Rais amteua Balozi Malambugi kuwa Balozi Mpya nchini Brazil!!


Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Balozi Francis Malambugi kuwa Balozi wa Tanzania Brasilia nchini Brazil .


Uteuzi wa Balozi Malambugi umefuatia kutokana na aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Balozi Daktari Joram Mkama Biswaro kuteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika.


Balozi Malambugi ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria na Mwanadiplomasia alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 1/1/1978 kama Wakili wa Serikali na amewahi kufanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Angola, Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Geneva, Ujerumani,Ethiopia na Ubelgiji.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment