TIMU YA TAIFA YA JUDO KWENDA NAIROBI KESHO!!


Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Nchini Idd Kipingu akimkabidhi Bendera ya Taifa Kapteni wa timu ya taifa ya Judo wakati chama cha judo nchini JATA kilipofanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea maadalizi yao na safari yao ya kwenda nchini Kenya katika jiji la Nairobi ambako mashindano ya kanda ya (5) baraza la Afrika katika mchezo wa judo yatayofanyika kuanzia 2-3 na baadaye yatafuatiwa na mazoezi ya pamoja kwa timu zote zitakazoshiriki katika mashindano hayo.
Timu inaondoka kesho alfajiri na inatarajiwa kurejea nchini tarehe 7/4/2010 na wachezaji wanaoondoka ni Omary Yusuf Ngowe, Andrew Thomas, Abuu Selemani, Athuman Abdalla na Zaidi Khamis (uzito wa kg60) wengine ni Fokas Mkude, Mohamed Korogombe, Philip Sabini (uzito kg66), Gervas Leonard, James Mapunda, Richard Martin (Uzito 73kg), Niclaus Mkinga, Gervas Taitas, Seif Malulu (Uzito81kg) na Eduward Nanda Mbambala (Uzito 90kg).
Wasichana ni Mary Francis, Latifa Mbezi (Uzito 63kg) na viongozi ni Kashinde Shaban Katibu Mkuu wa JATA na kocha wa timu hiyo Jose Valdes Silva na Hassan Mlilo Kiongozi wa Msafara, katika picha kushoto ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya judo Jose Valdes Silva.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment