Miss Arusha City Center kulindima Mei 7!

Vimwana wanaoshiriki katika shindano hilo.

Kampuni ya Sophy Entertainment ya mjini Arusha wameandaa shindano la Miss Arusha City Center linalotarajia kufanyika tarehe 7 mwezi wa tano katika ukumbi wa Naura Spring jijini humo.

Akizungumza na Full Shangwe hivi karibuni kwa njia ya simu, muandaaji wa shindano hilo, Bi. Sophia Urio alisema kuwa shindano hilo linatarajia kuwa na msisimko kwa vile linawashiriki kumi (10) wenye mvuto.

Bi. Urio alisema kuwa kwa sasa warembo hao wapo kambini wakijinoa tayari kujiandaa kwa ajili ya mashindano hayo.

Alitaka mataji yanayotarajiwa kushindaniwa na warembo hao kuwa, kutakuwa na mataji manne (4) ambayo ni kipaji, photogenic, balozi na Miss Arusha City Centre.
“Kiukweli najua mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisimko zaidi maana naona walimu wanawanoa warembo kwa kiwango cha juu zaidi,” alisema Bi. Urio.

Kwa upande wake Rachel Michael ambaye ni mwalimu wa Catwalk alisema kuwa anashukuru sana kuona warembo kuwa wana moyo wa kujituma katika mazoezi.
Nae Doreen Mecky ambaye ni mwalimu wa kucheza (dance) alisema kuwa warembo wamejifua vya kutosha na hana shaka katika kinyang’anyiro hicho.


Bi. Urio aliongeza kuwa katika shindano hilo litapambwa na msanii Prezoo kutoka nchini Kenya, Hussein Machozi pamoja na kikundi cha ngoma za asili kutoka jijini humo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Hongereni sana waandaaji!

Post a Comment