WAFANYAKAZI WIZARA YA HABARI WAKUTANA.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Seith Kamuhanda (wa pili kutoka kulia mstari wa kwanza) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 7 wa Baraza hilo leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine Bw. Seith Kamuhanda ametoa wito kwa watumishi wa umma kuepuka ubaguzi na upendeleo katika utoaji wa huduma.

Baadhi ya wajumbe wakichangia agenda mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment