ANC wakasirishwa na uamuzi wa mahakama!!

Chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress,ANC kimekasirishwa na uamuzi wa mahakama kupiga marufuku kuimba wimbo wenye maneno "Shoot the Boer" yaani "Kaburu auawe".
ANC imesema kampeni inayofanywa na wanaharakati wa kizungu kuzuia wimbo huo kutumika ni jaribio la kuwapandisha hadhi mawakala wa ubaguzi wa rangi kama wao ndio wanaodhulumiwa.
Kiongozi wa vijana wa ANC Julius Malema aliimba wimbo huo hivi karibuni, iliyosababisha kuwepo na madai ya kuchochea ghasia.
Bw Malema aliimba wimbo huo mjini Johannesburg, na kusababisha mabishano katika nchi ambapo ubaguzi wa rangi bado ni changamoto.
Katibu mkuu wa ANC Gwede Mantashe amesema chama chake kitafikisha suala hilo katika mahakama inayoshughulika na masuala ya katiba.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. hii balaa sasa.boer manaake mkulima kwa kidutch.hao makaburu waki holanzi wa regeshwe kwao kama hawatii amri maana kipindi cha aparteheid kimekwisha.hilo pia ni neno la kidutch aparteheid kuwatenganisha watu.mrudi kwenu mutuachie africa wauwaji nyie boeren.

    mdau mwenye uchungu na africa

Post a Comment