CD "Jakaya Kikwete 2010" kutoka kwao "Ngoma Africa Band" yatua nchini!!


Hayawi !Hayawi ! Sasa yamekuwa ile CD inayozungumziwa na washabiki wengi kila kona duniani Sasa imeshatua nchini .




CD hiyo yenye jina "JAKAYA KIKWETE 2010" Kutoka kwao "The Ngoma Africa Band" bendi yenye maskani yake huko Ujerumani, Sasa unaweza kupata kopi za CD hiyo kwa ANKAL Muhidin Issa Michuzi aka Mzee wa Libeneke, kwa simu 0754271266 wa blogu ya jamii.




Pia kwa yeyote yule anayetaka atumiwe mp 3 au kuweka nyimbo hizo katika mlio wa Simu za viganjani tafadhali usisite kuwasiliana na Ankal Michuzi kwa simu namba 0754271266 CD hiyo yenye muziki mtamu unaosindikiza ujumbe muhimu kwa watanzania zaidi ya milioni 40.




Hivi sasa CD hiyo ipo nchini na unaweza kupata kopi yake na kuitumia katika sherehe ,mitaani,katika biashara yako,ndani ya mabasi,harusini,sokoni n.k, ili upate raha na ujumbe uliomo katika CD "Jakaya Kikwete 2010" utunzi wake Ebrahim Makunja a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU wa Ngoma Africa Band.




Pia Jumamosi ya 31-07-2010 saa 4 asubui Ras Makunja atahojiwa na radio Free Africa ya Mwanza tafadhali tega sikio.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment