Balozi Khamis Kagasheki Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.
Na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dodoma
ILI kukabilina na kasi ya ujambazi wilayani Ngara Wizara ya Mambo ya Ndani imeahidi kupeleaka gari la polisi litakalowasiadia kupambana na wahalifu hao.
Ahadi hiyo ya Serikali imekuja kufuatia swali la mbunge wa Ngara Prof. Feetham Banyikwa (CCM), aliloliuliza bungeni mjinini Dodoma jana na kuiomba Serikali kupeleka magari ya kutosha Ngara ili kumaliza adha ya usafiri.
Mbunge huyo alisema kuwa kuwepo kwa wimbi kubwa la ujambazi katika baadhi ya kata wilayani Ngara jambo ambalo linahatarisha usalama wa raia na mali zao.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Balozi Khamis Kagasheki alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kupeleka gari katika kituo hicho na kuahidi kupeleka gari moja kabla ya mwezi April mwaka huu.
Alisema kwa sasa wilaya ya Ngara inazo pikipiki tatu na magari mawili vifaa ambavyo havitoshelezi ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wilaya kwa kuzingatia ukubwa wa wilaya husika na jiografia yake.
Balozi Kagasheki alisema jambo jingine linaloonyesha kuwepo kwa umuhimu kwa kupeleka gari katika wilaya hiyi ni kuwepo kwa tishio la kiusalama kutokana na wilaya hiyo kupakana na nchi jirani.
Alisema Serikali itaendelea kuongeza idadi ya vitendea kazi katika vituo vya polisi kwa wilaya mbalimbali nchini kulingana na upatikanaji wa fedha kwani ni nia ya Serikali kuhakikisha kuwa hakuna tatizo la usafiri katika jeshi la polisi.
Balozi Kagasheki alisisitiza kuwa licha ya kukosekana kwa vitendea kazi madhubuti kama usafiri katika wilaya ya Ngara, Polisi mkoani Kagera wataendelea kutoa msaada kwa wilaya hiyo na kutimiza majukumu yake ipasavyo wakati Serikali ikiendelea kushughulikia suala hilo.

0 comments:
Post a Comment