Wete watwaa Kombe la Muungano!!

Naibu Waziri Kiongozi na ambaye pia Waziri wa Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamhuna, akimkabidhi Kombe Nahodha wa Timu ya Wete, Ali Badru, baada ya fainali ya Kombe la Muungano linalodhaminiwa na Vodacom Tanzania, katika mchezo huo, Wete ilishinda 3-0 na kutwaa kombe hilo.
Mkurugenzi wa Masoko wa VodacomTanzania, Ephraim Mafuru akimvisha medali ya Shaba mmoja wa wachezaji wa Timu ya MUCOBA ya Mufindi baada mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano linalodhaminiwa na Vodacom Tanzania kati ya timu hiyo na Wete ya Pemba katika mchezo huo, wete ilishinda 3-0.

Wachezaji wa Wete wakishangilia ushindi wa baada kutwaa Kombe la Muungano baada ya kuikandamiza bila huruma timu MUCOBA ya Mufindi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment