Afisa Uatwala wa Klabu ya Simba Evodias Mtawala akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo leo wakati alipotangaza mkataba mpya na kocha Milovan Curkovic wa Serbia kushoto ni Cliford Ndimbo Msemaji wa klabu hiyo.
Timu ya Simba leo imetangaza kuingia mkataba mpya wa miaka miwili na kocha Mserbia Milovan Curkovic ambaye atawasili wakati wowote kuanzia sasa ili kuja kuinoa timu hiyo, awali kocha huyo aliwahi kuja nchini na kufundisha timu ya Simba kabla ya kurudi kwao Serbia kutokana na kutoelewana katika baadhi ya vipengele kwenye mkataba wake wa awali
Simba imetangaza azma hiyo baada ya kusumbuliwa mara kwa mara na kocha wao Mzambia Patrick Phiri ambaye amekuwa msumbufu kwa muda mrefu mara inapotokea anakwenda lilikizo kwao Zambia, hivyo vitendo vya kocha huyo kupelekea kuwachosha wanasimba, jambo lililofanya uongozi kufikia uamuzi wa kutafuta kocha mwingine.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi Afisa Utawala na Kaimu Katibu mkuu wa klabu hiyo Evodias Mtawala, amesema hata hivyo kabla ya yote wamemtumia barua ya kumtaka kujiuzuru Kocha Patrick Phiri kutokana na kukiuka makubaliano na klabu hiyo hivyo kuifanya klabu hiyo kuhangaika katika suala zima la mwalimu.
Wakati huohuo Mtawala amesema Simba inatarajia kufanya tamasha lake la Simba Day Agosti 8 mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru ambapo timu za Express ya Uganda zimealikwa pamoja na timu ya Azam FC ya jijini, wakati Express ikicheza na Simba siku hiyo Azam itacheza na Simba B katika mchezo mwingine katika kufanikisha tamasha hilo.
0 comments:
Post a Comment