HAWA NDIYO TMK UNITY WA KWELI, WAMWAGA NYARAKA HADHARANI!!

Hili ndiyo kundi halisia la TMK UNITY likiwa katika picha ya pamoja kuanzia kulia ni Issa Mussa, Hassan Mashaka, Nyembo Ayubu na Abdalla Rashid aliyechuchumaa, kwa habari zaidi shuka chini upate ukweli wa mambo mdau.
TMK UNITY katika pozi la mauzo si mchezo wadau

Kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Unity lenye makazi yake Wilayani Temeke limesema halitakubali mtu mwingine au kikundi chochote kitumie jina lao hilo kwani wao ndiyo wenye jina halisi na wana haki nalo kisheria.
Akizungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE meneja wa kundi hilo Bw. Ashraf Mosha amesema wao kama kundi wakati walipokuwa wakianzisha kundi lao miaka kadhaa iliyopita walijua kwamba watu wanakawaida ya kuchukua majina ya wenzao ili kufaidika kibiashara hivyo walifuata taratibu zote na wakasajiri BASATA, BRELLA na COSOTA kwa hiyo wana haki zote za kutumia jina la TMK UNITY kisheria na yeyote atakayejaribu kulitumia jina hilo ana makosa kisheria ni wizi .
Hivi karibuni wasanii wawili waliokuwa katika kundi la TMK wanaume Family Y. Dash na Y. P walitangaza katika mkutano na wanahabari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo kwamba wamejitoa katika kundi hilo na kuazisha kundi lao linaloitwa TMK UNITY kitendo ambacho kiliamsha hasira kwa wasanii wenye jina halisi la TMK UNITY na kuchukua hatua ya kwenda katika vyombo vya habari ili kuweka wazi nyaraka mbalimbali zinazowapa uhalali wa kutumia jina hilo.
Meneja huyo amewaonyesha wakuda wa FULLSHANGWE nyaraka mbalimbali zikiwemo za BASATA, BRELLA na COSOTA kitu ambacho kiliwafanya wakuda hao wa FULLSHANGWE kufunga safari mpaka COSOTA ili kujua imechukua hatua gani juu ya sakata hilo lakini waliambulia patupu baada ya kuambiwa na mmoja wa wafanyakazi wa ofisini hapo kuwa maafisa wote ambao wangetoa majibu sahihi wako nje ya ofisi kikazi.
Kundi hilo linaundwa na wanamuziki kamaIssa Mussa Sir G., Hassan Mashaka BMC, Nyembo Ayubu UB,Abdalla Rashid NEM na meneja wao Ashraf Mosha na wana Albam moja inayoitwa Haitoshi yenye nyimbo 9 ambazo ni Haitoshi yenyewe, Usione Soo, Napendwa, Kaburi la Dunia, Futi Sita, Kwenye Tv, Tulia, Paulina na Dira na tayari wana video moja inayochezwa katika vituo mbalimbali vya Redio inayoitwa Haitoshi na wana mpango wa kuingiza sokoni albam yao hivi karibuni kaeni mkao wa kula wadau

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment