MR SIMPLE ARUDI KIVINGINE!

Mr Simple katika poozi


Ilikuwa ni miaka ya mwishoni mwa tisini ambapo kundi la Love Forever lililokuwa linajumuisha wasanii Mr Simple na Marine Man lilikuwa juu sana baada ya nyimbo zao kama 'Umbo' na 'Shory' kuwa gumzo na kupigwa sana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni na redio nchini.

Baadaye waliachia albam ambayo kwa hakika haikuweza kuuza mpaka kufikia malengo yao hivyo wakaamaua kukaa benchi huku wakiusoma mchezo unavyokwenda.

Mwaka 2005,Renatus Pamba au kama anavyojulikana kama Mr Simple aliamua kutoka yeye kama yeye na kuona ya kwamba anaweza akafanya kitu na watanzania kupendenzwa nacho.Ndipo alipoachia wimbo wake mwenyewe akiwa kama mwanamuziki wa kujitegeemea uliokuwa unaitwa 'Mr Simple' aliomshirikisha mwanadada Jackline.

Wimbo huo uliokuwa kwenye mahadhi ya dancehall nao uliweza kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini.
Mwaka uliofuata,Simple aliachia nyimbo nyingine mbili kwa mpigo,'Father Of Dancehall' na 'kamata chati mbambali.

Tokea kipindi hiko chote,Mr Simple aliamua kupumzika kuhusu masuala ya muziki na kuamua kujishughulisha na shughuli nyingine.

“Niliamua kupumzika masuala ya muziki kidogo ili niweza kufanya shughuli zangu nyingine ambazo nilikuwa nahitaji muda mwingi kuzitekeleza na ndiyo maana sikuweza kusikika kwa takribani miaka mitatu.”Simple

Mwaka huu Mr Simple amedhamiria kufnaya mapinduzi halisi kwenye muziki wa dancehall nchini na mashabiki wake.
Mwanamuziki huyu aliongea na starehe na kusema ya kwmaba anarudi kwa nguvu zote mpaka aone ya kwmaba muziki wa aina ya dancehall unakubalika kama aina nyingine ya muziki hapa nchini.

“Nimerudi na sasa kwa nguvu zote,nawahakikishia ya kwamba nitafanya mapinduzi halisi,nataka kuutangaza vyema muziki wa dancehall nchini,sio kila siku tunang’ang’ania aina moja ya muziki,dancehall ni muziki bora ambao unahitaji kukubalika”Alisema.

Alipoulizwa ya kwamba kwa nini anasema ya kwamba dancehall ni muziki bora kuliko aina nyingine ya muziki,Simple alijibu ya kwmaba muziki huo ni bora kwasababu unachezeka na vilevile haupitwi na wakati kamwe.

“Sijawahi kusikia dancehall umepitwa na wakati,leo ukiwekewa nyimbo ya Sean Paul ya kwanza kabisa utasimama na kucheza,na ndiyo maana naamini ya kwamba dancehall ni muziki bora zaidi kulikko aina nyingine ya muziki .



“Ukifanikiwa kusikiliza nyimbo zangu mpya,utaamini haya nayosema kwakuwa kuna ladha flani ambazo lazima zitakuamsha kutoka kwenye kiti chako na kuanza kucheza,nyimbo zangu zote zinachezeka na sisiti kujisifia hilo kabisa kwakuwa naamini kile kitu ambacho nachokifanya”Alisema.

Albam ya Mr Simple itakayoijulikana kwa jina la ‘Father Of Dancehall’ ambayo anatarajia kuiachia mapema mwakani inatarajia kuwa na vibao nane vikiwemo vingine kama ‘Naapa’,’Senorita’ pamoja na ‘Nimestuka’ wimbo ambao ndio ataanza kuuachia kwanza.

Aliweza kufafanua kwanini ameamua kuiita albam yake hiyo ‘Father Of Dancehall’ kwamba anaamini yeye ndiye mkubwa wa muziki huo wa dancehall nchini na ndiyo maana ameamua kuiita albam yake jina hilo.

“Mimi ndiye ‘Father Of Dancehall’ hakuna ubishi kuhusu hilo hapa nchini,na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyosababisha niite albam yangu jina hilo”Simple.
Mbali na hayo yote,Simple alisema ya kwamba kamwe hawezi kufanya aina yeyote ya muziki zaidi ya dancehll kwakuwa ndio muziki ambao upo kwenye hisia zake saa zote hivyo hajawahi kuimba muziki wowote tofuati na dancehall na hatowahi kujaaribu kufanya hivyo.
Kabla ya kuwa mwanamuziki,Mr Simple alianza kwa kuwa Disko Joka,au kwa kifupi DJ huko mkoani Shinyanga na baadaye kuamaua kuacha kazi hiyo na kujikita kwenye muziki huku akiungana na mwezake kwa pamoja wakaunda Love Forever ambalo liliweza kudumu kwa takribani miaka sita na baadaye kuvunjika mwaka 2005.

Simple alipenda kuwashauri wanamuziki nchini kutokata tamaa labda baada ya kuona nyimbo zao hazipigwi kwenye redio,kwani alisema kila kitu kina muda wake muafaka hivyon watulize vichwa na kuanza upya.

“Wale wote waliojaribu kuimba na kukata tama,nawashauri watulize vichwa na kuangalia uystaarabu mwingine wa kutoka,nasema hivi kwasababu nina maana yangu,muziki hauhitaji pupa,wengie wameingia kwa pupa sasa hivi hawasikiki tena”Alisema.

Shukrani zake kwa dhati zinamuendea Mwenyezi Mungu kwani anaamini ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyemfikisha hapo alipo leo,hivyo kama asipomshukuru atakuwa hatendi haki na vilevile mashabiki wake wote.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment