HAPPYWHITNER AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA UMODO!!

Mshindi wa shindano la UmodoHappywhitner Gumbo lililoandaliwa na blogu ya
www.umodo.blogspot.com inayoendeshwa na Taji Liundi akiwa katika picha ya pamoja na mama yake mzazi mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi jana, mwanamitindo huyo aliyeibuka kidedea kwenye shindano hilo amefanikiwa kujipatia mkataba wa mwaka mmoja kutoka kampuni ya Nywele na vipodozi ya Sheal Ilution ya jijini ambapo atakuwa akilipwa shilingi laki mbili kila mwezi hivyo zawadi yake kwa ujumla ikiwa ni milioni 2.4 pamoja na kupewa huduma za urembo katika duka hilo zenye thamani ya shilingi laki moja pia atakuwa akifanya kazi za kampuni hiyo.
Yusuph Mlela akiongea mbele ya mashabiki wa mitindo wakati wa shindano la Umodo lililofanyika jana kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View katikati ni Sylivia na mwisho ni mchezaji wa filamu Kanumba.

Na huu pia
Angalia mtindo huu wa nywele
Hawa ndiyo wanamitindo wenyewe hapa wakipiga picha kuonyesha mitindo yao ya Nywele.
Wadau Carolin kushoto na Upendo kutoka kampuni ya TSN inayochapisha magazeti ya Dairlynews na Habari leo.
Yusuph Mlela kushoto na Kanumba ndiyo walikouwa majaji katika kuwapata wanamitindo walioingia fainali ya Umodo.

Wadau Neema kushoto na Jack kutoka Sheal Ilution kampuni iliyodhamini shindano hilo la Umodo lililofanyika kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach Jana.

Wadau wa chama cha wanamitindo Tanzania wakionyesha pozi zao katika picha.

Mbunifu wa mavazi Farha, Kemi na mwanamitindo Mgesi wakiwa katika picha ya pamoja.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment