HAKIKA UKIONA FILAMU HII HUTOAMINI KAMA NI MIMI NIMECHEZA..... NI CRAZY LOVE (KANUMBA)

Filamu hii hata mimi mwenyewe japo nimecheza lakini naipenda sana na naisubiri kwa hamu,ni moja kati ya filamu ngumu nilizowahi kucheza na nikamudu sawia nafasi yangu, Filamu hii itakuwa mtaani mwezi ujao (wa nane) ili kunifanya nimudu vyema na kuuvaa uhusika wangu ilinichukua mwezi mzima kusoma vitabu mbalimbali vya wasomi na watu mashuhuri duniani kama vile PLATO, KARL MAX, ALEXANDER THE GREAT, SAMUEL TAYLOR nk, lakini pia Ilinibidi kuwa karibu sana na waalimu kadhaa wa vyuo vikuu ili kujua tabia zao. ili kuiweka sawa kabla ya kucheza filamu hiyo.
TAFADHALI FILAMU HII SI YA KUKOSA,PATA NAKALA YAKO ORIGINO,, FILAMU HII IKITOKA NAOMBA MNIAMBIE KWA KUNITUMIA E MAIL MBALI ILI KUNIPA MAONI KAMA MUIGIZAJI WA BONGO AMBAYE NIMEWEZA KUCHEZA UHUSIKA HUO?NINA UHAKIKA MAONI YENU YATAKUWA CHANGAMOTO KWANGU KATIKA KUCHEZA FILAMU NYINGINE NGUMU NA NZURI ZAIDI YA HII. Hapa akionekana katika taswira nyingine ya Crazy Love.
Hapa Steven Kanumba akijipa raha huko Zanzibar hivi karibuni.

Hapa ni kivazi cha jioni, akiwa amejipigilia suruali yake ya kiaina fulani kama wenzetu kutoka kule bara la Asia.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment