SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA AFYA!


NA MAGRETH KINABO NA BENJAMIN SAWE – MAELEZO.

SERIKALI imesema kwamba inachukua juhudi za makusudi kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo kwa kuviboresha na kuongeza idadi ya watumishi wa kada mbalimbali. Hayo yalisemwa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Esther Nyawazwa( CCM) lililouliza kuwa hospitali ya Wilaya ya Geita inahudumia kata 33 na ina madaktari bingwa wawili na upanuzi wake unasuasua je ni lini Serikali itarekebisha matatizo hayo.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM) inachukua juhudi za makusudi kuimarisha vituo hivyo katika mwaka wa fedha wa 2010na 2011. hivyo hospitali hiyo inatarajia kupta madakatari wawili na madaktari wasaidizi watatu. Dk. Kigoda aliongeza kwamba ili kuboresha huduma za afya ziendane na ongezeko la idadi ya watu na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya. halmashauri ya wilaya ya Geita imejenga kituo cha faya cha Nyankumbu kilichopo mjini Geita na kimeanza kutoa huduma za afya. Alisema vituo viwili vya Kharumwa na Nzera vinaendelea kufanyiwa ukarabati ili kuvipanua viweze kuhudumia wagonjwa wengi zaidi.

Hata hivyo alisema kuhusu tatizo na utawala mbovu katika hospitali ya Geita Serikali inalifuatiali na kuhahakikisha watumishi wanafanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa. Hospitali hiyo ina watumishi wenye taaluma mbalimbali 218 kati ya watumishi 504 wanaohitajika sawa na asilimia 56.7.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment