo.


Ameongeza kuwa amerekodi katika studio tofauti ili kuleta radha tofauti ya muziki kwani kila producer ana uwezo wake na kipaji chake kama tulivyo sisi wanamuziki


amezitaja studio hizo kuwa ni (Big Tone, Metro, Dream Studio na Soundcrafters! albam hiyo inatarajiwa kuingizwa sokoni mwishioni mwa mwaka huu lakini kwanza nitaingiza single mbili moja kwenye vituo vya Televisheni na nyingine kwenye vituo vya Redio ili kuwaonjesha mashabiki wangu sambamba na kuanza kwa bendi yangu itakayojiulikana kama Zongo Band (The Dream)

ONGEZA SPEED KIDOGO!


Meneja wa Kilimanjaro Fitness Centre Bw. Nemes Chiwalala akimuonyeshaMary Mkini jinsi ya kutumia mashine ya mazoezi viungo katika viwanja vya mnazi mmoja katika kuadhimisha siku ya michezo nchini jumapili iliyopita,

UNAJUAGA VILE NAJUA FRENCH TU!
Warembo hawa kutoka marekani Casey Toth kulia na Mica Whit walivutiwa sana na muziki wa Akudo Impact kitu kilichwafanya kumfuata Totoo Ze Bingwa Rapa wa Bendi hiyo awaelekeze wapi wanafanya maonyesho yao hata hivyo ilikuwa kuwaelekeza kwani ana mpango wa kwenda Tuisheni ya kizungu mwaka 2010.

HIZI KETE MBILI NAMALIZA BAO!

Mwandishi mwandamizi na mtangazaji wa Televisheni ya Chanel Ten kulia Salum Mwalimu akionyesha uwezo wake katika michezi ya jadi kwa kucheza bao katika kuadhimisha siku ya michezo nchini iliyofanyika viwanja vya Mnazi moja jijini Dar.

HII NI SAIZI YA HASHEEM THABIT!


Mbaga Mwambona mmoja wa viongozi wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini akionyesha moja ya aina ya kiatu kinachotumiwa na wachezaji wa mpira huo katika maazimisho ya siku ya michezo nchini iliyofanyika jumapili 21/8/2008 katika viwanja vya mnazi mmoja.

SIKU SIMBA WA YUDA ALIPORUDI KUNDINI!


Nawaambieni wana simba mimi nilionewa tu nimefanya kazi kwa uwezo wangu wote na akili yangu yote huku "nikipewa Raha na Mke wangu" mwaka jana kila nilipoongoza msafara wa simba kwa ajili ya mechi za ligi kuu nilirudi na pointi tatu Mwana Kaduguda katibu mkuu wa klabu ya Simba akilonga mbele ya kutano mkuu.

SIYO KURAPU TU HATA KUFULAMA NA PIKIPIKI NAWEZA!


Msafiri Diof akionyesha anavyioweza kufanya maujuzi juu ya pikipiki japokuwa chombo hicho cha moto hakina mjuzi.

VIBRATION WANAVAIBRATE MUGONGOMUGONGO


Wana Vibration wakifanya vitu vyao chini ya Aistene Angai mwishini wa wiki!

SIKILIZENI IVO HAJATUTENDEA HAKI WALAAH !


Myenyekiti wa Yanga Imani Madega akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari katika kikao cha Dharura kwenye mtaa wa Samaora na kufafanua kuhusu suala la Ivo Mapunda kutokomea kusikojulikana

SIMBA JAMANI KULIKONI?, KAZENI BUTI EBO!


Kikosi cha simba kikiwa katika picha ya pamoja simba imeshapoteza michezo yake miwili na kushinda miwili kati ya michezo iliyocheza tangu ligi kuu ya Vodacom ianze.

KASSIM MAPILI AKILOGA



Mzee Kassim Mapili kulia akiongea na mwandishi wa gazeti la Spoti Starehe Peter Mwenda juu ya maandalizi ya Shindano hilo katikati ni mjumbe kamati ya maanadalizi komadoo Hamza Kalala.
CHAMUDATA YAANDAA SHINDANO LA WIMBO BORA
Chama cha muziki wa dansi nchini kimeandaa shindano la kutunga nyimbo kumi Bora litakalo shirikisha bendi mbalimbali hapa nchini kutoka mikoa tofauti ya Tanzania Bara.
Akizungumza na FULLSHASHGWE mwenyekiti wa CHAMUDATA na Kamati ya maandalizi Mzee Kassim Mapili, amesema Mpaka sasa bendi nyingi Tayari zimejitokeza na kulipa ada ya kushiriki kwenye shindano hilo linalotarajiwa kuanza 17/10/2008 katika viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka 15/11/2008 ambapo ndiyo itakuwa Fainali yake inayotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini.

Mapili amezitaja bendi zilizolipa ada za kushiriki na mikoa zinakotoka kuwa ni Anyanyaa Band kutoka Dar,Vijana Jazz Dar,Shikamoo Jazz Dar,Seven Blind Band Dar, Mark Music Band Dar, TMA Jazz Arusha Monduli, Super Volcano Dar, Magereza Jazz Dar,Sandton Band Dar,Abdull Salvador and The Hisia Band Dar, Victory Band Dar, Ufipa Sound Band Rukwa,Kingstone Band Morogoro,Rukwa Intarnetional ya Rukwa, Achigo Band Dar, Fax Music Band ya Tanga WAzee Sugu Dar, Akudo Impact Band Dar, Lunch Time Band Dar, Maina Music Band Dar na Bwagamoyo Sound kutoka Pwani

Ameongeza kuwa kutakuwa na vituo saba ambavyo ni Dar es alaam, Morogoro, Mwanza, Tabora, Mtwara, Dodoma, Arusha na Rukwa ambapo kila kituo kitatoa washindi wawili amabao watakutana na washindi kumi na sita watakaotoka mkoa wa Dar es salaam na kupambana kwenye Fainali ya Tarehe 15/11/2008 katika uwanja wa Taifa jijini na amezitaka bendi nyingi kujitokeza kwenye shindano hilo ili ziweze kuonyesha uwezo wao.

BALOZI JON LOMOY
Barozi wa Norwy Nchini Bw. Jon Lomoy akikaribisha wageni waalikwa kwenye Tamasha la muziki na chakula cha utamaduni wa Norway kwenye Hotel ya Movenpick ambapo kundi la Umoja Cultural Flying Carpet lenye wasanii mchanganyiko kutoka Tanzania, Norwy na Mosambique ndilo lililotoa burudani, tamasha hilo lilifanyika jumatatu iliyopita 15/09/2008 na liliandaliwa na ubarozi huo.



Enika Bukuku Nae akafanya vitu vyake


Joseph Olelesi na Mamaa Elly (Mama Kibanda)

Hawa nao walijimwaga hapo MovenPick kutoka kulee Zanzibar.

MIsosi ilikuwa ya kumwaga


wageni waalikwa walipata nafasi ya kuonja chakula cha utamaduni wa Norway pia kama unavyoona kila mtu anajisevia

Tuko Tayari Kwa Kuwapa Burudani



Wapiga vyombo wa kundi la Umoja wakiwa tayari kwa kutoa Burudani hapo Movenpick

Hapo Vipi?

Waneguaji wa kundi la umoja Cultural Flying Carpet wakifanya vitu vyao jukwaani



Wageni mbalimbali walijitokeza kwenye Tamasha la muziki na chakula cha utamaduni wa Norway lililotumbuizwa na kundi la Umoja Cultural Flying Carpet linalounganisha wasanii kutoka Tanzania Mosambique na Norwy tamasha hilo lililoandaliwa na ubarozi wa Norway nchini katika Hotel ya Movenpick mwanzoni mwa wiki

Tabora nayo Wamo


Mji wa Tabora unavyoonekana kwa chini Picha hii ametutumia mdau Gerald Hando aliyekuwepo kwenye Safari hiyo ya kwanza, mara baada ya ATC kuanzisha Rout ya Dar, Tabora na Kigoma.

ATC YAANZA SAFARI ZA TABORA NA KIGOMA

Shirika la ndege la Tanzania ATC limeanzisha safari zake kati ya Dar es alaam Tabora na kigoma katika kuwarahisishia watanzania usafiri hapa nchini na kuongeza ufanisi wa utendaji wa shirika hilo lakini pia kujiongezea faida Safari hizo zilizinduliwa jana kwa ndege yao mpya kama anavyoonekana mkurugezi wa shirika hilo David Mataka aliyekaa kushoto akiwa ndani ya ndege hiyo wakati iliporuka kuelekea Tabora na Kigoma kulia ni mtangazaji wa Radio Clouds Gerald Hando.

Mdau Daudi Mambya akipoozi na Warembo
Daudi mambya (kushoto) mmoja wa vijana maarufu hapa jijini alikuwepo katika kupongeza mabalozi wa Zain hivi karibuni katika ukumbi wa Guanzhou Garden huku Machozi Band ikishusha burudani kali.

BAADA YA USHINDI NAKULA RAHA!


Mwenyekiti wa Yanga Imani Mahugila Madegaa linaswa na Camera ya FULLSHANGWE akipunga upepo katika viwanja vya Readers mara baada ya timu yake kupata ushindi dhidi ya mtibwa kushoto ni mkurugenzi wa simba Evarist Hagila Na kulia ni Shabiki mkubwa wa Yanga Phill Mmari.

VIPI MNATUONAJE NA POOZI LETU?

Jannet Isinika a Chaz Baba wakila poozi Si Mchezo!

TWANGA PEPETA WAJIFUA VIKALI!

Kundi la Afrcan Stars Twanga Pepeta liko kwenye mazoezi makali kwa ajili ya kuingia studio kurekadi albam yao hivi karibuni akizungumza na FULLSHANGWE katibu wa Bendi hiyo Abuu Semhando amesema tayari wana nyimbo nne ambazo wanafanyia mazoezi vikali nyimbo hizo ni Sumu ya Mapenzi mtunzi (Chokoraa), Shida ni Darasa (Chaz Baba), Nazi haivunji jiwe (Thabit Abdull) na Naisha iliyotugwa na (Saleh kupaza) wanatarajia kurekodi katika studio yao ya Aset Records iliyoko Mbezi katika picha kuanzia kushoto ni Victor Mkambi, Chokoraa,Chaz Baba na Jannet Isinika

MASTAA KIBAO DHAHABU RECORDS!
Mkurugenzi mtendaji wa studio ya Dhahabu Records Dully Sykes amesema hivi sasa wasanii wengi maarufu katika muziki wa Bongo Fleva Wamevutiwa na ubora wa studio yake na wamejitokeza kwa wingi kwenda kurekodi katika Studio zake zilizoko Tabata wasani ambao wamesharekodi mpaka sasa ni Josse Chamelion kutoka Uganda,Chid Benz,Chege, Mh. Temba, Mwana FA na kundi la TMK Wanaume Family katika picha ni Dully Sykes kulia na Chege

Vipi Michango inatolewa mwenyekiti


Mh Temba aliyesimama akifuatilia kwa karibu kikao kinavyoendelea

MWANAUME KUOA BWANA Mheshimiwa Temba Kutoka Kundi la muziki la TMK Wanaume Family Anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni mwezi wa kumi na mbili ambapo ameielezea FULLSHANGWE kuwa harusi yake itafungwa Tarehe 13/12/2008 hapa jijini Dar es salaam na jana ndiyo kilifanyika kikao chake cha kwanza kwenye ukumbi wa sagara Tcc Club kikihudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo wachezaji wa mpira wa kikapu Temba hakutaka kuweka wazi hasa ni nani anatarajia kumuoa kwa madai kuwa atajulikana hapo baadae kama anavyoonekana meneja mkuu wa kundi hilo Said Fella wa pili kutoka kulia
katika picha akiongoza wenzake kuhakikisha mambo yanakwenda sawa jumla ya shilingi milioni Tano na nusu zilipatikana ikiwa ni ahadi na Fedha Taslimu

nimekuja kupiga mabao tu simba


Mshambuliaji wa kinaigeria wa simba akipiga stori na rafiki yake Alex.