Katika Hotuba ya Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida mjini alikuwa na haya machache ya kusema kwa Wanachi wake “Ndugu Zangu pamoja na mambo mengine leo hii nimekuja katika ziara ya kawaida ya kuhamasisha maendeleo ndani ya jimbo langu.
Lakini kama mtakumbuka niliwaandikia barua maafisa watendaji wa vijiji waniorodheshee majina ya mama wajawazito pamoja na watoto walio na umri chini ya miaka 5 ili nije niwapatie vyandarua vyenye dawa”.MO aliendele kusema “Ikiwa hii ni awamu ya pili kwani kwa awamu ya kwanza nilitoa Vyandarua zaidi ya 6,000 ndani ya vijiji vyetu 19 vya manispaa,mwaka 2007.
Ndugu zangu lakini mnaweza kujiuliza kwa nini nimelenga makundi haya,nimelenga makundi haya kwa sababu ugonjwa wa malaria bado unaongoza kwa kuuwa watu wengi mpaka sasa,tofauti na magonjwa mengine,Na takwimu zinaoonyesha,wanaoathirika zaidi na gonjwa hili la malaria ni mama wajawazito na watoto wenye Umri chini ya miaka 5,Takwimu zinaonyesha kuwa katika kila watoto 100 watoto watano wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria”MO alizidi kusisitiza.
Ndugu zangu sasa mimi kwa kutambua hili tatizo,nimeona bora nihamasishe jamii itambue umuhimu wa kutumia vyandarua vyenye dawa ya Kinga,nasisitiza kuwa hii ni hamasa tu,pia nawaomba viongozi wenzangu tushirikiane katika kutoa elimu juu ya matumizi ya Vyandarau”alisema MO.Mbali na MO kutoa vyandarua 6000,Kampuni ya simu za Mkononi Vodacom Tanzania Kitengo cha Vodacom Foundation kimetoa Vyandarua 10,000 jimboni kwa Mh.Mohammed Dewji hii yote ni kupambana na vita dhidi ya Malaria.
0 comments:
Post a Comment