KASSIM MAPILI AKILOGA



Mzee Kassim Mapili kulia akiongea na mwandishi wa gazeti la Spoti Starehe Peter Mwenda juu ya maandalizi ya Shindano hilo katikati ni mjumbe kamati ya maanadalizi komadoo Hamza Kalala.
CHAMUDATA YAANDAA SHINDANO LA WIMBO BORA
Chama cha muziki wa dansi nchini kimeandaa shindano la kutunga nyimbo kumi Bora litakalo shirikisha bendi mbalimbali hapa nchini kutoka mikoa tofauti ya Tanzania Bara.
Akizungumza na FULLSHASHGWE mwenyekiti wa CHAMUDATA na Kamati ya maandalizi Mzee Kassim Mapili, amesema Mpaka sasa bendi nyingi Tayari zimejitokeza na kulipa ada ya kushiriki kwenye shindano hilo linalotarajiwa kuanza 17/10/2008 katika viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka 15/11/2008 ambapo ndiyo itakuwa Fainali yake inayotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini.

Mapili amezitaja bendi zilizolipa ada za kushiriki na mikoa zinakotoka kuwa ni Anyanyaa Band kutoka Dar,Vijana Jazz Dar,Shikamoo Jazz Dar,Seven Blind Band Dar, Mark Music Band Dar, TMA Jazz Arusha Monduli, Super Volcano Dar, Magereza Jazz Dar,Sandton Band Dar,Abdull Salvador and The Hisia Band Dar, Victory Band Dar, Ufipa Sound Band Rukwa,Kingstone Band Morogoro,Rukwa Intarnetional ya Rukwa, Achigo Band Dar, Fax Music Band ya Tanga WAzee Sugu Dar, Akudo Impact Band Dar, Lunch Time Band Dar, Maina Music Band Dar na Bwagamoyo Sound kutoka Pwani

Ameongeza kuwa kutakuwa na vituo saba ambavyo ni Dar es alaam, Morogoro, Mwanza, Tabora, Mtwara, Dodoma, Arusha na Rukwa ambapo kila kituo kitatoa washindi wawili amabao watakutana na washindi kumi na sita watakaotoka mkoa wa Dar es salaam na kupambana kwenye Fainali ya Tarehe 15/11/2008 katika uwanja wa Taifa jijini na amezitaka bendi nyingi kujitokeza kwenye shindano hilo ili ziweze kuonyesha uwezo wao.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment