WABUNGE WA CCM WAPAMBANA KWA AHADI FAINALI ZA NSSF!!

Uhuru wakishangilia mara baada ya kutwaa ubingwa wa NSSF leo.
Fainali za kombe la NSSF zilizofanyika kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe leo ziligeuka uwanja wa mapambano kati ya wabunge wa CCM, katika fainali hizo ambapo zilikuwa zikicheza timu mbili za vyombo vya habari ambazo ni Uhuru Publication na New Habari Cooparation.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute kulitokea mashindano makubwa ya wabunge ambao ni Mh Rostam Azizi, Dr. Harrison Mwakyembe, mwanamama Anne Kilango na katibu mkuu wa chama hicho mzee Yusufu Makamba.
Mpambano huo kati ya wabunge hao ulianza baada ya Mbunge na mmiliki wa kampuni ya New Habari Cooparation Rostam Azizi kutuma ujumbe kwa mmoja wafanyakazi wa kampuni hiyo Muhingo Rweyemamu na kuahidi kuipa timu yake shilingi milioni 2 mbali ya zawadi itakayotolewa na NSSF endapo itaifunga Uhuru Publication tangazo hilo lilipotangazwa ndipo naye Dr. Harrison Mwakyembe alipotuma ujumbe wa kuipa timu ya Uhuru Publication Shilingi milioni 6 kama wataishinda New Habari.
Mpambano wa wabunge hao haukuishia hapo naye mama Anne Kilango aliahidi kuipa Uhuru Publication Milioni 2 na hatimaye katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba aliahidi kuipa timu hiyo shilingi Milioni 1 ikiwa itachukua ubingwa ahadi hizo zilionekana kuwapa nguvu Uhuru ambao walicheza kwa kujituma na kujipatia magoli matatu kupitia kwa wachezaji wake Emanuel Mushi, Jamal Rashid na Tuzo Jackson hivyo wakajizolea milioni mbili na nusu na kikombe pamoja na shilingi milioni 9 ambazo ziliahidiwa na wabunge Dr. Harrison Mwakyembe, Anne Kilango na Yusuf Makamba na kwafanya waibuke na kitita cha shilingi milioni 11.5 goli pekee la New Habari limefungwa na mchezaji Said Makala na kuondoka na shilingi milioni 2 na kikombe, katika fainali hizo pia kwa mchezo wa netiboli zilicheza timu za Busness Printers na NSSF ambapo NSSF waliibuka mabingwa katika mchezo huo
Wachezaji wa Timu ya New Habari wakipozi na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa.
Mh.Joel Bendera akiteta na Dr. Ramadhan Dau

Mh. Joel Bendera Naibu Waziri Mkuu wa Habari Utamaduni na Michezo akikagua timu ya New Habari Cooparation kabla ya kuanza kwa kipute cha Fainali ambapo Uhuru Pablication walishinda magoli 3-1.
Mgini wa Rasmi Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera akikagua timu ya Uhuru Pablications kabla ya pambano la Fainali kati kati ni mkurugenzi wa NSSF Dr. Ramadhan Dau.

Taji Liundi mkurugenzi wa TBC International kushoto na Antony Katona wa Media Solution ambao walikuwa ni wajumbe wa kamati ya mashindano ya NSSF wakipozi kwa picha mara baada ya kumalizika kwa fainali hizo kwa mafanikio.
Nao mashabiki wa Uhuru Publications hawakuwa nyuma kuisapoti timu yao.

Mashabiki wa New Habari Cooparation wakifuatilia kwa makini mpambano wao wa fainali kati yao na Uhuru Publications katika viwanja vya TCC Chang'ombe leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment