Waasi 100 wauawa nchini Chad!


Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Chad, amesema wanajeshi wa serikali wamewauawa zaidi ya waasi 100 karibu na mpaka wa nchi hiyo na Sudan katika kipindi cha siku tatu zilizopita.
Waziri wa habari nchini humo amesema mwanajeshi mmoja wa serikali aliuawa na wengine 4 walijeruhiwa kwenye makabiliano hayo kati ya jeshi la serikali na waasi wa the Popular Front for the National Rebirth F.P.R.N.

Waziri huyo alifahamisha BBC kuwa waasi hao, ambao aliwataja kama mamluki wa kigeni, wametoroka kufuatia makabiliano hayo.

Lakini msemaji wa kundi hilo la waasi amepinga takwimu hizo zilizotolewa na serikali na kusema jeshi la serikali ndilo lililoshindwa wakati wa makabiliano hayo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment