Aliyewahi kuwa mshauri wa Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salmin Amour Bw. Maohamed Raza akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Satrlight jijini Dar es salaam leo wakati alipompongeza Makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume kwa kukubaliana na kuendeleza uamuzi wa azimio la Butiama lililokuwa limependekeza serikali ya pamoja visiwani Zanzibar na kamati maalum ya CCM ili kudumisha amani katika visiwa vya Zanzibar.
Raza pia amempongeza katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF kwa kumtambua Rais Karume na kwamba huo ni mwanzo mzuri wa amani visiwani Zanzibar na hii ni furaha kwa wazanzibari wote, watanzania wote na jumuiya za kimataifa.
Akizungumzia kuhusu rais Karume kuongezewa muda wa urais amesema rais karume mwenyewe amekataa na amesisitiza kuwa muda wake wa kuiongoza Zanzibar umekwisha kikatiba, hata hivyo Mohamed Raza amesema kuhusu suala la kuongeza muda au kuunda serikali ya pamoja ni suala la kikatiba ambalo linahitajika kupelekwa kwa wananchi wote ili wapate muda wa kulijadili na watakalopendekeza ndilo lifanyiwe kazi kikatiba .
Pia akawataka Wawakilishi wa baraza la wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Cahama cha Mapinduzi kuwa makini na mjadala wa suala hilo, hivyo wanatakiwa kufanya maamuzi yao huku wakijua kuwa wanaiwakilisha CCM na wanachama wa chama hicho kwa ujumla
0 comments:
Post a Comment