WANARIADHA NA MAKAMPUNI KUSHIRIKI MBIO ZA LIVE EARTH RUN FOR WATER!!


imetajwa kua miongoni mwa moja ya miji ya kimataifa inayoshiriki katika changamoto ya kihistoria yakusaidia kutatua janga la maji ulimwenguni. Aprili 18,2010 Ndani ya masaa 24, nchi mbalimbali ulimwenguni zitashiriki katika tukio liitwalo DOW Live Earth Run For Water litakalojumuisha mfululizo wa mbio/matembezi ya km6 (km6 ni wastani wa umbali ambao wanawake na watoto wengi duniani hutembea kila siku kutafuta maji safi) zikishirikisha matamasha na shughuli zinazoelimisha masuala ya maji yanayolenga kuhamasisha mbinu za kusaidia kutatua janga la maji.
Hapa Tanzania Dow Live Earth Run for Water itajumuisha matembezi ya km6 na mbio za km15 zikianzia na kuishia nje ya uwanja mpya wa taifa ambapo mbio za kukimbiza Mwenge wa olompiki wa mwaka 2008 zilifanyikia. Mazoezi ya kupasha joto mwili yataanza saa 11:30 asubuhi, bendera ya mbio itapeperushwa saa 1asubuhi na bendera ya matembezi itapeperushwa saa 2 asubuhi. Tumepanga kuanza asubuhi na mapema ili baadae washiriki wa mbio na matembezi pamoja na watazamaji waburudike na tamasha la bure likishirikisha wasanii maarufu nchini Tanzania kama WITNESS, MH.TEMBA, CHIDI BENZ, AT, MIKE TEE na DIAMOND MUSICA. Pia kutakuwa na mfano wa vijiji vya maji kusisitizia umma juu ya uvumbuzi wa janga la maji. Tunawapa changamoto wananchi wote ,makampuni,taasi za kiserikali na zisizo za kiserikali kuungana na kuwa sehemu ya juhudi za ulimwengu za kutatua janga hili kubwa linaloathiri karibu moja ya nane ya idadi ya watu duniani.
“Janga la maji ni miongoni mwa kikwazo cha afya‘ alisema Berta Ikua-Akaunti Meneja wa Kampuni ya Spearhead Africa ‘Lakini suluhisho lipo, Tukio la Dow Live Earth Run for Water hapa Dar es Salaam ni moja ya njia ya kukusanya jamii duniani juu ya suala tete la upungufu wa maji na kuwapa wananchi uwezo na nafasi ya kuwa sehemu ya suluhisho’.
Ukosefu wa maji ni suala linaloathiri nchi,jamii na familia mbalimbali duniani kote.Mmoja kati ya watu nane hawana njia ya kupata maji safi na salama.Jamii mbalimbali barani Afrika ,Amerika ya Kusini na Asia zinakabiliwa na vifo vya watu milioni moja nukta nane kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuhara;vifo vya watoto elfu tano( 5000) kila siku kutokana na miundombinu ya maji isiyotosheleza kila sikui. Katika maeneo haya wanawake na watoto hulazimika kutembea kilomita sita (maili 3.7) kutafuta maji ambayo yamkini hayafai kwa kunywa. Hata hivyo janga hili la maji halipo katika nchi zinazoendelea tu,bali katika miji kama vile Los Angeles na Sidney. Pamoja na mambo haya yote , Mabadiliko ya hali ya hewa yanachangia kutokupatikana maji safi na salama duniani kote.
Kila mtu anahesabika katika kusaidia kutatua janga la maji. Dow Live Earth for Water ni mkakati ulimwenguni ambao unalenga kitendo cha kila mtu mmoja kua na uwezo wa kuchukua hatua kushughulikia kikamilifu suala hili. Watu wanapewa changamoto KUANZA kutatua tatizo hili leo, OKOA maji; tumia juhudi ya kuhifadhi maji kuanzia kwenye familia hadi ngazi ya jamii, TOA fedha ili kuchangia miradi ya maji safi na salama na SAIDIA kwa kushirikiana kwa njia moja au nyingine na waratibu wa tukio kuhamasisha kueneza habari nchini Tanzania kuhusu changamoto hii.
Baadhi ya miji inayoshiriki kwenye Dow Live Earth Run for Water ni Buenos Aires- Argentina,Cape Town-Afrika kusini, Chicago-Marekani, Hongkong -China, London- UK , Los Angeles-CA -USA, Melbourne -Australia, Mji wa Mexico ,Mineapolis,-Marekani, Newyork -USA,Rio de jenero- Brazil, Singapore,Stockholm -Sweden.
“Tunafuraha kutangaza kuwa Benki ya Exim Tanzania na TIGO ndio wadhamini wakuu wa Dow Live Earth Run for Water Dar es salaam”,alisema Bertha Ikua. “Ikiwa ni sehemu mojawapo ya malengo yao endelevu ya 2010, wamejitolea kutumia teknolojia kusaidia kutatua baadhi ya vikwazo vikubwa duniani kama janga la maji. Wadhamini wengine ambao tunapenda kuwashukuru ni Cool Blue, Reni International, Davis and Shirtliff, Image Masters, A1 Outdoor, Southern Sun, Hugo Domingo, What’s happening in Dar na Geita Gold Mines, ambao wamechukua hatua kuunga mkono tukio hili kubwa la ulimwenguni.
Lengo mojawapo la tukio hili ni kuwahamasisha kila mmojawetu na makampuni kuchangia kiasi chochote wanachopenda na kuwasajili wafanyakazi wao wengi iwezekanavyo kwa ajili ya mbio na matembezi na sehemu ya fedha za usajili zitazopatikana zitakwenda kwenye shirika lisilo la kiserikali liitwalo PRACTICA FOUNDATION ambalo shabaha yake ni kutengeneza vituo 20 vya maji salama (vinavyofanya kazi )kwa ajili ya watu 3000 Njombe Iringa. Asilimia mia ya michango yote itakwenda PRACTICA FOUNDATION.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment