Urusi yaomboleza rasmi!!


Huku Urusi ikiwakumbuka rasmi na kuomboleza vifo vya watu 39 katika mashambulio ya kujitoa mhanga katika vituo vyake viwili vya treni mjini Moscow siku ya Jumatatu, Rais Dmitry Medvedev amewataka maafisa wa serikali kutunga sheria mpya kupambana na ugaidi.
Ametamka hayo huku Warusi wakiitenga siku ya Jumanne katika kuomboleza.
Warusi wamekuwa wakiwasha mishumaa na kuwacha maua mahali ambako milipuko hiyo miwili ilitokea.
Magazeti ya Urusi yamekuwa yakiilaumu serikali kwa kukosa kuzingatia kikamilifu suala la usalama kwa jumla.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment