MVUA IMETUHARIBIA PROGRAMU YA MAZOEZI, HATA HIVYO TUKO TAYARI KWA VITA!!

Kocha wa timu ya taifa Taifa stars MARCIO MAXIMO akionyesha karatasi yene majina ya wachezaji wa timu hiyo wakati alipozungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Shirikisho la mpira wa Miguu nchini TFF Karume kuhusu mchezo wa timu hiyo dhidi ya Rwanda vijana wa AMAVUBI .
Amesema kikosi hicho kipo imara kwa ajili ya mchezo huo wa kufuzu kucheza fainali za michuano ya mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN fainali zitakazofanyika nchini Sudan hata hivyo amesema mazoezi hayakuwa mazuri kutokana na mvua kunyesha bila kukatika.

Amesema licha ya mvua kuharibu programu ya mazoezi hayo lakini timu ipo safi kushinda mchezo huo.

Pia amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya mchezo ili kuwahamasisha wachezaji waweze kufanya vizuri katika mchezo huo.

Taifa Stars inacheza mchezo wa pili baada ya mchezo wa awali kushinda kwa kuifunga timu ya SOMALIA magoli sita kwa bila katika mchezo uliofanyika uwanja wa UHURU JIJINI DSM, katika picha kushoto ni Teddy Mapunda Meneja Mwasiliano na Uhusiano Serengeti Breweriers SBL ambao ndiyo wadhamini wakuu wa timu ya Taifa
Picha kwa hisani ya

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment