SIMBA YAFIKISHA POINTI 42 BAADA YA KUIBANJUA TOTOAFRICA!!

Kikosi cha Simba.
Latika mfurulizo wa michezo ya Ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba ya jijini Dar es salaam Leo ikicheza na timu ya Toto Africa ya mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba imeibanjua timu hiyo magoli 2-0 katika mchezo mkali uliochezwa jijini humo.
Timu ya simba katika kipindi cha kwanza ilitoka bila kupata goli kutokana na wachezaji wa Toto Africa kucheza kwa nguvu katika kipindi chote huku wakiikosesha raha za mapema timu ya Simba iliyokuwa ikipata upinzania kwa nguvu katika kipindi hicho.
Hata hivyo katika kipindi cha kwanza Simba iliingia uwanja kwa nguvu na ari kubwa kitu kilichopelekea wachezaji wake Muss Hassan Mgosi na Ramadhan Chombo Redondo kupachika magoli katika dakika za 50 na 54 hivyo timu hiyo kuibuka kidedea katika uwanja huo mgumu kwa timu ya Simba.
Katika mchezo wa leo Simba imejikusanyia pointi tatu muhimu hivyo kuifanya izidi kupaa katika msimmamo wa Ligi kuu ya Vodaco kwa kuwa na jumla ya pointi 42.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment