MWILI WA HAYATI MZEE RASHID KAWAWA SIMBA WA VITA KUAGWA KESHO KARIMJEE!!

Hayati Mzee Rashid Kawawa.
Mwili wa Hayati Mzee Rashid Mfaume Kwawa unatarajiwa kuagwa kwenye ukumbi wa Karimjee kesho ambapo viongozi na wananchi mbalimbali watapata nafasi ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa keshokutwa Jumamosi nyumbani kwake Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaaam.
Akizungumzana wandishi wa habari jioni hii Naibu Katibu mkuu kiongozi wa Ikulu Mh George Yambesi amesema viongozi pamoja na watu mbalimbali ndugu na Jamaa wataanza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kuanzia saa nane mchana kabla ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake Madale hiyo Jumamosi
Mwili wa hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Jeshi la Wananchi Lugalo, hayati Mzee Rashid Kawawa amefariki leo asubuhi kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari

NYUMBANI KWA SIMBA WA VITA NI MAJONZI TU!!

Mbunge wa jimbo la Namtumbo Mkoani Ruvuma ambaye pia ni Mtoto wa Marehemu Mzee Rashid Kawawa Vita Kawawa akimfariji baba yake mdogo ambaye ni mdogo wa marehemu mzee Jafari Kawawa mara baada ya kuwasili nyumbani kwao Wazo Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Familia Brigedia Jenerali Francis Mbena wa kwanza kulia aliyekaa akiongoza kikao cha familia nyumbani kwa ,arehemu mzee Rashid Kawawa huko Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaam leo mchana, serikali imesema itatangaza wakati wowote juu ya taratibu za mazishi ya mwili wa Marehemu na imetangaza maombolezo ya siku saba huku bendera zikipepea nusu mlingoti.

HUU NDIYO UJUMBE WA ZITTO KABWE KWA WATANZANIA KUTOKANA NA KIFO CHA MZEE WETU RASHID MFAUME KAWAWA (SIMBA WA VITA)

Mh. Zitto Kabwe.
Leo tukiwa katika siku ya mwisho ya mwaka 2009 na tukijiandaa kuingia mwaka mpya wa 2010, tumepatwa na habari za msiba wa Kiongozi mwanzilishi wa Taifa letu Simba wa Vita Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa Mtanzania yeyote kifo hiki ni pigo kubwa sana, lakini pia ni fursa ya kukumbuka vyema historia ya Tanganyika na Tanzania. Ni fursa ya kuona Watanzania waliojitoa kuona kuwa kunakuwa na Taifa kutoka miongoni mwa nchi iliyokuwa ni mkusanyo tu wa makabila zaidi ya 120. Watu waliojitoa bila kuwa na uzoefu wowote wa si tu kuongoza serikali bali muhimu zaidi uzoefu wa kukusanya makabila, dini na wasio na dini na kuunda Taifa moja imara na la kujivunia linaloitwa Tanzania. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa ni mmoja wa watu hawa waliorithi kutoka kwa mkoloni mwingireza nchi iliyokuwa na wakazi takribani milioni 8, isiyo na chuo kikuu hata kimoja, yenye madaktari wawili tu na isiyo na mfumo kabisa. Uhai wa mzee Kawawa, kuwepo kwake na kupumua kulitupa ahueni kuwa tunapo pa kukimbilia na kujifunza kama lolote lingetokea.
Mzee Kawawa ni mfano wa kuigwa kuhusu maana halisi ya utumishi wa Umma. Alikuwa jemedari wa kutegemewa katika utekelezaji wa Dira na ajenda za kujenga Taifa bila kujali maumivu yake kisiasa. Sisi vijana tuliozaliwa miaka ya sabini mwishoni mpaka themanini hatukuona kwa jicho la kuelewa kipindi kigumu cha ujenzi wa Taifa na ujenzi wa Ujamaa nchini. Hata hivyo tulikuwa tukisikia wakubwa wakizungumza na kummlaumu sana Mzee Kawawa kutokana na utekelezaji wa sera mbalimbali kana kwamba zilikuwa ni zake na sio maamuzi ya vikao vya TANU na Serikali iliyokuwa inaongozwa na TANU. Tukiwa masomoni tumejifunza kuwa yeye ndiye alikuwa mtekelezaji mkuu wa maamuzi magumu chini ya Mwalimu Nyerere. Katika kutekeleza huku alibeba lawama za kisiasa, hakujali. Hakutikisika. Muhimu zaidi alimkinga Mwalimu Nyerere kwa yeye kubeba lawama zote za utekelezaji wa maamuzi yote ya chama. Aliweka Taifa mbele ya maslahi yake ya kisiasa. Simba wa Vita alichukulia uongozi katika mantiki ya utumishi haswa na sio katika mantiki ya sasa ya uheshimiwa. Hili ni jambo kubwa la kujifunza.
Maisha ya Mzee Kawawa Kisiasa na Kiuongozi yanawakilisha taathira ya Utanzania kwa maana ya Utu na Usawa bila ya kutumia madaraka yake kujikweza kitabaka. Watoto wa Mzee Kawawa wamesoma katika shule ambazo watoto wa Watanzania wengine wamesoma. Mimi binafsi nimesoma na binti yake anayeitwa Zainab na tulikuwa naye katika harakati za wanafunzi pale Mlimani kama mwanafunzi mwingine yeyote. Hii iliwezekana tu kwa sababu waasisi hawa wa Taifa walihakikisha kuwa shule za Umma ni bora kuweza kuelimisha Watanzania. Hivi sasa hali ni tofauti kwani viongozi tunashindana aina za shule ambazo watoto wetu wanasoma. Hii ni kwa sababu tumedidimiza shule za Umma, na kwa kuwa hazituumi ni rahisi sana kuzipuuza. Sera za kiliberali zimefanya elimu kuwa bidhaa inayouzwa katika soko. Wasisi wa Taifa hawakutaka hili kwani kama wangekuwa na fikra hizi toka mwanzoni mwa uhuru watoto wengi wa masikini ambao ndio viongozi wetu leo wasingepata elimu. Utekelezaji wa Azimio la Arusha ambalo lilitekelezwa kwa ujasiri mkubwa na Mzee Kawawa ulifungua fursa kwa watoto wote wa Tanzania bila kujali hali za wazazi wao kupata elimu na huduma nyingine za jamii. Hali ni tofauti kabisa katika nchi nyingine za Kiafrika ambapo mwenye mali ndio anapata huduma bora.
Kifo cha Mzee Kawawa ni fursa. Ni fursa ya kutafakari na kujadiliana kuhusu misingi na Dira ya Taifa letu kama ambavyo walifikiri na kuijenga wakati walipokuwa wakipigania uhuru na hata baada ya kupata Uhuru. Ni jukumu la Vijana wa sasa kuona kuwa Wazee hawa waasisi ambao ndio wanakwisha hivyo na kutangulia mbele ya haki walifanya wajibu wao - kuleta Uhuru na kujenga Taifa. Vijana wanapaswa kuhakikisha kuwa tunahodhi jukumu la kuirejesha, kuilinda na kuienzi misingi ya Taifa ya Umoja, Utu na Uzalendo kwa Taifa.
Historia inatuambia kitu kimoja kuhusu Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwamba, Kama Mwalimu Nyerere alikuwa Wino ulioandika TANZANIA, Mzee Kawawa alikuwa Kalamu. Nenda Simba wa Vita, msalimu rafikiyo kipenzi Mwalimu.

RAIS JAKAYA AKITANGAZA RASMI KIFO CHA SIMBA WA VITA IKULU LEO!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza Rasmi kifo cha Mzee Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) mapema leo, Rais pia ametangaza siku saba za maombolezo kwa nchi nzima na bendera zitapepea nusu mlingoti kwa muda wa siku hizo saba mipingo mingine ya Serikali inaendelea juu ya utaratibu wa mazishi na wakati wowopte itatangaza utaratibu huo.

AFANDE KOVA AWATAKA WAKAZI WA JIJI KUWA WATULIVU!!

Afande Sul;eiman Kova.

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wametakiwa kutokuwa na wasiwasi wakati huu wa sikukuu ya mkesha wa mwaka mpya 2010 unaofanyika leo kote duniani.
Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi kanda maalum ya mkoa wa Dar es salaam afande Suleiman Kova alipoongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, amesema wakazi wa jiji wasiwe na wasiwasi lakini pia wanatakiwa kuwa watulivu wakati wote wa sikukuu ya mwaka mpya huku wakisaidiana na polisi katika kubaini wahalifu.
Ameongea kuwa hali ni shwari na watu wasiwaache watoto wakizurura peke yao na pia waachane na vitendo vinavyoweza kupelekea uhalifu ikiwa ni pamoja na kulewa kupita kiasi na kufanya fujo mbalimbali mitaani kwani jeshi hilo limejipanga kikamilifu ili kupambana na uhalifu wowote utakaotokea wakati huu wa sikukuu.

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA KUTWANGANA KESHO UHURU!!

Mabondia Rashid Matumla (Snake Man) kulia na Joseph Marwa na (Smart Man) wakitunishiana misuli wakati walipokuwa wakitambiana baada ya kupima uzito kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo asubuhi mara baada ya kuongea na waandishi wa habari juu ya mpambano wao unaotarajiwa kupigwa kesho kwenye uwanja wa Uhuri jijini Dar es salaam.
Joseph marwa ana kilo 87 wakati Rashid matumla ana kilo 86 na pambano lao litakuwa la uzito wa 86 na litakuwa la Raundi 10 na Rashid Matumla ameshawahi kuchukua mataji ya IBU,WBU na WBA wakati Joseph Marwa amewahi kuchukua mataji ya PABA na UBO , kiingilio katika mapambo hayo kitakuwa kati ya 3000. 5000 na 10.000 waote mnakaribishwa ili kujionea masumbwi hayo mazito.

VIJANA WA KINONDONI WAJADILIANA JINSI YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI!!

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Jordan Rugimbana akizungumza wakati wa kongamano la Vijana lililoandaliwa na vijana wa Kinondoni ambapo walijadili mambo mablimbali yanayohusu Uchumi, Biashara na jinsi ya kujikwamua katika umasikini ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa SACCOS ya vijana katika wilaya hiyo, kongamano hilo lilifanyika jana kwenye ukumbi wa Manipaa ya Kinondoni.
Mbungu wa Jimbo la Kinondoni Mh. Idd Azan akizungumza katika kongamano hilo lililohudhuriwa na vijana kutoka wilaya ya Kinondoni.
Wajumbe mbalimbali wa kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Wilaya ya Kinondoni jana wakati wa kuajdili mikakati mablimbal;i ya vijana kujikwamua katika lindi la umasikini ambapo pia ulizungumziwa mkakati wa kuanzisha SACCOS ya Vijana katika Wilaya ya Kinondoni.

KAPUMZIKEA MAHALA PEMA PEPONI HAYATI MZEE RASHID MFAUME KAWAWA!!

Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa enzi za uhai wake.

Habari zilizotufikia zinasema Mzee Rashid Mfaume Kawawa Simba wa Vita amefariki dunia leo asubuhi yapata saa 3:20 asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu
Habari zilizotolewa na Daktari aliyekuwa akimtibu katika hospitali hiyo Dr. Mpoki Ulisubisya ambaye ni mkuu wa idara ya Usingizi na wagonjwa mahututi zinasema mzee Rashid Kawawa amefariki kwa ugonjwa wa kisukari na mwili wake umehamishiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya serikali na Familia kukaa kikao na kujadili kwa pamoja mambo muhimu ya kufanya kwa ajili ya msiba huu mkubwa wa kitaifa.
Mzee Kawawa ambaye alizaliwa Liwale Mkoani Lindi mwaka 1926 aliwahi kushika nyazifa nyingi Serikalini ikiwa ni pamoja na kuwa Waziri mkuu mwaka 1962 mpaka mwaka 1977 na baadae katibu mkuu wa Chama cha mapinduzi CCM kabla ya kustaafu

Rooney sets goal target

Wayne Rooney

Wayne Rooney admits he would be stunned if he failed to eclipse his best seasonal goal tally of 23.
Rooney found the net for the 15th time this season as he scored the first goal in Manchester United's 5-0 hammering of Wigan at Old Trafford on Wednesday. The result took the Red Devils to within two points of Premier League leaders Chelsea heading into 2010, just as Sir Alex Ferguson demanded.
In addition, United have clawed back Chelsea's massive goal difference advantage. Now they trail by just two, with Rooney certain he is going to get a few more.
"I would hope to beat my best total," he said. "If I don't get another eight goals from now until the end of the season there is something seriously wrong. I hit the post before I scored and the bar afterwards. I am doing well and I feel fit. Hopefully that will continue."
Following on from his superb performance at Hull on Sunday, it was another masterclass from Rooney, which drew warm praise from Ferguson. "Wayne was absolutely fantastic again, just like Sunday," said the United boss. "The energy he showed in his game and his desire is marvellous."
Even Wigan boss Roberto Martinez was purring. "Wayne Rooney has been showing great maturity for the whole season," he said. "He is among that elite group of players in the Premier League who are truly world class."
Valencia improveHowever, Rooney was not alone in excelling. Antonio Valencia in particular had a productive night against his old club, taking his own tally to seven by netting the final goal of the year after Michael Carrick, Rafael Da Silva and Dimitar Berbatov had found the net.
"Valencia is doing really well," said Rooney. "He is really quick and is aggressive getting to the ball and his crosses are brilliant. To score seven goals already is a great achievement."
Ferguson believes the Ecuador winger will get even more as the season goes on, and they will be needed too as United chase a record fourth consecutive Premier League title. Aston Villa's stumble over the Christmas period seems to have turned the title battle into a three-horse race between United, Chelsea and Arsenal, who have a match in hand. "It is fairly close at the top," Rooney added. "Arsenal are up there as well and the team who is most consistent from now on will win the league."
It was Wigan's misfortune to catch United on a night when they produced their best performance of the season so far. However, Martinez's side showed a worrying willingness to let United play and he admitted it was a bad night.
"We made it easy for them," he said. "We didn't play like a team and showed our weaknesses. You have to work as a group. We were just individuals. We have to try and get rid of that inconsistency because we are hurting."
However, Martinez declined to condemn Hendry Thomas for walking slowly off the pitch when he was substituted and refusing to shake the hand of his replacement Scott Sinclair. "There is no problem," said Martinez. "We are all frustrated and disappointed. If Hendry didn't feel hurt there would be something wrong."

Rais Kikwete amtembelea Mzee Kawawa Hospitali ya Muhimbili!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jana jioni(picha na Freddy Maro)



Kocha wa Bolton atimuliwa

Aliyekuwa kocha wa Bolton Gary Megson.

Kocha wa timu ya Bolton Gary Megson amefukuzwa kazi.
Megson alizomewa na mashabiki siku ya Jumanne baada ya timu yake kutoka sare ya 2-2 na Hull.
Megson amedai kuwa tabia kama hiyo ya kuzomewa inaathiri timu hiyo.
Meneja msaidizi Chris Evans na kocha wa kikosi cha kwanza Steve Wigley ndio watasimamia timu hiyo iliyo katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
Megson anakuwa kocha wa tatu wa ligi kuu ya England kufukuzwa kazi msimu huu, ikiwa ni siku chache baada ya Mark Hughes wa Manchester City kufukuzwa.

ILIKUWA SAME NA SASA KILOSA, HEBU TUJIHADHARI JAMANI!!

Mwezi wa nane TMA walitabiri kuwa kutakuwa na mvua za El nino zingenyesha mwezi unaofuatia oktoba lakini hazikunyesha, nadhani pengine ndo hizi, nasema pengine kwa sababu utabiri ule ulikuwa wa mwezi September na watu wengi walishaanza kupuuzia kwama huenda mvua hizo zisingenyesha tena sasa tusijekujisahau huende mvua zilizotabiriwa ndiyo hizi zilizoanza kuleta madhara maeneo mbalimbali nchini mwetu kama kule Same na Morogoro Kilosa sasa.

UNAKARIBISHA KATIKA SEMINA YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI ITAKAYOFANYIKA MIJI MBALIMBALI!

KARIBU KWENYE FURSA YA BIASHARA JE wewe ni mwajiriwa au sio mwajiriwa nani tegemezi wa KIPATO chako?JE unayo familia na wewe ndiyo kiungo chakuendesha familia?JE una watoto,ndugu na marafiki wanaokutegemea?Ikitokea bahati mbaya ukawa kilema wa maisha au Mungu amekuchukua, JE familia yako na watoto wako watalipwa na ofisi yako maisha yao yote?JE, ungependa uwaache wapo kwenye shida nakuomba misaada kwa marafiki zako?JE wewe ni mmoja kati ya watu wanaosumbuliwa na KIPATO? Au unafikiria kuwa na NYUMBA NZURI, GARI ZURI, AMANI, au KUSOMESHA WATOTO?JE unafahamu kuwa watu wengi wanamaisha duni kwa sababu tu hawana MTAZAMO sahihi wa maisha?JE unafahamu familia ngapi ambazo zinaishi kwa taabu sababu tu kiungo cha familia hiyo ambacho kilikuwa chanzo cha mkate wa siku Mungu amekipumzisha mahali pema peponi?JE una ndoto(Malengo) yoyote mwaka huu? Imekamilika au ipo mbali kukamilika? Umepanga chakufanya?Umefika wakati wakabadili mfumo(mawazo mgando) wetu wakufikiri na tutumie muda wetu kwa manufaa yetu wenyewe.
Karibu kwenye semina ya Bure itakayokupa fursa nyingine mbadala kwa kutumia muda wako wa ziada uweze kufikisha malengo yako uliyojipangia.MAHALI: DSM, ELITE CITY BUILDING 2nd Floor. ARUSHA ,BLUE ROCK HOUSE MKABALA NA GOLDEN ROSE,MWANZA PPF PLAZA SECOND FLOOR .DODOMA UKUMBI WA VETA,MBEYA FOREST HILL HOTEL ,IRINGA –KIHESA KICHANGANI STUDENT CENTREMUDA: SAA 9:00 ALASIRISIKU: JUMAMOSI NA JUMAPILIKWA WAKAZI WA ARUSHA WIKI HII TUPO IKWETA HOTEL KARIBU SANAMawasiliano:- 0719 886 193JACKIE

Obama ataka majibu kuhusu usalama

Rais Barack Obama wa Marekani.
Rais Barack Obama ametaka vyombo vya usalama vya marekani kueleza mara moja ni kwa nini habari kuhusu raia wa Nigeria aliyejaribu kulipua ndege ya marekani hazikutumiwa ipasavyo.
Bwana Obama amezipa idara za usalama hadi alhamisi tarehe 31, kueleza jinsi Umar Farouk Abdulmutallab alivyoruhusiwa kupanda ndege ya marekani wakati ambapo tahadhari ilikuwa imetolewa kumhusu.
Wazazi wa Umar walikuwa wametahadharisha ubalozi wa marekani nchini Nigeria kuhusu mwenendo wa mwana wao.
Obama ameshutumu idara hizo kwa uzembe ambao nusura ungesababisha maafa. Amesema kuwa iwapo habari kumhusu Umar zingetumiwa vilivyo na idara za usalama, raia huyo wa Nigeria hangeruhusiwa kusafiri.
Umar mwenye umri wa miaka 23 alikuwa amejaribu kulipua ndege ya Marekani iliyokuwa na abiria 300 mnamo tarehe 25 mwezi desemba.

MAANDALIZI YA KUPOKEA WAGENI WORLD CUP 2010 HAPA NCHINI YANAKWENDA VYEMA- DR.KAWAMBWA!!

Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010 Mh. Dr. Shukuru Kawambwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Wizara hiyo leo asubuhi wakati alipoelezea maandalizi ya kamati hiyo juu ya kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo.
Dr. Kawambwa amesema jumla ya shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia kampeni hiyo ikiwa ni mambo ya matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na vya kimataifa, ulinzi na kuzigharamia timu na wageni wengine baadhi ya mambo wakati watakapokuwa hapa nchini, mpaka sasa televisheni za Supersport kutoka Afrika Kusini na SunVideo kutoka Brazil ziko tayari kufanya kazi ya kutangaza mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania na maadalizi ya timu mbalimbali zitakazokuwa hapa nchini vyombo vingine ni BBC, Dautchwelle, Al jazeera VOA na vingine vingi.
Ameongeza kwamba kwa upande wa Timu ya Ivory Coast itawasili hapa nchini Januari 2 na kucheza na timu ya taifa Taifa Stars januari 4 na pia itacheza na timu ya Rwanda Januari 7 ambayo itawasili hapa nchini Januari 6 kwa ajili ya mchezo huo, waliopo kwenye picha kutoka kulia ni Dan Mrutu Kutoka Baraza la Biashara na Frolence Turuka katibu mkuu wa wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya juu
Naye Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Rodger Tenga amesema tayari wana mawasiliano na nchi nyingi zilizofanikiwa kuingia kwenye Fainali za Kombe la Dunia chini Afrika Kusini, na amezitaja nchini hizo kuwa ni Ujerumani, Italia,DenmarkNew Zealand, Brazil,Australia, Korea Kaskazini,Japan, Argelia na Nigeria na nchi zingine ambazo bado mazungumzo yanaendelea.

JOTO LA MPAMBANO KATI YA TAIFA STARS NA THE ELEPHANTS LAANZA KUPANDA!!

Bodi ya Utalii TTB ikishirikiana na Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF wameanza kampeni ya kuhamasisha umma wa watanzania kwenda kuiunga mkono na kuishangilia timu yao ya Taifa Taifa Stars wakati itakapopambana na timu ya taifa ya Cote d, Voire (Ivory Coast) katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa januari 4 kwenye uwanja wa Taifa.
Katika kampeni hii wanategemea kuweka mabango makubwa na madogo ya matangazo ikiwa ni pamoja na vipeperushi, matangazo ya redio, magazeti na televisheni pamoja na vijarida ili kuhamasisha mashabiki mbalimbali kujitokeza na kwenda kushangilia timu yao kama inavyoonekana katika kipeperushi hiki.

Clinical Torres delights Benitez

Fernando Torres.
Rafa Benitez hailed Fernando Torres as one of the best strikers in the world after his late goal against Aston Villa reignited Liverpool's UEFA Champions League hopes. The Spanish star netted his 50th league goal for the Reds in the third minute of injury time to become the fastest player to achieve a half century for the Merseysiders in his 72nd Premier League game.
Victory enabled Liverpool to reduce the gap to fourth-placed Tottenham Hotspur to four points, and moved them within two points of Villa.
"We knew we had to reduce the gap," said Benitez. "Sometimes we have had some really bad luck. Today we have scored a late goal and I'm really pleased for Fernando and the team.
It was his 50th league goal and when he signed for us I knew we were getting a very good player with good quality and a good mentality. You saw that today. He has one chance and he can score. He is one of the best strikers in the world.
When he signed for us I knew we were getting a very good player. He has one chance and he can score. He is one of the best strikers in the world.
Liverpool manager Rafa Benitez on Fernando Torres
Benitez knows the importance of keeping Torres, who has been troubled by a groin problem, fit for the majority of the campaign, although he revealed an ankle injury has also given cause for concern.
"Fernando has had some problems with his ankle more than his groin, and he has been working very hard with the fitness coach and the physio," the former Valencia coach explained. "It depends on how he feels (in terms of how many games he can play) but today he was okay."
Benitez also repeated his "guarantee" that Liverpool would finish in the top four. "People keep asking me this but I will say again, the manager has to believe and I believe we will be in the top four at the end of the season," he said.
O'Neill rues Reina savesVilla manager Martin O'Neill was deflated after his side's second defeat in three days, following the 3-0 loss at Arsenal on Sunday. And he felt the extra 24 hours Liverpool had to recover from their game against Wolverhampton Wanderers on Saturday may have been a factor.
"It's a blow, there's no doubt about it, a real, real blow to us," he rued. "We will just have to reflect on it. It was said to me that it's been a poor Christmas and, of course, yes, in terms of results it has been, but we should have won.
"We played two games in 48 hours - this sounds very much like a bleat - but at this stage of the season those extra hours might have made a difference. Having said that, I thought we finished very strongly. There was a little period about 20 minutes into the second half where I thought we got a bit of control, came again very strongly.
"Their goalkeeper (Pepe Reina) has made a great save in each half, one from Stewart Downing and one from Gabby (Agbonlahor) later on. We have had two which have gone inches past the post. It's hard to take but we will come again."

Mary Naali Hands over The Queen's Baton to President Kikwete!!

Tanzania's top Athletics gold medalist Mary Naali hands over The Queens' Baton to President Jakaya Mrisho Kikwete shorly after she arrived at Dar es Salaam State House following the 12.4Km route from Uhuru stadium to State House yestarday evening(photo by Freddy Maro)

Mapacha Africa Sauti za Busara Festival Artists 2010!!

Utilising traditional rhythms and instruments, Mapacha Africa has brought forth another dimension to popular Kenyan music. The septet traces its beginnings to western Kenya in 1989 when these seven friends were in primary school. Inspired by the sounds they heard from street musicians in their small Kenyan village, Mapacha Africa has successfully adapted these rhythms into their own mix of contemporary and traditional sound.
One of the most notable elements of Mapacha Africa's unique style is the use of a curious instrument called an adeudeu. The adeudeu, which really has no western equivalent, can be said to resemble a large boat-shaped harp, and is made from cow skin, wood and shoe strings. As one masters the instrument more and more strings can be added. One observer states that the sound that it produces is “better than the guitar”. It was this instrument, and the sense of community that it brought, that first inspired the founding members of Mapacha Africa. As the members narrate, it was common to see old men sitting and singing at the village square, an adeudeu between each pair of feet, all sharing a pot of traditional liquor.
While Mapacha Africa continued to perform in western Kenya for several years, their big break came in 2005 when they performed for Gatina Primary School in Nairobi's Kawangware area. In attendance at the event was world renowned athlete, and ambassador to the World Food Programme, Paul Tergat, who later introduced the group to Sarakasi Trust, a performing arts development organisation working toward building capacity in the arts sector in Kenya.
Working with Sarakasi Trust, the group created their first album in January 2006, entitled Angalia (meaning “Look” in Swahili). The group then went on to work with Sarakasi, performing at several festivals including the North Sea Jazz concert at Kasarani (Nairobi) in February 2006.
In March 2008, the group was invited to Holland by Mundial Productions to record their second album, Songa Yee with the band New Cool Collective. In May 2008, the group was invited back to Holland to perform at the Mundial Festival.
Mapacha group members include: Kassim Munyanya Erima, Donald Witila Mulongo, Shadrack Onyango, Isaac Sidika, John Aziz, Solomon Mwanish Kaiga, and Maurice Mala Otieno. They are now looking forwards to exposing more listeners worldwide to the adeudeu and traditional Kenyan music.

MREMA APINGA KAULI ZA VIONGOZI WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE FAUNDATION!!

Mwenyekiti wa chama cha TLP Taifa Mh. Augustino Lyatonga Mrema akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alpopinga kitendo cha Viongozi wa Tasisi ya Mwalimu Nyerere Faundation kumshutumu Rais Jakaya Kikwete kwamba utawala wake ni dhaifu na anahitaji kuchukua maamuzi mazito katika utawala wake ili kuinusuru nchi na ufisadi, hata hivyo mwenyekiti huyo wa TLP amesema kufanya hivyo ni kuhatalisha usalama wa nchi kwani kuna utaratibu wa kumkosoa rais ndani ya chama chao cha Mapinduzi CCM na kama hawawezi basi wajiunge na vyama vya upinzani ili kuendelea na shughuli za Kisiasa.

SERENGETI YAMWAGA ZAWADI KIBAO MECHI YA TAIFA STARS NA IVORY COAST!!

Meneja uhuasiano wa kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika kiwandani hapo kuhusu promosheni ya shangilia Taifa Stars inayoanza kesho wakati timu hiyo itakapocheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya Ivory Cast Januari 4 na 7 jijini Dar es salaam Ivory Coast inajiandaa na mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Angola.
Promosheni hiyo itawafanya mashabiki mbalimbali wa soka katika baa mbalimbali kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Bia za Serengeti, Kofia, Fulana na jezi za timu ya Taifa pamoja na tiketi za kuingilia katika michezo hiyo, wanaofuatia katika picha ni meneja mkuu wa kampuni hiyo Mr Kagusa, Bahati Singh meneja matukio na promosheni na mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa.
Bahati Singh Meneja Matukio na Promosheni wa SBL akifafanua jambo katika mkutano huo.


Meneja uhusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akiwa katika piocha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa walioshika jezi zenye majina yao na kulia mwisho na afisa habari wa shirikisho la mpira nchini TFF Frolian Kaijage

PONGEZI KWA LADY JAYDEE & MACHOZI BAND!!

Ni nadra sana na adimu kwa wasanii wetu kukumbuka kuwa watoto pia wanastahili kupewa burudani na kukumbukwa kipindi cha sherehe,hii ki masoko ni kitu makini na muhimu maana unawajenga watoto na kuwapa image sahihi na kuwafanya wakue na wapende muziki muziki wako ni imani yangu wale watoto watakuwa wapenzi wa baadae wa Machozi band na wataendelea kuwa mabalozi wazuri wa bendi yako wakiwa mashuleni,nyumbani etc.
Sio tu kuongeza mashabiki bali ni kuongeza thamani ya bendi na kuwapa watoto haki yao ya msingi kukutanika na kupata burudani,nakupongeza sana na kukupa big up sana kwa idea yako maana ki ukweli watoto walifurahi sana na kupata burudani fresh. Mungu akuzidishie maisha marefu na kukupa kheri katika yote,kwani maisha ni mapambano so aluta continua.
Na MDAU EDWIN TEMBA!

NAKUPA HONGERA PAPIC KWA KUIBADILISHA YANGA NA KUIPA UBINGWA WA KOMBE LA TUSKER!!

Nakupa hongera kocha Kostadin Papic wa Yanga kwa kubadilisha timu hiyo kiufundi na kuanza kucheza soka la hali ya juu tangu uichukue timu hiyo iliyokuwa ikicheza mpira na kushinda, kutoa droo ama kufungwa katika michezo yake mbalimbali lakini bila kuonyesha kiwango kizuri cha uchezaji wa mpira kama tunavyoona sasa baada ya kocha Papic kujiunga na Yanga akichukua mikoba ya kocha Kondic.
Ameonyesha kuwa ni mwalimu anayejua kusoma mchezo na kuwapa mbinu wachezaji wake ili kuweza kumkabili adui wakati wote wa mchezo hivyo kuiweka timu katika mchezo mzuri na kujituma katika kufanikisha ushindi.
Mashindano haya ya kombe la Tusker yaliyomalizika ambayo timu ya Yanga ndiyo iliyoibuka mabingwa jana yameonyesha dhahiri uwezo wa kocha huyo baada ya kutopoteza hata mchezo mmoja, huku wachezaji wakicheza kwa kuelewana karibu michezo yote mpaka kufikia fainali na hatimaye jana ukafanikiwa kuitoa timu ngumu ya Sofapaka kutoka Kenya ambayo watu wengi walikuwa wakitabiri kuwa huenda ndiyo ingechukua ubingwa wa kombe la Tusker mwaka huu 2009 baada ya timu ya Simba kufungwa na kutolewa pia na Timu ya Yanga huku ikiambilia nafasi ya tatu baada ya kuifunga Tusker ya Kenya
Kinachotakiwa sasa ni kwa uongozi wa Yanga kumpa nafasi na ushirikiano kocha Papic ili aweze kufanya kazi yake ya kufundisha timu vizuri kama alivyoianza na hatimaye tuanze mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya Vodacom kwa upinzani wa kweli wa kisoka uwanjani Hongera sana kocha PAPIC.
Kapteni wa klabu ya Yanga Abdi Kassim Baby kulia akimkabidhi kombe Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Imani Madega (katikati)katibu mkuu Laurence Mwalusako(kulia)baada ya kutwaa uchampion wa michuano ya kombe la Tusker kwa kuifunga klabu ya SOFAPAKA 2-1 katika mchezo wa fainali uliyochezwa uwanja wa Uhuru, jijini dar es Salaam.

Mashabiki wa klabu ya Yanga wakishangilia baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa huku Yanga ikishinda 2-1.


AFRICAN STARS YATAMBULISHA WATATU KUTOKA FM ACADEMIA!!

Queenb Suzy akipiga msamba katika moja ya staili zake alizozionyesha jana wakati wakati bendi ya African Stars ilipotambulisha wanenguaji watatu iliowachukua kutoka bendi ya FM Academia kwenye viwanja vya Learders jijini Dar es salaam, bendi hiyo imeendelea kujizatiti kwa kuimarisha idara mbalimbaliza bendi ili kuboresha muziki na maonyesho yake.
Asha Sharapova akionyesha mgandisho kiuno kama unayoona kwenye picha mdau.
Mnenguaji Sabrina Pazi kutoka bendi ya FM Academia akionyesha uwezo wake kwa mashabiki.
Hawa wadau wa Muziki na wanazi wakubwa wa Yanga wakihamishia furaha yao Leaders baada ya timu yao ya Yanga kuibuka mabingwa wa Kombe la Tusker kwenye uwanja wa Uhuru jana ilipoifunga Sofapaka kutoka Kenya kwenye mchezo wa fainali, kati ni Jose Mara wa FM Academia Mac Temba kulia na rafiki yao Inocent.
Mashabiki mmbalimbali wakiangalia utambulisho wa wanenguaji wapya kutoka FM Academia waliojiunga na bendi ya African Stars jana kwenye viwanja vya Leaders.

MASHABIKI WA AFRICAN STARS WASUGUA KISIGINO LANDMARK!!

Wanenguaji wa Bendi ya African Stars ya jijini Dar es salaam wakishambulia jukwaa wakati wa onyesho lao lililofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Land Mark Ubungo jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo katika kusherehekea sikukuu ya Krismass, hivi sasa bendi ya African Stars ni moja ya bendi zinazofanya vizuri sana kwenye maonyesho yake na kufanya mashabiki wengi kujitokeza katika maonyesho ya bendi hiyo ili kupata burudani, heko wana wa kutwanga na kusugua kisigino.
Mashabiki wakisugua kisigino na Twanga.
Mashabiki wakipagawishwa na wanenguaji wa bendi hiyo.
Hapa waimbaji wa Bendi hiyo wakiimba jukwaani.
Mwandishi bora wa jumla wa mwaka 2009 Jerry Murro kutoka TBC kushoto akiwa katika picha ya pamoja na mwandishi mwanadamizi wa New Habari 2006 Siddy Mgumia katikati pamoja na mwanamuziki mahiri wa bendi ya African Stars Saleh Kupaza wakati bendi hiyo ilipofanya onyesho la sikukuu ya Krismass kwenye ukumbi wa Hoteli ya Land mark Ubungo jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Jerry Murro mtangazaji wa TBC akiwa na rafiki yake mamaa Jennifer wakifuatilia kwa karibu onyesho la bendi ya African Stars wana wa Kutwanga na Kupepeta kwenye ukumbi wa LandMark usiku wa kuamkia leo katika kusherehekea sikukuu ya Krismass.

KHERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA 2010



Asia idarous alipotoa msaada kituo cha watoto yatima!

Mama mbunifu wa mavazi hapa bongo,Asia Idarous Hamsini toka Fabak Fashions jana mchana ametoa msaada wa vitu mbalimbali zikiwemo nguo,viatu na vifaa vya shule kwa kituo cha kulelea watoto yatima,kiitwacho New Life Orphans home kilichopo Kigogo jijini Dar,Mama Asia aliambatana na Mzee wa Libeneke wa Glogu ya Jamii Issa Michuzi pichani kulia wakiwa na watoto wa kituo hicho,ambao walishukuru sana kwa msaada huo.


AsiaIdarous akiwa pamoja na watoto kituoni hapo

Merry Christmas and a Prosperous New Year!

Dear Friend
I wish you a magical Festive Season filled with Loving Wishes and Beautiful Thoughts. May 2010 mark the beginning of a Tidal Wave of Love, Happiness and bright futures..

Merry Christmas and a Prosperous New Year!
God Bless You.


Aron Msigwa.

SOFAPAKA YAWABAMIZA NDUGU ZAO TUSKER 4-0!!

Timu ya Sofapaka kutoka nchini Kenya leo imeifunga timu ya Tusker pia kutoka Kenya magoli 4-0 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo.
Mchezo huo uliokutanisha ndugu wawili ulikuwa ni wa nusu fainali ya kombe la Tusker ambalo hufanyika kila mwaka hapa nchini, na kushirikisha timu za nyumbani na timu alikwa kutoka nchi jirani pia.
Ushindi huu wa timu ya Sofapaka ya Kenya unaifanya kutinga katika fainali za michuano hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa Jumapili mwishoni mwa wiki hii katika uwanja mkuu wa Taifa.
Timu hiyo hivi sasa inasubiri mshindi kati ya watani wa jadi kutoka hapa nchini Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa katika uwanja Mkuu wa Taifa kesho kuanzia saa moja jioni, hivyo timu yoyote itakayoshinda kesho kati ya Yanga na Simba ndiyo itakayocheza fainali na timu ya Sofapaka, na timu itakayofungwa kesho itakutana na Tusker kutafuta mshindi wa tatu mchezo utakaopigwa Jumamosi
Timu za Mafunzo ya Zanzibar na Mtibwa Sugar waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo tayari zimeshaaga michuano hiyo baada ya kutolewa katika hatua za awali

Jackline John anasema Merry Christmas!

Wishing you a Merry Christmas
and a Blessed 2010!!!

EAST AFRICAN BREWERIS YATIA UBANI KOMBE LA MAREALLE

Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, Bw. Aggrey Marealle akiongea na waandishi wa habari kutangaza East African Breweries Foundation kama wadhamini wa mashindano ya Chifu Marealle 2009. Kulia kwake ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Ibrahim Kyaruzi.


Taasisi ya EABL Foundation chini ya kampuni ya East African Breweries ndiyo itakuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya kombe la Chifu Marealle yanayotarajiwa kufanyika Mjini Moshi kuanzia tarehe 27 Desemba 2009 mpaka tarehe 2 Januari 2010.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masuala ya Jamii wa East African Breweries, Bw. Ken Kariuki amesema “Sisi EABL tumedhamiria kuboresha maisha ya watu hapa Afrika Mashariki katika njia endelevu”.
Mashindano haya pia yanatumika kutoa elimu kwa vijana kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi na kuwafundisha vijana jinsi ya kuishi maisha bora. "Tunaamini kuwa mashindano haya yataunganisha watu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuweka msingi imara wa vijana na maendeleo ya michezo na kuchangia kutoa elimu kuhusu Ukimwi”, alisema Kariuki.
Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waandaaji wa mashindano hayo Aggrey Marealle alisema zaidi ya timu 14 za soka, timu 7 za netiboli na timu 10 za pool kutoka wilaya za Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Siha, Hai na Vunjo zote za mkoa wa Kilimanjaro zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo yanayofanyika kwa mwaka wa tatu. Mashindano hayo yatafanyika katika kata mbalimbali za manispaa ya Moshi kama vile Pasua, Ikulu KDC, Majengo na viwanja vya George Memorial. Fainali zitafanyika katika uwaja wa MUCCOBS siku kumi baada ya uzinduzi. Timu za soka zitakazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Majengo, Bondeni, Lambo FC, Mawenzi , Kiboriloni, Korongoni, Longuo, Miembeni, Rau, Karanga, Kiyungi, Msaranga, Mji Mpya, Pasua, Soweto, Forest, Njoro, Kilimanjaro, Pasua B, Kaloleni, Langasani na Bafana Bafana

VODACOM YADHAMINI KOMBE LA MAPINDUZI!!

Naibu Waziri kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo Ali Juma Shamhuna (kushoto)akikabidhi vifaa vya michezo kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa timu ya Simba Mohamed Kajole mara baada ya kukabidhiwa na Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa kombe la Mapinduzi (katikati)Maneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Atilio Lupala.


Kampuni ya simu za mikononi Vodacom Tanzania imedhamini mashindano ya soka ya kombe la Mapinduzi kwa mwaka huu kwa zaidi ya Shilingi milioni 68.
Meneja udhamini wa Vodacom Tanzania, Emillian Rwejuna alisema kuwa udhamini huo ni wa vifaa vya michezo na fedha taslim.
Akiongea wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo na kusaini mkataba mpya wa kombe la mapinduzi kwa ZFA na kukabidhi vifaa hivyo kwa Waziri kiongozi Habari na Michezo Juma Ali Shamhuna tayari kwa ligi hiyo kuanza rasmi, alisema kuwa vifaa hivyo ni imara na vya kisasa ambavyo vinafaa katika hali ya kimchezo hapa nchini na kimataifa pia. Alisema lengo la udhamini huo ni kutaka kuendeleza michezo hapa nchini na kuweza kupata wawakilishi wazuri watakaopeperusha vyema bendera ya nchi yetu katika jukwaa la kimataifa.
Rwejuna alisema mashindano haya hujumuisha timu kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani na kushindana kama ligi zikiwa katika kundi moja, alizitaja timu hizo kuwa Simba,Yanga,Mtibwa zikitokea Tanzania bara,na Tanzania Visiwani ni Malindi,Miembeni,Mafunzo na Ocean View.
“Nae Waziri kiongozi Juma Ali Shamhuna ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliipongeza Kampuni ya Vodacom kwa kuwa kampuni inayojishughulisha na maendeleo ya Michezo hapa nchini na kuwapa changamoto makampuni mengine yaweze kujitokeza ili kuendeleza sekta hii ya michezo.
Shamhuna alisema mashindano haya yamekuwa yakifanyika kila mwaka mwezi wa kwanza kama sehemu ya kuadhimisha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kutukumbusha mazuri yaliyotokea kwa kujitawala wenyewe mnamo januari 12 1964.
Aliongeza kuwa kwa kawaida mashindano haya huanza mwezi wa kwanza na kufikia tamati tarehe 12 siku ambayo ndiyo kilele cha sherehe za Mapinduzi ambako zitafanyika Gombani Pemba.