TANZANIA KUPATA BILIONI 322 KUTOKA BANKI YA AFRIKA (ADB)

Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana mjini Dares salaam wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt Sipho Moyo.

Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akibadilishana hati jana jijini Dar es salaam ya makubaliano ya msaada wa kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt Sipho Moyo.

Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) imetiliana saini makubaliano ya msaada wa kifedha na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha sekta ya barabara na reli nchini.
Makubaliano hayo yataiwezesha Tanzania kupata jumla ya bilioni 322.5665 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani 235.49.
Makubaliano hayo yatiwa saini jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi Ramadhan Khijjah kwa niaba ya Tanzania na Mwakilishi Mkazi kutoka ADB Dkt . Sipho Moyo katika Ofisi za Hazina.
Katibu Mkuu huyo alisema kati ya fedha hizo kiasi cha bilioni 319 zitasaidia kuimarisha miradi ya barabara kwa ajili ya kuboresha huduma kwa ajili kuharakisha maendeleo nchini.
Khijja alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha huduma za usafiri wa barabara kati ya Iringa na Dodoma yenye kilimeta 260 na kati ya Tunduma na Namtumbo yenye kilometa 193.
Aliongeza kuwa fedha hizo pia zitasaidia kuboresha usafiri Zanzibar na kuboresha Bandari ya Mtwara ili kuboresha huduma za bandari nchini.
Khijjah alisema kuwa sehemu ya fedha hizo pia itasaidia hatua ya pili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kutoka Isaka kwenda Kigali na Keza -Musonati.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo utasaidia kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji wa mizigo ndani ya nje ya Tanzania.
Kwa upande wa Mwakilishi Mkazi kutoka ADB hapa nchini Dkt.Moyo alitoa wito kwa Serikali ya Tanzania kuharakisha utekelezaji wa masharti kwa ajili ya kukamilisha taratibu za makubaliano ya kupata mkopo huo.
Alisema kuwa kukamilika kwa hatua hizo zitasaidia Tanzania kunifaika na mkopo ambao hatimaye utasaidia kupunguza umaskini sio tu kwa Watanzania bali kuunganisha Tanzania na jirani zake.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment