Waziri mkuu mpya aanza kazi Guinea!

Jean Marie Dore waziri mkuu mpya wa Guinea.

Waziri mkuu mpya wa muda wa Guinea, mwenye jukumu la kuandaa uchaguzi utakaomaliza utawala wa kijeshi ameanza kazi rasmi.
Jean Marie Dore aliteuliwa na kiongozi aliyepo madarakani, Sekouba Konate, baada ya serikali ya kijeshi kukubali kuachia madaraka.
Dore alitoa hotuba fupi akielezea mambo aliyokusudia kutekeleza, kurekebisha jeshi la Guinea ikiwa ni jambo alilolipa kipaumbele.
Hata hivyo, hatua hiyo si jambo rahisi kwa nchi iliyodhibitiwa na jeshi kwa miongo kadhaa.
Serikali iliyopo sasa iliingia madarakani Desemba 2008 baada ya kifo cha Lansana Conte, yeye mwenyewe akiwa mwanajeshi aliyepindua serikali miaka 24 kabla ya kifo chake.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment