Kapumzike kwa amani mpiganaji mwenzetu Primtiva Pancars.!

Mume wa Marehemu Primtiva Pancras ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa kampuni ya New Habari Cooparation 2006 Bw. Joachim Mushi akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya mke wake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam,
Marehemu Primtiva alifariki juzi mkatika Hospitali ya Lugalo baada ya kuugua ghafla na kupoteza uhai wake,Marehemu atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuandika habari na makala zenye mguso kwa jamii hivyo kujipatia heshima kubwa kwa wasomaji wake ingawa alikuwa bado mchanga kwa kiasi fulani katika fani hii ya uandishi.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Primtiva Pancars AMEN.


Waombolezaji wakibeba Jeneza lililowekwa mwili wa Marehemu Primtiva Pancras tayari kwa mazishi katika makaburi ya Kionodoni leo.

Bw. Joachim Mushi ambaye ni Mhariri wa makala wa Gazeti la Jambo Leo akiuaga mwili wa marehemu mke wake Primtiva Pancras kwa majonzi makubwa wakati wa ibada ya kuaga mwili huo iliyofanyika kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni jijini Dar es salaam.
Hawa ni wakurugezni wa Gazeti la Jambo leo kulia ni Juma Pinto na kushoto ni Benny Kisaka wakishiriki katika ibada ya mazishi ya Mwandishi Primtiva Pancras, Marehemu Primtiva alikuwa ni mke wa Mwandishi wa habari na Mhariri wa makala wa Gazeti la Jambo leo Joachim Mushi.
Mpiganaji John Badi kutoka gazeti la This Day naye ameshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Primtiva, ni kweli Primtiva alikuwa mtu wa watu.

Mpiga picha wa New Habari Cooparation 2006 Anthony Siame pamoja na muombolezaji mwingine wakimsaidia mmoja wa waombolezaji aliyeshindwa kujizuia mara baada ya kuona mwili wa marehemu Primtiva Pancras na kupoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni leo.

Mdau Jerry Muro mbele kulia na mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima Absalom Kibanda nyuma pamoja na waombolezaji wengine wakiwa aktika ibada hiyo ya mazishi leo.
Mwanahabari Robert Komba ambaye ni mfanyakazi wa New Habari Cooparation 2006 kama mhariri wa Mtanzania Jumapili akiwapa pole wafanyakazi wenzie kushoto ni Mwandishi Siddy Mgumia na Mwanaharusi Pongwa ambaye pia ni mfanayakazi wa kampuni hiyo katika kitengo cha matangazo baada ya kuondokewa na kipenzi chao, mfanyakazi mwenzao Primtiva Pancras.
Ulikuwa ni wakati wa majonzi kwa ndugu na jamaa wa marehemu Primtiva Pancras wakati wa ibada ya kuaga mwili leo.
Waombolezaji na waandishi mbalimbali wakishiriki katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu Primtiva Pancras kwenye kanisa Katoliki la Hananasifu Kinondoni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment