SIMBA KUWAFUATA WAARABU JUMAPILI ARFAJIRI!!

Timu ya Simba inayoshiriki katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika CAF inatarajiwa kuondoka jumapili alfajiri ikiwa na msafara wa watu 25 ikiwa ni wachezaji 20 na viongozi 5 ambapo itapiga kambi katika jiji la Cairo kwa muda kabla ya kuondoka Alhamis kuelekea Alexandria ambako itacheza mchezo wake kati yake na waarabu wa Haras el-Hodood(Sawahel) kwa jina la utani wakifundiswa na kocha mzawa Tarek El Ashry kati ya ijumaa, jumamosi au jumapili katika uwanja wa El Max Stadium.

Simba ambayo itaongozwa na Kocha wa timu hiyo mzambia Patrick Phiri na mwenye mafanikio makubwa katika timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi inawahi kwenda huko ili kuzoea hali ya hewa na kusoma mazingira ya Misri kabla ya mchezo wao huo ambapo katika mchezo wa awali kwenye uwanja wa Taifa Simba iliwafunga waarabu hao magoli 2 kwa 1 wiki iliyopita.

Ili kuendelea katika michuano hiyo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote au suluhu ili iweze kuwakilisha vyema Tanzania katika mashindano hayo, hata hivyo timu hiyo ina rekodi nzuri dhidi ya timu za misri na imekuwa ikifanya vyema mara kadhaa inapokutana na timu hizo mfano mzuri ni pale ilipoivurumusha katika michuano timu ngumu ya Zamalek ambayo ilikuwa ni bingwa mtetezi wa Klabu bingwa Afrika mwaka 2003.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment