BASI LA NAJMUNISA LAPATA AJALI NA KUSABABISHA VIFO KADHAA!!

Ajali ya Kanegele - Fuso na Super Najimunisa Kahama Mkoani Shinyanga jana kama unavyoona picha mbalimbali zilizochukuliwa eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo inayodaiwa kusababisha vifo vya watu 18 . Cha ajabu ajali imetokea mita 10 kutoka katika kizuizi cha askari wa maliasili wanaokagua mazao ya maliasili.
Katika ajali hiyo inasemekana askari aliyekuwa akisindikiza basi hilo alikatwa kicha baada ya fuso kuharibiwa vibaya na basi. hebu Jionee mwenyewe picha zilizopigwa katikaajali eneo la tukio huko Kanegele kama inavyoonekana Sura ya Basi la Super Najimunisa baada ya Ajali.(Picha na Bernard Kinte wa mtandao wa Wanabidii)
Waokoaji wakitafuta maiti ndani ya Fuso.

Eneo la ajali-Kwenye kizuizi cha Kanegele.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia ajali hiyo wakichungulia Maiti zilizopakjiwa ndani ya magari aina ya Toyota Landcruiser hardtop.

Askari wa usalama Barabarani katika eneo la ajali.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment