Kuongezeka kwa malalamiko ya wauguzi katika Hospitali ni changamoto!

Na. Catherine Sungura,MOHSW
Kuongezeka kwa malalamiko kuhusu ubora wa huduma za afya zinazotelewa zikiwemo za uuguzi karibu mikoa yote nchini ni dalili kuwa huduma inayotolewa inakabiliwa na changamoto nyingi.
Hayo yametolewa leo jijini hapa na Waziri wa afya na ustawi wa jamii Profesa David Mwakyusa katika mkutano wa kutoa taarifa kwa wadau juu ya utekelezaji wa mpango wa kuimarisha elimu ya maadili kwa wauguzi na wakunga nchini.
Profesa Mwakyusa alisema kuongezeka kwa malamiko hayo katika sekta ya afya inatokana na wauguzi kutumia kauli mbaya,lugha isiyofaa kwa wagonjwa pamoja na kutozingatia sheria na miongozo iliyowekwa ya uuguzi hivyo kupelekea ufanisi mdogo wa fani hiyo.
“Suala la maadili ni la kudumu hivyo kila wakati lazima lizungumziwe na liwe somo la kutahiniwa katika vyuo vyetu vyote vya wauguzi ili vijana wawe na msingi mzuri wa maadili na wakazane kulisoma kama masomo ya taaluma”.
Aidha aliwasihi wale wote waliopata mafunzo wawe chumvi itakayosambaa kila mahali na kutekeleza mikakati ili huduma za afya ziwe za kurudhisha na kuboreshwa ili kuona malamiko pamoja na vifo vinavyoepukika vinapungua.
“Katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia baadhi ya malaengo yanakwamishwa na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya watendaji wenzetu, kwa kuzingatia kuwa wauguzi na wakunga ni asilimia 50 ya watoa huduma ni wajibu wenu kujituma na kutoa mchango katika kuinua hali ya afya na kuzuia vifo vinavyoweza kuepukika”malengo hayo hatatafikiwa ikiwa hakutakuwa na wauguzi waadilifu na wenye upole, aliongeza.
Hatahivyo aliseam serikali inaendelea kutoa hamasa kwa akina mama kujifungulia katika vituo vya afya na kuwakinga akina mama na watoto na ugonjwa hatari wa malaria kwa kuwapatia hati punguzo za vyandarua vilivyowekwa dawa pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu wa sekta ya afya na vituo vya kutolea huduma hadi katika ngazi za vijiji.
Jumla ya waauguzi na wakunga 304 toka kanda sita nchini ikiwemo mbeya, mtwara, moshi,morogoro, Dodoma na mwanza wamepatiwa elimu ya maadili ya wauguzi na wakunga ambayo yanaratibiwa na baraza la wauguzi na wakunga nchini na kufadhiliwa na mfuko wa uadilifu,uwajibikaji na uwazi,ofisi ya Rais,sekkretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment