Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUAASSO) Yusuph Yahya (kulia alievaa kizibao cheusi ) leo jijini Dar es Salaa ameongea na waandishi wa habai kuhusu matatizo mbalimbali yanayokabili chuo chao.(kushoto) Makamu wake Adriano George.(Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO )
Pamoja na matatizo hayo Rais huyo wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi muhimbili MUAASSO amesifia uongozi wa chuo hicho kwa kukarabati miundombinu na kuwa ya kisasa zaidi kwa sasa jambo ambalo lilikuwa linakera na lilikuwa tatizo hapo mwanzo.
Ameongeza kuwa Majengo ya utawala, Mabweni yamejengwa mapya na kukarabati mengine vitanda vipya, meza na viti kwa ajili ya wanafuzi kukalia na kusomea vyote ni vipya "kwa kweli sasa hivi chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kinavutia manake zamani ulikuwa huwezi hata kutamani kupiga picha katika maeneo ya shule lakini sasa hivi kala mahali panapendeza kwa kupiga picha" Amesema Yusuph Yahya Rais wa MUAASSO.
0 comments:
Post a Comment