Rais Obama ahutubia Marekani!

Rais wa Marekani Barack Obama.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa katika bunge la Congress Rais wa Marekani Barack Obama amezungumzia matatizo ya kiuchumi yanayoikumba nchi hiyo.
Amekiri kuwa mpango wake wa kufufua uchumi wa Marekani haukuwapendeza baadhi ya wananchi lakini akasema hatua hiyo ilikuwa muhimu na kwamba kama haingechukuliwa ukosefu wa ajira ungeongezeka.
Amesema anaweka lengo jipya la kuimarisha soko la bidhaa za Marekani nje ya nchi.
Rais Obama pia amesisitiza nia yake ya kutekeleza mabadiliko katika sekta ya afya nchini humo.
Kuhusu sera ya kigeni,Rais Obama amezitaja silaha za nuclear kama tishio kubwa zaidi ambalo linaikabili Marekani.
Amesema kuwa juhudi za kidplomasia zinaendelea kukabiliana na tishio hilo na kuonya kuwa Iran itachukuliwa hatua iwapo itaendelea kupuuza swala la nuclear.
Rais Obama pia amezungumzia swala la kuongezwa kwa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment