FULLSHANGWE INAKUMUVUZISHIA MATUKIO YA USIKU WA NCHINGA SOUND MDAU, HEBU PATA VITU!

Wanengaji hawa walitisha sana wakati wakiwa na bendi hii kulia ni Amina Rusha Roho na Queen Vero wakiongoza mashambulizi jukwaani huku Rogat Hega na Muumini Mwinjuma wakichombeza kwa taratiibu kwa nyuma katika onyesho la usiku wa Nchinga lililofanyika kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza usiku wa kuamkia leo onyesho hilo lilikutanisha wanamuziki wote waliowahi kupiga muziki na bendi ya Nchinga Sound na lilikuwa maalum kwa kumpa pole aliyekuwa mlezi wa bendi hiyo
Mh. Mudhihir M. Mudhihir kutokana na kupoteza mkono wake mmoja katika ajali ya gari iliyotokea miaka kadhaa iliyopita jimboni kwake wakati akiwa katika shughuli za kijamii, onyesho lilikuwa zuri na la kuvutia na watu wengi walitamani bendi hiyo iendelee kufanya maonyesho mengine, Tovuti FULLSHANGWE pia inampa pole Mh. Mudhihir Mudhihir lakini pia inawapongeza wanamuziki hao kwa kukubaliana na kufanya onyesho hilo maana limetukumbusha mbali sana, kwa matukio mbalimbali ya onyesho hilo shuka chini ili upate uhondo zaidi mdau.
He! naye mamaa Maimartha mwana wa Jesse kutoka televisheni ya Afrika Mashariki EATV akafanya mambo makubwa ili kuweka kumbukumbu ya usiku huo wa Nchinga kama unavyomuona katika picha akiwa ameshika kinasa sauti akijiandaa kuongea na watu mbalimbali ukumbini hapo ili kuelezea hisia zao juu ya usiku wa Nchinga uliofanyika kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza usiku wa kuamkia leo.

hapa alikuwa hakamatiki mtu kwa shangwe mdau kila mtu alijipa raha vyakutosha.
Ilikuwa si haba manake watu walipata burudani walioitarajia kutoka kwa vijana hao wa Mh. Mudhihir M. Mudhihir enzi hizo.

Vimwana hawa wakaselebuka vyakutosha kwa shangwe za usiku wa nchinga.

Hapa kama kawaida yake Muumini Mwinjuma ameshawapandisha mzuka mashabiki wa bendi hiyo yaani nilitamani iendelee kufanya maonyesho kila wiki mdau.

Prince Muumini Mwinjuma akipandisha mzuka wa mpiga kinanda Deo Mwanambilimbi.


Kikosi cha Nchinga Sound kikianzisha mashambulizi kikiongozwa na Prince Muumin Mwinjuma, kwakweli lilikuwa ni bonge la onyesho kwa maana kwamba Nchinga ile ya zamani ilirudi kwa nguvu na kasi mpya.
Dada yake na Mbunge wa Nchinga Mh. Mudhihir M. Mudhihir Zuhura M. Mudhihir akitoa shukurani zake kwa waliokuwa wanamuziki wa Nchinga Sound kwa kumuenzi kaka yake kutokana na mchango aliokuwa akiutoa katika bendi hiyo Zuhura alimuwakilisha Mh Mudhihir ambaye hakuwepo kwenye onyesho hilo kutokana na sababu za kiafya.

Mkurugenzi wa TOT Plus John Komba kulia akiteta jambo na mwanamuziki mwalikwa wa Kalunde Band Kasaloo Kyanga kushoto ni mpiganaji Ojuku Abraham.
Wana Kalunde wakishambulia jukwaa kuanzia kulia ni Queen Vero, Junior, Rola Maganga, Deo Mwanambilimbi na Tunu.

Mwanamuziki mwalikwa wa bendi ya Kalunde Kasaloo Kyanga akifanya mambo makubwa na mnenguaji wa bendi hiyo Queen Vero kabla ya kuanza kwa onyesho la Usiku wa Nchinga kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment