WATANI WA JADI KUSAKA POINTI WIKIENDI HII!!

Watani wa jadi Simba na Yanga.

Timu za Simba ya Jijini Dar es salaam na Yanga ya jijini pia ambao ni watani wa jadi katika mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini zinatarajia kushuka dimbani wiki hii katika viwanja tofauti ikiwa ni mfurulizo wa michezo ya Ligi kuu ya Vodacom mzunguko wa pili.
Wakati Simba itakuwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ikitifuana na timu ya Toto Afrika ya mkoani humo siku ya jumapili , Yanga itakuwa ikimenyana na timu ya Majimaji kutoka mkoani Ruvuma kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam hapo kesho siku ya jumamosi .
Afisa habari wa Timu ya Simba inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 39 akizungumza na mwandishi wa FULLSHANGWE kwa njia ya simu Cliford Ndimbo, amesema timu ya Simba imejiandaa vyema ili kuikabili timu ya Toto Africa, na wachezaji wote wako katika morali ya ushindi wa mchezo huo ili kujiwekea mazingira bora ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2009/2010, isipokuwa mchezaji Amri Kiemba ambaye ni majeruhi na amebaki Dar es salaam kwa matibabu.
Naye Msemaji wa timu ya Yanga Louis Sendeu amesema japokuwa baadhi ya magazeti yameripoti kwamba timu yake ina majeruhi sio kweli, kwani hakuna majeruhi hata mmoja na timu iko tayari kuisasambua timu ya Majimaji ya Songea ili kuhakikisha tunajiwekea mazingira mazuri ya kuwafikia wapinzani wetu Simba.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment