Rais Bashir aonya wapinzani wake!!


Saa chache kabla ya mkutano wa viongozi wa upinzani nchini Sudan, ambapo wanatarajiwa kutangaza kuwa wanataka uchaguzi uhairishwe, Rais Omar al Bashir ameonya ikiwa watasusia uchaguzi hataruhusu kura ya moani kuhusu kujitawala kwa Sudan Kusini ifanyike mwaka 2011.
Rais Bashir ambaye amekuwa akitoa matamishi makali wiki chache kabla ya uchaguzi huo amenukuliwa na vyombo vya habari nchini humo, akitoa onyo hilo wakati wa kampeni mjini Khartoum.
Chama chake cha National Congress Party ( NCP) kinasisitiza kuwa uchaguzi lazima ufanyike Aprili 11.
Lakini vyama vya upinzani kikiwemo kile cha Sudan's People Liberation Movement (SPLM), kinachotawala kusini mwa nchi hiyo, vinataka shughuli hiyo ihairishwe.
Viongozi wa vyama hivyo wanasema hawaamini kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.
Kundi la waangalizi kutoka shirika linaloongozwa na rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, limekiri kuna matatizo mengi ya utaratibu wa kuandaa uchaguzi huo na wanaunga mkono ucheleweshwe.
Uchaguzi huo unafanyika kulingana na makubaliano ya amani yaliotiwa saini na utawala wa Khartoum na waliokuwa waasi wa SPLA mwaka wa 2005.
Kwenye makubaliano hayo, pande zote mbili pia ziliafikiana kuwa kura ya maoni ipigwe mwaka wa 2011 ili raia wa kusini mwa Sudan waamue ikiwa watajitawala.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment