MABALOZI WA MALARIA WATOA MSAADA WA VYANDARUA KWA WAJAWAZITO MWANZA!!

Mtangazaji wa Clouds FM B dozen kwa niaba ya wasanii wenzake akizungumza machache mbele ya Wazazi ndani ya wodi ya wazazi ndani ya hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure mara baada ya kuwakabidhi vyandarua leo jioni ,yote hiyo ikiwa ni kwenye mpango mzima wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa malaria iliyozinduliwa hivi karibuni ya ZINDUKA.

Shoto ni B Dozen,Young D,Rebeca kutoka kituo cha THT,Mwasiti pamoja na waja wazito katika picha ya pamoja jioni hii,mara baada ya kuwakabidhi Vyandarua vya msaada kupitia mpango mzima wa kampeni ya kupambana na malaria nchini wa ZINDUKA.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao wapo kwenye ziara ya tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,ambao pia ni mabalozi wa Malaria hapa nchini,Mwasiti pamoja na Chege wakiwakabidhi Vyandarua Muuguzi mkuu (kushoto) Bi.Eva Mudayi pamoja na afisa muuguzi wa wodi hiyo Bi Adelina jioni hii,yote hiyo ikiwa ni kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria kupitia mpango wa ZINDUKA.

Mtangazaji wa Clouds FM Hamis Mand a.k.a B Dozen akiwakabidhi Vyandarua Muuguzi mkuu (kushoto) Bi.Eva Mudayi pamoja na afisa muuguzi wa wodi hiyo Bi Adelina jioni hii,yote hiyo ikiwa ni kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria kupitia mpango wa ZINDUKA.

Mabalozi wa Malaria nchini wakiwa wamepozi picha ya pamoja na waja wazito jioni hii mara baada ya kuwakabidhi Vyandarua vya msaada kupitia mpango mzima wa kampeni ya kupambana na malaria nchini wa ZINDUKA.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment