Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroers leo imeitandika bila huruma timu ya vijana wa chini ya umri huo kutoka Malawi kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo hii ambapo katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Malawi timu hizo zilitoka sare ya magoli 2 kwa 2.
Vijana wa Ngorongoro Heroers walipigana vikali kuhakikisha wanaondoka na ushindi mnono dhidi ya wamalawi hao waliokuwa wakicheza mpira wa kiwango cha juu japokuwa umaliziaji wao haukuwa mzuri mara kadhaa walipofika langoni mwa Ngorongoro Heroers.
Iliwachukua dakika tatu tu vijana wa Ngorogoro Heroers kupata goli lililofungwa na mshambuliaji machachari wa timu hiyo Omega Seme ambapo timu hiyo iliendelea kuleta madhara katika lango la Malawi na mara nyingine Thomas Ulimwengu aliipatia goli la pili timu ya Ngorongoro kabla ya kwenda mapumziko.
Katika kipindi cha pili kila timu ilijitahidi kupata goli kwa nguvu zake zote hata hivyo walikuwa ni wamalawi waliopata goli la kufutia machozi katika dakika ya tisini kwa njia ya penati iliyopigwa na mchezaji Lastin Simkonda baada ya wachezaji wa Stars kufanya mazambi langoni mwao.
Goli hilo lilipandisha hasira za Ngorongoro Heroers ambapo ilicheza vizuri katika dakika za lala salama, katika dakika ya 91 mchezaji hatari wa timu hiyo Rashid Issa Rashid aliukokota mpira mpaka wingi ya kushoto na kutoa pasi nzuri kwa Thomas Ulimwengu aliyunganisha mpira huo na kuandika goli la tatu kwa timu ya Taifa Stars Ngorongoro Heroers hivyo kufanya matokeo kuwa 3 kwa Taifa Stars na Malawi 1
0 comments:
Post a Comment